2813; Kwanza umefanya?
Huwa ni rahisi kuyaangalia matokeo na kukatishwa nayo tamaa pale yanapokuwa tofauti na mategemeo.
Lakini mtu unasahau kwamba matokeo yoyote yale huwa hayaji kimiujiza.
Bali yanaathiriwa na kile ambacho mtu amefanya.
Hivyo kabla hujaumizwa na matokeo, kwanza jiulize umefanya?
Je umefanya kile unachopaswa kufanya?
Kama jibu ni ndiyo umefanya, kuna swali jingine linalofuata ambalo ni umefanya kwa msimamo kiasi gani?
Kufanya mara moja au chache ni rahisi, lakini hizo haziwezi kuleta matokeo kamwe.
Kufanya kwa msimamo bila kuacha ndiyo njia ya uhakika ya kupata matokeo mazuri.
Kwa maana hiyo basi, tunaweza kusema hakuna kushindwa kama unafanya.
Maana kufanya kwa msimamo bila kuacha ndiyo kujiweka kwenye uhakika wa kupata kile unachotaka.
Kushindwa ni pale unapoacha kufanya.
Kama unaendelea kufanya hujashindwa, ni wakati tu wa matokeo haujafika.
Hatua ya kuchukua;
Hakikisha mara zote unafanya kile unachopaswa kufanya. Fanya kwa msimamo bila kuacha. Matokeo unayopata yasikukatishe tamaa, wewe endelea kufanya.
Tafakari;
Kukaa kwenye kufanya kunakuweka kwenye fursa ya kupata matokeo mazuri kuliko kutokufanya.
Ni bora ufanye chochote kuliko kutokufanya kabisa.
#LetsBuildBusinesses
#NothingElseMatters
#BillionairesInTraining
#WeAllGonnaMakeIt
#WorkHardAndYouWillSucceed