2417; Maamuzi ya kufa na kupona…
Kuna maamuzi machache sana ambayo ukiyafanya kwenye biashara ni ya kufa na kupona.
Kwa maana kwamba kuna hatari ya biashara kufa kabisa.
Lakini maamuzi hayo ni machache mno.
Maamuzi mengine mengi, pamoja na ugumu na umuhimu wake, yanaweza kurekebishika tu.
Funzo ni nini hapa?
Usichelewe kufanya maamuzi ya kibiashara kwa sababu unaogopa kukosea.
Fanya maamuzi, hata kama utakosea una nafasi ya kurekebisha.
Lakini pia una fursa ya kujifunza zaidi kupitia maamuzi uliyokosea kuliko kutokufanya maamuzi kabisa.
Ni mtazamo huu ndiyo utakaokuwezesha kuendana na kasi ya madabiliko ya kibiashara na kujitofautisha na wengine.
Fanya maamuzi,
Tengeneza changamoto mpya kwenye biashara,
Zitatue,
Songa mbele.
Kocha.
Asante Sana kocha kwa makala hii nzuri. Kukwepa kufanya maamuzi kwa kusingizio cha kuogopa kushindwa ni kujizuia kukua kitu ambacho ndiyo muhimu zaidi kwa mtu.
LikeLike
Karibu Tumaini.
LikeLike