Rafiki yangu mpendwa,

Kwa miaka mitano iliyopita, tangu mwaka 2016 tumekuwa tunakutana ana kwa ana kwenye semina kubwa ya KISIMA CHA MAARIFA inayofanyika mara moja kila mwaka.

Leo ninayo furaha kubwa kukualika kwenye semina ya sita ya KISIMA CHA MAARIFA itakayofanyika mwaka huu 2021. Semina ya mwaka huu itakuwa ya tofauti kabisa na za miaka mingine na hakikisha kwa namna yoyote ile hukosi semina hii.

Kwa semina tano zilizopita tumekuwa tunakutana ndani ya jiji la Dar es salaam kwa siku moja nzima, tunapakia maarifa na hamasa ya kutosha kutusukuma kwenye safari ya mafanikio kwa mwaka mzima.

Semina ya KISIMA CHA MAARIFA ya mwaka 2021 inakwenda kuwa na tofauti kubwa nyingi, moja ni itafanyika jijini Dodoma badala ya Dar es salaam. Mbili ni semina itafanyika kwa siku mbili baada ya siku moja.

Kama semina ya siku moja ilikuwa inakupa msukumo mkubwa wa kupambana kwa mwaka mzima, hebu fikiria semina ya siku mbili itakupa msukumo mkubwa kiasi gani? Hapa ndipo inaingia ile kanuni ya mafanikio kwamba 1 + 1 = 11. Siyo mbili kama ulivyozoea kwenye hesabu, bali zaidi ya mbili, maana jumla inaongezeka kwa mkusanyiko (compounding).

Rafiki yangu ninayekupenda sana, semina ya KISIMA CHA MAARIFA 2021 siyo ya kukosa hata kidogo. Kwani hapo ndipo mahali pekee unapokutana na watu wenye kiu ya mafanikio makubwa na wanaopambana usiku na mchana kuyafikia. Kuwa ndani ya jamii ya aina hii ni bahati kubwa, kwani utapata msukumo wa kufanya makubwa bila ya kuchoka.

Baada ya utangulizi huo muhimu, karibu upate taarifa zaidi kuhusu semina ya KISIMA CHA MAARIFA 2021.

KUHUSU SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021.

Kauli mbiu ya semina ya KISIMA CHA MAARIFA 2021 ni safari ya kuelekea kwenye ubilionea.

Tarehe ambazo semina ya KISIMA CHA MAARIFA 2021 itafanyika ni siku ya Jumamosi tarehe 16/10/2021 na Jumapili tarehe 17/10/2021.

Mahali ambapo semina ya KISIMA CHA MAARIFA 2021 itafanyika ni jiji la Dodoma kwenye moja ya hoteli zilizopo kwenye jiji hilo.

Mpangilio mzima wa semina.

Siku ya kwanza ya semina utajifunza misingi muhimu ya mafanikio kwa kuanza na falsafa ya KISIMA CHA MAARIFA, kujifunza jinsi ya kulijua na kuliishi kusudi la maisha yako na kuweka na kupitia ndoto kubwa ulizonazo. Pia siku hii ya kwanza utalipata somo kuu ambalo ni safari ya kuelekea kwenye ubilionea ambapo utaijua misingi ya kuishi na mikakati ya kufanyia kazi kwenye safari hiyo. Siku hii pia utapata shuhuda za mafanikio kutoka kwa wenzetu ambao wanapambana kwenye maeneo mbalimbali.

Siku ya pili ya semina utajifunza hatua kwa hatua jinsi ya kujenga mfumo wa biashara yako ili iweze kujiendesha bila hata ya uwepo wako wa moja kwa moja. Hapa utafanya kwa vitendo kabisa na unapotoka kwenye semina na kurudi kwenye biashara yako ni kwenda kutekeleza tu. Kwenye siku hii pia utapata shuhuda za wale ambao wameshajenga mifumo ya biashara zao na kujifunza moja kwa moja kutoka kwao.

Kwenye siku za semina hii, utapata nafasi ya kukaa ana kwa ana na Kocha Dr. Makirita Amani na kwa pamoja mtalipitia kusudi la maisha yako, ndoto kubwa ulizonazo, malengo ya muongo na ya mwaka, mkakati unaokwenda kufanyia kazi kwenye mwaka wa mafanikio unaokwenda kuanza na changamoto mbalimbali unazokabiliana nazo. Kwa kupata mazungumzo haya ya ana kwa ana na Kocha, utaweza kuweka mikakati yako vizuri ambayo utaifanyia kazi mwaka mzima.

Manufaa makubwa utakayoyapata kwa kushiriki semina ya KISIMA CHA MAARIFA 2021.

Umewahi kushiriki semina mbalimbali na umekuwa msomaji mzuri na ambaye umeshajifunza mengi kwenye vitabu. Je kuna manufaa ya tofauti utakayoyapata kwa kushiriki semina ya ana kwa ana ya KISIMA CHA MAARIFA?

Jibu ni ndiyo, manufaa yapo na ni makubwa sana, hapa ni baadhi ya yale makubwa kabisa.

1. Kukutana pamoja na watu wenye mtazamo wa mafanikio makubwa kama wewe. Hakuna kitu chenye nguvu kama kukutana ana kwa ana na watu wenye mtazamo na kiu kubwa ya mafanikio. Kwani unaona inawezekana kabisa na kuwasahau wale ambao wamekuwa wanakukatisha tamaa.

2. Kupata mafunzo na mikakati yenye hatua za kuchukua kabisa ili uweze kufanya makubwa na kupata mafanikio unayoyataka.

3. Kupata hamasa kubwa ya kukusukuma kuendelea na safari ya mafanikio, hasa pale unapopata shuhuda za wengine walio kwenye safari hii. Utajionea wazi kwamba siyo wewe tu unayekutana na magumu na changamoto, hivyo hupaswi kukata tamaa.

4. Kujenga na kuimarisha mtandao wako wa kimafanikio, kwa kujuana na watu sahihi kwako, ambao unaweza kushirikiana nao kwa namna mbalimbali katika safari hii ya mafanikio.

5. Kujifunza misingi muhimu ya kuishi na kuisimamia katika safari ya kuelekea kwenye utajiri mkubwa na uhuru wa kifedha.

6. Kupata mikakati ya kwenda kutekeleza ili kuweza kufika kwenye utajiri mkubwa na uhuru wa kifedha.

7. Kupata nafasi ya kukaa ana kwa ana  na Kocha, kupitia kusudi na ndoto zako kubwa na mkakati unaokwenda kufanyia kazi kwenye mwaka wa mafanikio unaokwenda kuanza.

8. Kupata nafasi ya kufuatiliwa kwa karibu na Kocha kwa mwaka mzima. Unapotoka kwenye semina, Kocha anakuwa nyuma yako kwenye utekelezaji wa mikakati uliyojiwekea kwenye mwaka mzima wa mafanikio.

9. Kutengeneza mfumo wa kuiendesha biashara yako na kuweza kuutumia mfumo huo kwenye biashara yako moja kwa moja huku ukisaidiwa kwa karibu na Kocha.

10. Kujitambua, kujiamini na kujiheshimu baada ya kuungana na wengine wenye sifa hizo, kitu kitakachokupa nguvu ya kuendelea na mapambano zaidi.

Kwa manufaa hayo 10 na mengine mengi, hili siyo tukio la kukosa kabisa kwenye maisha yako.

Ada na utaratibu wa kulipa.

Ada ya kushiriki semina ya KISIMA CHA MAARIFA 2021 ni tsh laki mbili (200,000/=).

Ada ya kushiriki SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA itagharamia chai ya asubuhi, chakula cha mchana, chai ya jioni, vinywaji, kalamu, notebook na ukumbi ambao semina inafanyika kwa siku hizo mbili. Ada haitagharamia malazi na chakula cha jioni kwenye siku hizo za semina.

Mwisho wa kulipa ada ya kushiriki SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021 ni Ijumaa ya tarehe 01/10/2021.

Unaweza kulipa ada yako kidogo kidogo kwa wiki au mwezi kwa kadiri unavyoweza ili uwe umemaliza ndani ya kipindi cha malipo.

Sitaki chochote kiwe kikwazo kwako kushiriki semina hii, kwa sababu najua ina nguvu ya kuleta mapinduzi makubwa kwenye maisha yako.

Chagua mpango wako wa malipo, nishirikishe na uanze kuchukua hatua ili usikose semina hii ya kipekee kabisa na muhimu kwa safari yako ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa.

Nafasi za kushiriki semina.

Kwa kuwa kwenye semina ya KISIMA CHA MAARIFA 2021 nitakaa ana kwa ana na kila mshiriki kuweka na kuputia mikakati yake anayokwenda kufanyia kazi kwa mwaka mzima, kutakuwa na nafasi chache za kushiriki semina hii.

Nafasi zitakuwa 100 pekee na haitaongezeka hata moja, lengo ni niweze kumhudumia kila mtu na kumfuatilia kwa karibu kwa mwaka mzima wa mafanikio 2021/2022.

Nafasi hizi ni chache ukilinganisha na uhitaji uliopo kwenye kushiriki semina hii ya KISIMA CHA MAARIFA 2021, na zitatolewa kwa anayewahi kutoa taarifa na kukamilisha ada yake ya kushiriki semina.

Chukua hatua sasa.

Rafiki yangu mpendwa, baada ya kupata taarifa hii ya semina ya KISIMA CHA MAARIFA, chukua hatua sasa ili usikose nafasi hii muhimu sana kwenye safari yako ya mafanikio.

Chukua hatua hizi mbili muhimu sasa;

1. Tuma ujumbe wenye majina yako kamili na namba ya simu pamoja na maelezo kwamba utashiriki semina ya KISIMA CHA MAARIFA 2021 kwenda namba 0717396253, ujumbe unaweza kutuma kwa wasap au mesej ya kawaida.

2. Chagua mpango wako wa malipo na shirikisha, kama utalipa kila wiki au kila mwezi na ueleze kabisa tarehe unayopanga kulipa ili iwe rahisi kukumbushwa pale unaposahau.

Chukua hatua hizo mbili kwa sasa ili kujihakikishia nafasi ya kushiriki kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021, kama ulivyoona, nafasi ni chache hivyo usichelewe ukapoteza nafasi hii adimu.

Nafanya maandalizi makubwa ili semina ya KISIMA CHA MAARIFA 2021 iende kuwa tukio la kipekee kwako, tukio litakaloweka alama kubwa kwenye maisha yako ambayo hutokaa uisahau kamwe.

Usikubali kukosa kushiriki semina hii kwa namna yoyote ile. Taarifa ya siku ambazo semina inafanyika umeshaipata mapema, hivyo kama unahitaji kupata ruhusa ya kusafiri kuja kwenye semina Dodoma, anza kufanya maandalizi mapema ili uweze kupata ruhusa kwenye tarehe hizo.

Nakusubiri kwa hamu kubwa kwenye semina ya KISIMA CHA MAARIFA 2021 tarehe 16 na 17 Oktoba 2021 ndani ya jiji la Dodoma Tanzania. Karibu sana tujumuike pamoja kwenye tukio hilo kubwa na la kipekee kabisa kwenye safari yako ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa.

Rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,

Kocha Dr Makirita Amani.

0717 396 253