2964; Onyesha kazi yako.
Rafiki yangu mpendwa,
Wakati upo shuleni, ulifundishwa namna sahihi ya kufanya hisabati.
Kila swali la hisabati lilikuwa na sehemu tatu.
Sehemu hizo ni swali, kazi, jibu.
Katika kujibu maswali hayo ya hisabati hukutakiwa tu kutoa jibu sahihi, bali ulitakiwa kuonyesha njia uliyotumia kupata jibu hilo.
Mara nyingi, hata kama ulikosa jibu, bado ulipata sehemu ya alama kwa kazi uliyoonyesha.
Hivyo pia ndivyo ilivyo kwenye maisha yetu ya kila siku.
Kuna changamoto ambayo ndiyo swali, kuna kuchukua hatua ambako ndiyo kazi ya kufanya kwenye changamoto hiyo na kuna matokeo ambayo ndiyo jibu.
Kama ilivyo kwenye hisabati, hata kwenye maisha, unaweza kupata sehemu ya alama kwa kuonyesha kazi, hata kama jibu siyo sahihi.
Kuonyesha kazi ndiyo kitu tunachoita kukaa kwenye mchakato.
Watu wengi wamekuwa wanahangaika na njia za mkato ili kupata haraka matokeo wanayotaka.
Lakini ushuhuda upo wazi, mwisho wao umekuwa siyo mzuri.
Hata pale walipoanza kwa kupata matokeo mazuri, waliishia kwenye anguko baya sana.
Lakini wale wanaokaa kwenye mchakato sahihi, hata kama matokeo wanayoanza nayo siyo sahihi, kitendo tu cha kukaa kwenye mchakato kinawapa manufaa makubwa sana.
Twende kwa mfano ili tuelewane vizuri.
Kuna watu huwa wanaanzisha biashara, wanatumia njia zisizo halali na kupata matokeo makubwa mwanzoni.
Wanaweza kusifiwa kwa matokeo hayo, lakini huwa haichukui muda wanapata anguko kubwa na kuharibu sifa yao yote.
Lakini kuna ambao wanaanzisha biashara, wanafuata mchakato sahihi lakini kutokana na mambo yaliyo nje ya uwezo wao, biashara zinashindwa.
Kupitia kuonyesha kwao kazi, kwa kukaa kwenye mchakato sahihi, watu hao huendelea kuaminika na kuungwa mkono, kitu kinachokuja kuwapa matokeo makubwa na mazuri sana mbeleni.
Hivyo basi rafiki yangu, wajibu wako mkubwa ni kuonyesha kazi yako, kwa kukaa kwenye mchakato sahihi mara zote.
Haijalishi sana ni matokeo gani unayopata sasa, kukaa kwenye mchakato sahihi ni ushindi wa kwanza na muhimu.
Kwa kuendelea na hilo, unakuwa na uhakika wa ushindi mkubwa sana kwenye matokeo baadaye.
Kukaa kwako kwenye mchakato sahihi ni kinga nzuri kwako pale mambo yanapokwenda tofauti na matarajio yako, kitu ambacho huwa kinatokea mara nyingi sana.
Watu watakuja kwako na njia za mkato, wakikuonyesha majibu ili uyanakili tu.
Lakini kama hutaweza kuonyesha kazi iliyokufikisha kwenye majibu hayo, umejenga nyumba juu ya mchanga bila ya msingi imara.
Kuanguka ni swala la muda tu.
Kukaa kwenye mchakato kamili na sahihi muda wote ni hitaji muhimu sana kwenye safari yako ya mafanikio.
Epuka sana njia za mkato, zitaishia kukuacha na mikato mingi.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#BilioneaMafunzoni
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Mchakato kamili na sahihi ndio suluhisho la muda wote
LikeLike
Tukae kwenye mchakato.
LikeLike
Swali,kazi,jawabu… Kweli Kila kitu kina kanuni zake tokea kale. Asante sana. Hakuna mbadala wa kukuaa kwenye mchakato.
LikeLike
Tunajifanyaga wajanja kuziacha kanuni ambazo zimefanya kazi miaka na miaka.
Hakuna ukweli mpya, kanuni ni zile zile.
LikeLike
Asante kocha,nitakaa kwenye mchakato ili nijenge msingi imara zaidi kuliko kutafuta urahisi zaidi.
LikeLike
Kutafuta urahisi ni kujipeleka kwenye magumu.
LikeLike
Kinachoturudisha wengi wetu nyuma ni Ile hali ya kujiuliza haya yanawezekana Vipi. Mtu anataka kuiona safari yote ya kuanzia dar Hadi Dodoma Kwa pale alipo.
Hilo halitawezekana. Kinachowezekana ni kukaa kwenye basi la kwenda Dodoma na majibu yote ya safari utayapata ukiwa kwenye safari.
Ni kweli gari inaweza kuharibika njia, lakini hilo hutaweza kuliona kabla ya kuanza safari. Tukubali kukaa kwenye basi na matokeo yake tutayaona Kwa kufika kituo b salama . Lakini pamoja na kufika hatukuweza kutabiri Kila kitu kitakachotokea kwenye safari hiyo. Ndivyo ilivyo kwenye kazi au biashara zetu. Tuendelee kukaa kwenye mchakato.
LikeLike
Hakika,
Na utamu wa safari ni kutokujua nini kitatokea safarini.
Ungekuwa unaiona njia nzima mpaka mwisho wa safari, usingepata hata msukumo wa kusafiri.
Tukae kwenye mchakato.
LikeLike
Mchakato kamili na sahihi ni hitaji muhimu na la lazima kwenye safari ya mafanikio.
LikeLike
Tusihangaike na mengine yasiyo na tija.
LikeLike
Kukaa kwenye mchakato,kukaa kwenye mchakato, kukaa kwenye mchakato,hilo ndiyo hitaji kubwa sasa kwangu.
LikeLike
TUKAE KWENYE MCHAKATO.
LikeLike
Hakika.
LikeLike
Asante sana Kocha kukaa kwenye mchakato ndio njia sahihi inayotufikisha mahali tunapopataka. Kufuata njia ya mkato ni sawa na kujenga nyumba juu ya mchanga
LikeLike
Upepo ukija hamna nyumba.
Tujenge msingi sahihi unaoweza kuhimili kila dhoruba.
LikeLike
Kukaa kwako kwenye mchakato sahihi ni kinga nzuri kwako pale mambo yanapokwenda tofauti na matarajio yako, kitu ambacho huwa kinatokea mara nyingi sana.
LikeLike
Hata mambo yaendeje, jibu ni moja, kukaa kwenye mchakato.
LikeLike
Kukaa kwenye mchakato ni sawa na kuonyesha kazi katika kufanya swali la hisabati.
Nitakaa kwenye mchakato daima.
LikeLike
Acha tukae kwenye mchakato kwa kweli, hili la wale waliopata mafanikio kwa ujanja ujanja ninaushahidi kabisa jinsi walivyoangukia puwa. Maisha yanatutaka tukue taratibu.
LikeLike
Wasio na misingi hawajui hili.
Wanaingia kwa papara na kuruka kwa njia zisizo sahihi.
Mwishowe wanaishia kuungua jua.
LikeLike
Kabisa, bila njia sahihi, majibu yanakuwa ya kubahatisha.
LikeLike
Acha tukae kwenye mchakato kwa kweli, hili la wale waliopata mafanikio kwa ujanja ujanja ninaushahidi kabisa jinsi walivyoangukia puwa. Maisha yanatutaka tukue taratibu.
LikeLike
Tujifunze na kutorudia makosa ya wengine.
LikeLike
Ni kweli kocha hilo ndilo lililomtokea Andani aliekuwa tajiri zaidi wa bara La Asia,,Baada ya kuripotiwa kama anatumia njia za panya kujitajirisha utajiri wake umepungua kwa zaidi ya bilioni 100 ndani ya mwezi mmoja.
LikeLike
Tukae kwenye mchakato.
Unaweza kuwadanganya watu kwa muda mfupi.
Lakini muda ni hakimu mzuri,
Kila kitu huwa hadharani.
LikeLike
Njia ya mkato itakuacha kwenye mkato.Kazi kuu ni kukaa kwenye mchakato hata kama mamtokeo siyo sahihi,muhimu njia iwe sahihi
LikeLike
Tukae kwenye mchakato.
LikeLike
Lengo kuu ni kuonesha kazi yako na kazi yenyewe ni kukaa kwenye mchakato.
Asante sana
LikeLike
Hakika.
LikeLike
Kukaa kwenye ndio Siri kuu ya mafanikio yoyote kwenye maisha
Asante
LikeLike
Kweli.
LikeLike
Hii ni sahihi sana sana kwa kweli na mchakato ndio jambo kubwa sana..
LikeLike
Tukae kwenye mchakato.
LikeLike
Daima nitakaa kwenye mchakato
LikeLike
Safi sana.
LikeLike
Hakika kocha kukaa kwenye mchakato ndio kila kitu kwetu.
LikeLike
TUKAE KWENYE MCHAKATO.
LikeLike
Kwa kuonyesha kazi tunapunguza baadhi ya maswali katika mafanikio tutakayoyapata. Asante kocha
LikeLike
Kweli.
LikeLike
Kweli kabisa .i.i ni mwalimu wa hisabati, bila kuonyesha njia hupati chochote. Maisha pia na by asa biashara tunaihitaji zaidi kukaa kwenye mchakato.
LikeLike
Tukae kwenye mchakato, hiyo ndiyo njia kuu.
LikeLike
Mchakato ndiyo mpango mzima, njia ya mkato kutafuta matokeo haitakuwa ya kudumu Bali ni furaha ya muda mfupi. Weka kazi na andaa mchakato imara.
LikeLike
Tukae kwenye mchakato.
LikeLike
Mara zote nakaa kwenye mchakato ili kupata matokeo yaliyosahihi hata kama itanichukua mida mrefu nitavumilia kuliko kupita njia za mkato.
Asante kocha
LikeLike
Tukae kwenye mchakato, nje ya hapo ni kujipoteza.
LikeLike
Onyesha kuwa unaijali kazi yako kwa kushirikiana na vijana waonyeshe njia onyesha kazi yako achana na njia za mkato
LikeLike
Hakika
LikeLike