
Hicho ni kitu ambacho kipo nje ya uwezo wako kabisa.
Lakini wengi wamekuwa wakihangaika nacho, wakitaka kuifanya dunia iende wanavyotaka wao na watu wawe vile wanavyotaka.
Hilo linaposhindikana wanaumia na kukata tamaa. Mtu pekee unayeweza kumdhibiti na kumbadili hapa duniani ni wewe mwenyewe.
Hivyo peleka nguvu zako kwenye kujibadili na kujiboresha wewe mwenyewe. Kwa kufanya hivyo, inaweza kuwavutia wengine nao wajibadili na kujiboresha na hilo litaweza kupelekea dunia iwe bora zaidi.
Yaani dunia itakuwa bora siyo kwa sababu umehangaika kuibadili, bali kwa sababu umehangaika kujibadili mwenyewe. Kazana na yale yaliyo ndani ya uwezo wako kuyaathiri, mengine achana nayo.
Wapo watu waliofikiri kwa mamlaka yao wangeweza kuifanya dunia iende watakavyo na watu wawe wanavyotaka wao, lakini walichoweza kuzalisha ni machafuko na mauaji makubwa.
Pambana na wewe mwenyewe na ukiwa bora, dunia itakuwa bora.
#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma
Asante sana kocha kwa tafakari, hakika Mambo ni mengi lakini kama Mimi ninachoweza ni kuyaishi maisha yangu kwa ubora.
LikeLike
Karibu Beatus
LikeLike
Umenikumbusha, kuweka nguvu na muda wangu katika kufanya yaliyo muhimu kwangu. Nikisha litambua hili nitaishi maisha bora yenye furaha na mafanikio makubwa.
Asante sana Kocha.
LikeLike
Vizuri Datius.
LikeLike