#SheriaYaLeo (315/366); Vuka ukabila.
Ukabila una mizizi ndani ya asili ya binadamu. Ulitusaidia sana kipindi ambacho usalama wa mtu ulitegemea sana kuwepo ndani ya kundi.
Kuwa nje ya kundi ilikuwa hatari kubwa kwa maisha ya mtu yeyote.
Lakini kwa sasa mambo yamebadilika, hali ya usalama ni kubwa na hakuna hatari ya kuwa nje ya kundi.
Na pia mabadiliko makubwa ya kiteknolojia ambayo tumeyafikia, yamefanya hali ya ukabila kuwa hatari sana.
Kwani kuendekeza ukabila kwenye zama hizi za teknolojia kunaweza kuwa hatari kubwa kwa wale wanaojitenga na wengine.
Tunapaswa kujua sisi sote ni binadamu, kundi moja ambalo tunafanana kuliko tunavyotofautiana.
Binadamu wote ni kitu kimoja. Tofauti tunazozitumia kujigawa ni vitu vya kutengeneza tu.
Hivyo tunapaswa kushirikiana kama binadamu wote na kuepuka hali ya ukabila ya kujigawa kwenye vikundi na kuamini vikundi vyetu ni bora kuliko wengine.
Ushirikiano wetu kama binadamu una nguvu kubwa ya kuleta matokeo bora na ya kibunifu.
Sheria ya leo; Tunapaswa kukubali kwamba kundi kuu ambalo tupo ndani yake ni jamii ya binadamu. Kujiweka kwenye makundi mengine yanayowagawa binadamu ni ukabila ambao ni hatari sana kwenye zama hizi.
#NidhamuUandilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji