Rafiki yangu mpendwa,

Ukiwa unasoma vitu ambavyo wengine wanaandika, unaweza kuona uandishi ni kitu rahisi mno.

Unaweza kusoma na kuhamasika na kujiambia na wewe utaandika pia.

Hamasa hiyo inakusukuma kuandika kwa siku chache, lakini baada ya muda hamasa hiyo inazima na huku ukiwa na kazi ngumu ya kuandika mbele yako.

Hapo ndipo wengi wanapojua kweli kuandika ni kugumu, hasa mwanzoni ukiwa hujajijengea tabia ya uandishi.

Waandishi wote ambao ni wazoefu au wabobezi wanajua kitu kimoja, huwezi kuandika kwa kusubiri hamasa.

Mwandishi Steven Pressfield amewahi kuulizwa huwa anaandika kwa kusubiri hamasa au kwa kufuata ratiba. Alijibu huwa nafuata hamasa, lakini hamasa hiyo huwa inakuja kila siku saa mbili asubuhi.

Kwa upande wake, kila siku saa mbili asubuhi anakaa chini kuandika, iwe ana hamasa au hana, iwe anajisikia au hajisikii, muda wa kuandika ukifika anakaa chini na kuandika.

Na hili ndiyo limemwezesha kutoa kazi bora kabisa, hiyo ndiyo tabia ambayo waandishi wote wameweza kujijengea.

Kuna watu wengi ambao kila mwaka wanajiwekea lengo la kuandika vitabu au makala. Wanakuwa na msukumo mkubwa ndani yao, wa kutaka kushirikisha wengine maarifa na uzoefu walionao.

Wanaanza kwa siku chache lakini wanaishia njiani. Pale hamasa ya mipango inapoisha na wao ndiyo wanaishia hapo. Wanasubiri tena mpaka mwaka mwingine na kupanga hivyo.

Kama mwaka huu umepanga kuandika kitabu au chochote, basi nina habari njema kwako.

Ninakupa nafasi ya kukusimamia mpaka ukamilishe uandishi wako ndani ya mwaka huu.

Yaani ambacho nakuambia ni ndani ya mwaka huu utakamilisha kile ulichopanga kuandika. Kama ni kitabu basi kuwa na uhakika kwamba utakikamilisha ndani ya huu mwaka.

Lakini nikutahadharishe kabla hujafurahia na kuona umepata kitonga, utahitajika kufanya kazi, utahitajika kuandika kila siku na kuonesha kile ulichoandika.

Uzuri ni kwamba, kama utafuata kile nitakachokuelekeza, kama utakuwa tayari kuweka juhudi, basi mwaka huu utakamilisha uandishi wako.

Na kama utahitaji msaada zaidi kwenye kuhariri kazi yako, kutengenezewa ganda la kazi yako na hata kuchapiwa kazi hiyo, basi nitakuunganisha na watu wa uhakika ambao nimekuwa nafanya nao kazi hizo.

Ninachokuambia rafiki yangu ni hiki, kama umekuwa na msukumo wa kuandika ndani yako, basi una nafasi kubwa ya kukamilisha hilo mwaka huu, njoo tufanye kazi pamoja.

Hatua ya kuchukua ili uweze kukamilisha uandishi wako mwaka huu ni kutuma ujumbe wenye maneno NATAKA KUANDIKA MWAKA HUU kwa njia ya wasap kwenda namba 0717396253. Ukishatuma ujumbe huo utapata maelekezo zaidi ili uweze kuanza na kukamilisha uandishi wako.

Tahadhari ya mwisho kabla hujatuma ujumbe huo, usitume ujumbe huo kama ndiyo umepata wazo la kuandika baada ya kusoma hapa. Tuma kama tayari umekuwa na wazo hilo kwa muda ila huanzi au ukianza unaishia njiani. Nataka uwe tayari na moto ndani yako na kazi yangu iwe kuongeza kuni, siyo uje huna moto kabisa na mimi niwe na kazi ya kuanza kuuwasha.

Na mwisho kabisa kabisa, uwe tayari kuwekeza vitu viwili, muda na fedha. Chochote chenye thamani kwenye maisha kina uwekezaji wa muda na fedha. Usiniandikie ujumbe huo halafu uniambie huna muda au huna fedha za kukamilisha mpango huo. Kama rasilimali hizo mbili kwa sasa ni kikwazo kwako, zifanyie kazi kwanza na ukishazipata njoo nikuhakikishie kukamilisha uandishi wako.

Karibuni sana kwa wale ambao mpo tayari, nafasi ninazotoa ni chache, hivyo unapopata ujumbe huu huku ukiwa na vigezo nilivyoeleza, andika sasa ujumbe kwenda wasap namba 0717396253 wenye maelezo NATAKA KUANDIKA MWAKA HUU.

Rafiki, karibu upate na kusoma vitabu vizuri vya maendeleo binafsi na mafanikio kwa lugha ya Kiswahili. Pakua na weka app ya SOMA VITABU na upate maarifa sahihi. Kwa maelezo zaidi fungua; https://amkamtanzania.com/somavitabuapp

Makala Hii Imeandikwa Na Dr. Makirita Amani Ambaye Ni Daktari Wa Binadamu, Kocha Wa Mafanikio, Mwandishi Na Mjasiriamali.

Kupata vitabu na uchambuzi wa kina wa vitabu jiunge na channel ya SOMA VITABU TANZANIA kwa kufungua kiungo hiki; www.t.me/somavitabutanzania