Maisha tayari ni mafupi, mambo ya kufanya ni mengi na muda ulionao ni mchache.

Usikubali kuyapoteza maisha yako kwa kuhangaika na mambo yasiyo na tija kwako kama kubishana.

Usihangaike na kila anayekupinga au kuamini tofauti na wewe. Hata ukihangaika kuwabadili, bado hawatabadilika.

Lakini kama jambo ni muhimu kweli, kama inabidi kweli ulibishanie basi hakikisha unauelewa upande unaobishana nao kuliko walio upande huo wanavyouelewa.

Kwa kuwa na uelewa huo wa kina utajua kwa nini wanasimama upande huo na hapo utajua namna ya kuwashawishi au ukaamua kuwapotezea hasa unapoona wameshikilia kama imani au itikadi.

Usipoteze muda wako kubishana na wenye imani au itikadi kali, haina manufaa kwako wala kwao, maana chochote utakachosema, kitazidi kuimarisha imani na itikadi zao.

Ukurasa wa kusoma ni kabla ya kubishana; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/06/03/2346

#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma