Rafiki yangu mpendwa,
Kwa miaka saba sasa, nimekuwa najifunza, kutafiti na kuandika kuhusu maendeleo binafsi ya mtu (Personal Development).
Ni safari ngumu ambayo haijawahi kunichosha, kwa sababu ni kitu ninachokipenda na ambacho nimejitoa kukifanya kwa maisha yangu yote.
Katika kipindi hichi, nimeweza kufanya yafuatayo;
1. Nimesoma na kusikiliza vitabu zaidi ya 700 pamoja na kusoma maelfu ya makala mbalimbali.
2. Nimeandika makala zaidi ya 5000 kupitia blog mbalimbali ninazoendesha.
3. Nimeandika vitabu 15, 10 kwa mfumo wa nakala tete (softcopy) na 5 vilivyochapwa (hardcopy).
4. Nimeendesha semina kubwa za kukutana ana kwa ana 6.
5. Nimefundisha kwa karibu watu zaidi ya 500.
6. Nimewasimamia kwa karibu (coaching) zaidi ya watu 50 huku wengi wakipiga hatua kubwa.
7. Nimekuwa na ukuaji binafsi kimafanikio pia.

Katika safari hii, nimeweza kujifunza mengi kupitia wale ambao nimekuwa nawafundisha na kuwasimamia kwa karibu.
Nimeweza kuona changamoto kubwa ambazo ni kikwazo kwa mafanikio ya walio wengi.
Na kikubwa kabisa ambacho nimeona ni changamoto hizi zinajirudia kwa watu, yaani hakuna changamoto mpya, nyingi ni zile zile.
Kwa kuwasaidia baadhi ya watu kutatua changamoto zao, nimeweza kupata uzoefu mkubwa ambao unaniwezesha kuwasaidia wengine wanaopitia changamoto zinazofanana.
Sasa nakuja kwako, nikikupa nafasi ya wewe kunufaika na uzoefu huu ambao nimejijengea mpaka sasa.
Ninachotaka kwako ni nikusaidie kuweza kufika mafanikio makubwa kwenye maisha yako.
Kwa sababu ujuzi wa kukuwezesha ufike huko ninao na uzoefu wangu binafsi pamoja na wa wengine ambao wamefanikiwa tayari ninao.
Nina safari ya miaka kumi, kwenye muongo huu tuliopo sasa wa 2020 mpaka 2030.
Nimejitoa kufanya kazi na watu wachache waliojitoa kweli kufanikiwa, ambao hawakubali kukwamishwa na chochote.
Nimejitoa kufanya kazi kwa karibu mno na watu hao kwa kipindi cha miaka kumi, bila kumuacha nyuma hata mmoja.
Na safari hii imeshaanza kupitia KISIMA CHA MAARIFA.
Kama siyo mmoja wa walio kwenye safari hiyo, ninakupa nafasi ya upendeleo leo kuipata nafasi hiyo.
Safari ndiyo kwanza ipo mwanzoni, bado tuna muda mrefu mbele yetu na ambao tunaweza kufanya makubwa mno.
Hivyo karibu mno kama bado hujawa sehemu ya safari hii, karibu tuambatane kuyafikia mafanikio makubwa kwenye maisha yetu.
Kitu kimoja ninachoweza kukuhakikishia ni kwamba kama umejitoa kweli kufanikiwa, kama hukubali chochote kikurudishe nyuma, basi tukienda pamoja safari hii lazima ufanikiwe.
Lakini nisikudanganye, safari hii haitakuwa rahisi, vikwazo na changamoto lukuki zinakusubiri tu uanze safari vianze kukushambulia.
Lakini utakapokuwa kwenye njia sahihi, tukiambatana pamoja, hakuna kikwazo au changamoto yoyote itakayoweza kukuzuia au kukuangusha.
Hivyo rafiki yangu mpendwa sana, hatua pekee unayoweza kuchukua mwaka huu 2021 na mwaka 2030 ukajishukuru mno, ni kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA.
Nilishafunga dirisha la kupokea wanachama wapya kwenye KISIMA CHA MAARIFA, ila kipindi hiki cha mwanzo wa mwaka kuna wengi wameonesha nia ya kupenda twende pamoja.
Hivyo nafungua dirisha hili kwa leo, kama kweli unataka kufikia mafanikio makubwa, basi nafasi yako ni leo, chukua hatua sasa.
Najua umekuwa unanisoma kwa muda mrefu, na umeendelea kufanya hivyo kwa sababu kuna vitu unajifunza na vinakusaidia. Sasa kama unataka kwenda zaidi ya hapo ulipofika sasa, karibu ujiunge na KISIMA CHA MAARIFA.
Usifikirie mara mbili, wewe jiunge na fanyia kazi yale tunayopeana, hutajuta.
Tuma sasa ujumbe wenye maneno KISIMA CHA MAARIFA kwa njia ya wasap kwenda namba 0717396253 na utapewa maelekezo ya kujiunga.
Pia kama una mtu wako wa karibu ambaye umekuwa unaona anapitia changamoto mbalimbali kwenye maisha, mkaribishe naye ajiunge, atapata manufaa makubwa mno.
Rafiki, nafasi hii ni kwa leo tu, unaposoma hapa, chukua hatua mara moja ili usikose nafasi hii ya kipekee na baadaye ukajutia.
Nakusubiri kwa shauku kubwa, tuungane pamoja kuweza kufika kwenye mafanikio makubwa kwenye maisha yako. Tuma ujumbe sasa wenye maneno KISIMA CHA MAARIFA kwenda wasap namba 0717396253.

Rafiki, karibu upate na kusoma vitabu vizuri vya maendeleo binafsi na mafanikio kwa lugha ya Kiswahili. Pakua na weka app ya SOMA VITABU na upate maarifa sahihi. Kwa maelezo zaidi fungua; https://amkamtanzania.com/somavitabuapp
Makala Hii Imeandikwa Na Dr. Makirita Amani Ambaye Ni Daktari Wa Binadamu, Kocha Wa Mafanikio, Mwandishi Na Mjasiriamali.
Kupata vitabu na uchambuzi wa kina wa vitabu jiunge na channel ya SOMA VITABU TANZANIA kwa kufungua kiungo hiki; www.t.me/somavitabutanzania