2274; Kushindwa kwa kujitakia…

Ukianzisha ugomvi na mtu, wewe ndiye unayeshindwa.
Kwa sababu kwenye ugomvi wowote ule, kuna kushinda na kushindwa.
Iwapo utashindwa, hapo iko wazi umeshindwa, kwa ugomvi ulioanzisha wewe mwenyewe.
Na iwapo utashinda, bado wewe ndiyo umeshindwa, kwa sababu umejishusha kwenye ngazi ya chini kwa yule uliyeshindana naye.
Hii ina maana kwamba, ushindani wowote unaoingia kwenye maisha yako, utaishia kushindwa.
Iwe ni kwenye kazi, biashara na mengine kwenye maisha, ukishaingia kwenye mashindano, maana yake umeacha njia yako na kuingia kwenye njia ya mwingine, na hapo unachopata ni kushindwa tu.
Hakuna aliye kama wewe, hakuna anayeweza kufikia viwango vyako, hivyo acha kujidhalilisha na kujipeleka kushindwa.
Mshindani sahihi kwako ni wewe wa jana.
Kila siku mpya unayoianza, pambana kuwa bora kuliko siku iliyopita, pambana kila leo uwe bora kuliko jana.
Ukimshinda wewe wa jana umepata ushindi mkubwa.
Ukimshinda mwingine yeyote umeshindwa, kwa sababu wakati unashindana umeacha kuwa wewe.
Usijiingize kwenye kushindwa kwa kujitakia.
Kocha.