
Ukisikia tu kuna kitu rahisi na kinakipa sana, mbio unakimbilia kukifanya. Kwa kuwa wengi wanapenda urahisi, mnajikuta wengi mpo kwenye kitu hicho, ushindani unakuwa mkali na wengi hamnufaiki.
Mnasikilizia tena wapi ni rahisi, na kupakimbilia. Miaka inaenda unashangaa hupigi hatua kubwa. Unajiona labda una bahati mbaya, lakini tatizo ni moja, unahangaika na mambo rahisi.
Hebu achana na hayo rahisi na uone jinsi utapiga hatua kubwa. Angalia tatizo au changamoto watu wanayo na ni ngumu kutatua hivyo wengi wanaikimbia, kisha wewe weka juhudi kwenye hilo, toa thamani ya kweli na utapiga hatua kubwa.
Ukurasa wa kusoma ni kuanzia chini siyo rahisi; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/08/12/2416
#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma
Asante Sana kocha.
LikeLike