Rafiki yangu mpendwa,
Mitandao ya kijamii ilikuwa sehemu ya kistaarabu sana kabla ya kugunduliwa kwa kitufe cha like.

Enzi hizo watu waliingia mwenye mitandao ya kijamii kuwasiliana na wale wanaowajua na kupata taarifa mbalimbali.

Lakini baada ya kuja kwa kitufe cha like, mitandao hiyo imebadilika.
Imeacha kuwa sehemu nzuri ya kukutana na kugeuka kuwa mashindano ya kitoto.

Na kikubwa ambacho watu wanashindania na kujilinganisha na wengine ni idadi ya wafuasi na likes ambazo mtu anapata.

Hili la kutaka wafuasi na likes nyingi limewasukuma watu kufanya mambo ya kijinga na yanayowadhalilisha sana.
Watu wamekuwa tayari hata kuweka picha na maudhui yasiyo na maadili ili tu kupata wafuasi na likes nyingi zaidi.

Kwenye kitabu cha EPUKA UTUMWA WA KIDIJITALI, nimeeleza kwa kina sana jinsi ambavyo ujio wa kitufe chs like ulivyowajengea watu uraibu wa matumizi ya mitandao hiyo.
Nimekuonyesha madhara makubwa ya mitandao hiyo ya kijamii na namna inakuwa kikwazo kwako kuwa na utulivu na kuweza kufanya makubwa.

Katika kukusaidia kuondoka kwenye utumwa wa mitandao ya kijamii, nilikupa vigezo vitatu vya kupima, yaani utumie mtandao pale tu vigezo hivyo vitatu vinakuwepo.

Hapa nitazungumzia kigezo kimoja, vingine viwili utaweza kuvisoma kwenye kitabu cha EPUKA UTUMWA WA KIDIJITALI, ambacho unakipata kwa kuwasiliana na 0752 977 170.

Badala ya kuhangaika na idadi ya wafuasi na likes kwenye mitandao ya kijamii, hangaika na kitu hiki kimoja, kiasi cha fedha unacholipwa.

Angalia ni kiasi gani cha fedha unachoingiza kwa matumizi yako ya mitandao ya kijamii.
Kama unaitumia kila siku na huingizi kipato chochote basi jua umejiweka kwenye upande wa kupoteza.

Uzuri ni wapo wanaolipwa kwa matumizi yao ya mitandao hiyo hivyo na wewe unaweza kulipwa pia.
Kama huingizi kipato kwa mitandao siyo kwa sababu huwezi, ila kwa sababu hujui.

Una bahati ya kipekee sana kwani leo unakwenda kujua kile usichojua na uweze kuingiza kipato kwa matumizi yako ya mitandao ya kijamii.

Na hapo huhitaji kuhangaika na wafuasi au likes, bali unapaswa kuhangaika na kitu kimoja kikuu.

Kitu hicho kimoja nimekieleza kwa kina kwenye sura ya pili ya kitabu kipya nilichotoa kinachoitwa SIMU YANGU OFISI YANGU.

Kwenye sura ya kwanza ya kitabu hicho nimekupa msingi muhimu na sura ya pili inayo nguzo muhimu.
Ukiielewa nguzo hiyo na kuifanyia kazi, hutahangaika tena na wafuasi au likes, bali utakuwa bize sana kukusanya pesa huko mtandaoni.

Na hili sitanii, kwa sababu kuna watu watakuwa wamekubana sana uwape vitu fulani kiasi kwamba hutapata muda wa kuhangaika na mengine.

Pata leo kitabu cha SIMU YANGU OFISI YANGU na uanze kunufaika kifedha kwa matumizi ya simu yako kwenye mtandao wa intaneti na mitandao ya kijamii.

Kupata kitabu hiki kizuri ambacho hupaswi kukubali ukikose kwa namna yoyote ile, wasiliana na 0717 396 253.

Rafiki yako anayekupenda sana,
Muuza Matumaini Kocha Dr Makirita Amani
http://www.somavitabu.co.tz