
Ni rahisi kujipima na kushindana na wengine, lakini unapoingia tu kwenye mashindano hayo, unakuwa umejipoteza.
Mtu sahihi wa kushindana naye ni wewe mwenyewe, kila siku kuhakikisha unakuwa bora kuliko ulivyokuwa jana yake.
Wewe ndiye unayejijua zaidi, wewe ndiye unajua unataka nini na ndani yako una nini.
Kama hujajua hayo, utahangaika na mashindano yasiyo na tija kwako.
Yeyote unayetaka kushindana naye hamfanani kwa chochote, hivyo hata kama utamshinda, wewe ndiye utakuwa umeshindwa kwa sababu umeacha yako na kuhangaika na ya wengine.
Ukurasa wa kusoma ni mashindano yatakufikisha wapi, fungua; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/01/20/2212
#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma
Kila siku,kila mara hayo ni maneno ya msingi kwangu,ndiyo maana kocha mimi nimeamua ku print MWONGOZO WA KISIMA CHA MAARIFA KWA MWAKA WA MAFANIKIO 2020/2021 ,Huku nikijiwekea viwango vyangu vya kutimiza.ubarikiwe sana kocha.
LikeLike
Safi sana Beatus.
LikeLike