Mawazo 10 ya kuingiza fedha ushonaji wa nguo.
Ufundi wa kushona nguo huwa unaonekana ni kitu ambacho kila mtu anaweza kujifunza na kufanya.
Na hivyo wengi wamekuwa hawalipi uzito hilo, wale wanaofanya hubaki wakifanya kwa mazoea na kulalamika hawawezi kuingiza kipato kwa njia hiyo.
Hapa kuna mawazo kumi ya kuingiza kipato kupitia ushonaji wa nguo.
- Kushona nguo kwa wateja mbalimbali wanaokuja kwa kutaka huduma hiyo.
-
Kushona nguo na kuziuza badala ya kusubiri watu waje kuweka oda ya kushonewa.
-
Kubuni mitindo mipya ya mavazi na kushona kisha kuuza kwa wanamitindo na wengine.
-
Kutafuta tenda za kushona kutoka taasisi mbalimbali zinazovaa sare kama shule, vyuo, hospitali n.k.
-
Kuwafundisha wengine ushonaji na wakakulipa ada.
-
Kuajiri mafundi wa kushona na kuweza kuongeza uzalishaji na kuuza zaidi.
-
Kuuza vifaa mbalimbali vya ushonaji kama vitambaa, nguzi, mashine na vifaa vyake.
-
Kuwashonea na kuwavalisha watu mashuhuri ili kupata wateja zaidi.
-
Kushona vitu tofauti na nguo, mfano mabegi ya vitambaa.
-
Kuwa na mashine na vifaa vingine unavyokodisha kwa wale ambao hawawezi kununua.
Njia nyingi tulizojifunza hapo zinahitajika mtu atoke kabisa kwenye mazoea na kufanya vitu kwa utofauti mkubwa.
Kocha.
Asante Sana kocha.
LikeLike