#SheriaYaLeo (343/366); Ungana na kitu kikubwa kuliko wewe.

Mara nyingi changamoto tunazokutana nazo kwenye maisha huwa zinatupa msongo na hata sonona.
Hilo huweza kututikisa kwa kiasi kikubwa na kutuzuia kufanya makubwa tunayotaka.

Njia ya kuondoka kwenye hali hizo ni kuungana na kitu kikubwa kuliko wewe.
Kwenye maisha yako kuna kipindi umewahi kuwa kwenye hali nzuri na ya ukamilifu kabisa.
Inaweza kuwa wakati wa utoto, ujana au wakati mwingine ambapo kila kitu kilikuwa kinaenda sawa.

Wakati unapopitia hali ngumu ndiyo unapaswa kuunganika na hali hizo zilizokuwa nzuri kwako.
Jione ukiwa ndani ya hali zilizokuwa nzuri kwako na hilo litakurudisha kwenye hali ya utulivu wa kuendelea kufanya mambo yako.

Kumbukumbu zako za nyuma ni moja ya vitu vikubwa kuliko wewe, ni kitu ambacho kinaweza kukurudisha kwenye utulivu pale mambo yanapokuwa yamekuyumbia.

Sheria ya leo; Pitia kumbukumbu zote za maisha yako na chagua zile ambazo ni nzuri, kipindi ambacho mambo yako yote yalikuwa sawa. Kila unapopitia magumu na changamoto, jikumbushe kumbukumbu hizo nzuri, hilo litakurudisha kwenye utulivu mkubwa.

#NidhamuUandilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji