2300; Kama hujafika unakotaka kufika…
Huna wakati wa anasa na mambo yasiyokuwa na umuhimu.
Kila dakika unapaswa kuiweka kwenye juhudi za kukufikisha unakotaka kufika.
Unapaswa kutumia kila fursa iliyopo mbele yako katika kufikia malengo yako.
Ushauri pekee unaohitaji katika kipindi hicho ni ule wa kukufikisha unakotaka kufika.
Sahau kuhusu mlinganyo wa maisha na kazi, sahau kuhusu matokeo yatakupa furaha au la, wajibu wako ni kupata unachotaka kwanza.
Na hilo ni deni kwako, kwa familia yako na kwa kesho yako kupata kile unachotaka.
Hivyo tumia kila wakati kuhakikisha unapata unachotaka.
Ni muhimu kujikumbusha hili muhimu kwa sababu kuna wakati tunadanganywa na kujidanganya wenyewe kwamba tulichopata kinatosha au tunachotaka siyo muhimu sana.
Kuna watu watakuambia ya nini unajisumbua sana wakati umeshapiga hatua.
Wapo ambao wataona wanajua namna gani bora unapaswa kuyaendesha maisha yako na kuanza kukushauri hayo.
Kama hutarudisha umakini wako wote kwenye kile unachotaka kufikia, utadanganyika na uishie njiani.
Hata kama watu wana ushauri mzuri kiasi gani kwako, kama hujapata unachotaka, hizo zote ni kelele, pambana kufikia unachotaka, maana hiyo ndiyo njia ya kuyaishi maisha yako na kutumia uwezo mkubwa ulio ndani yako, ambao hakuna anayeujua ila wewe mwenyewe.
Pata unachotaka au kufa ukiwa unakipambania, mengine ni kelele tu.
Kocha.
Asante kocha
LikeLike
Karibu Alex
LikeLike