#SheriaYaLeo (115/366); Epuka muungano wa uongo.

Hakuna mtu anayeweza kufanikiwa peke yake kwenye maisha bila ya kuungana na wengine.
Tunategemeana sana katika safari ya maisha na mafanikio.

Lakini siyo kila muungano una manufaa kwako.
Kuna muungano wa uongo na muungano wa kweli.
Unapaswa kujua tofauti za aina hizo za muungano ili uchague ulio sahihi.

Muungano wa uongo ni ule unaojengwa kwenye mahitaji ya haraka ya kihisia.
Muungano huu unakutaka uache kuwa wewe na utegemee wengine kwa kila kitu.
Muungano wa aina hii unakuzuia wewe kufanya maamuzi yako mwenyewe.
Muungano huu unakunyima huru na kukufanya uwe tegemezi kwa wengine.

Muungano wa kweli unajengwa kwenye manufaa ya pande zote.
Kila upande ukitoa kile ambacho upande mwingine hauna na kupata kile ambacho hauna.
Muungano huu siyo wa kihisia na haukutaki uache kuwa wewe.
Badala yake unakuweka huru kuwa wewe na kuishi utofauti wako, maana ndiyo wenye manufaa kwa upande mwingine.

Sheria ya leo; Jenga muungano wa kweli. Tafuta wale ambao unaweza kuwanufaisha na wao wakakunufaisha bila ya kuwa tegemezi kwa kila kitu. Pamoja na kuungana na kushirikiana na wengine, uhuru wako ni kitu kikubwa sana, usikubali kuupoteza kwa namna yoyote ile.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji