Siyo yule anayeongea sana, bali yule anayekaa kimya.

Anayeongea sana anaweka kila kitu wazi kuhusu yeye, hivyo unaweza kujua mipango yake na kujiandaa mapema.

Anayekaa kimya hujui anapanga nini na huwezi kujiandaa kwa ajili yake.

Hivyo hofia zaidi wale wanaokaa kimya kuliko wanaoongea sana.

Lakini pia wapo wanaoongea sana kama njia ya kukuhadaa, usijue dhamira zao halisi, hivyo kuwa makini pia.

Na kwa upande wako, usiwe mtu wa kusema kila kitu, kuweka kila kitu hadharani.

Kadiri wengi wanavyojua kila kitu kuhusu wewe ndivyo wanavyokuchukulia poa zaidi.

Ukurasa wa kusoma ni nini unachoficha; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/06/06/2349

#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma