
Tumeshajifunza sana manufaa ya fikra chanya, namna zinavyotuwezesha kuziona fursa zaidi na kutupa matumaini badala ya kukata tamaa.
Lakini kila lenye faida huwa pia lina hasara zake. Fikra chanya pia zina madhara kama haziambatani na matendo chanya.
Kuna watu wanakuwa na fikra chanya kweli kweli, lakini hakuna hatua zozote chanya wanazochukua. Kinachotokea ni wanajikuta wanaridhika kama vile wameshapata kile walichotaka.
Lengo la fikra chanya ni kukupa wewe msukumo wa kuchukua hatua ili upate unachotaka.
Kuwa na fikra chanya bila kuchukua hatua ni sumu kubwa kwa mafanikio yako. Ni sawa na imani bila matendo, inakuwa siyo kitu.
Kuwa chanya mara zote na chukua hatua chanya kila wakati. Kwa kila jambo jiulize ni hatua zipi chanya unachukua, kisha fanya hivyo.
Usikubali fikra chanya zikuridhishe haraka, pambana.
Ukurasa wa kusoma unahusu kusafisha akili yako, fungua; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/01/19/2211
#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma