Mitandao ya kijamii imewageuza watu kuwa misukule wanaofanya kazi bila kulipwa. Inawahadaa watu kwa umaarufu feki unaopatikana kwa kupost vitu vya kijinga mtandaoni.

Lakini umaarufu huo hauna manufaa kwa mtu zaidi ya kumharibia sifa yake. Umaarufu wenye manufaa ni ule unaotokana na kazi inayotoa thamani kwa wengine, ila huo unahitaji muda.

Watu wengi wanapenda njia za mkato na za haraka, hivyo hawapo tayari kuweka kazi na muda. Tatizo la njia za mkato ni kila mtu anazitumia na hivyo kwenye kupost ujinga, watu wanazidi kupost ujinga usio na ukomo.

Usikimbilie kupost ujinga ili kupata umaarufu, weka kazi inayoongeza thamani kwa wengine. Usihangaike na umaarufu, hangaika na kazi na umaarufu utakuja wenyewe kupitia thamani unayozalisha kwa wengine.

Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu umaarufu feki na halisi, fungua hapa kusoma; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/01/10/2202

#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma