Kitu chochote kile ukikiangalia kwa nje, huwa kinaonekana ni rahisi kufanya na chenye manufaa makubwa. Ni mpaka uingie ndani ndiyo unakua ugumu na changamoto za kitu hicho.

Hali hii ya kuona vitu ni rahisi imekuwa kikwazo kwa wengi kupiga hatua kwa sababu unapokutana na ugumu kwenye kile ulichochagua kufanya, ni rahisi kukiacha na kwenda kwenye kile unachoona ni rahisi zaidi.

Kuna mambo mawili ya kujikumbusha hapa kwanza vitu siyo rahisi kama vinavyoonekana na pili hata vikiwa rahisi, havitakupa mafanikio makubwa.

Mafanikio makubwa hayajawahi kutoka kwenye vitu rahisi.

Ukurasa wa kusoma ni kuhusu vitu vipya na vizuri, fungua; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/01/23/2215

#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma