2969; Tegemeo lako.
Rafiki yangu mpendwa,
Hakuna kipindi kizuri kwenye kujenga biashara kama kipindi ambacho biashara ina wateja wachache.
Wengi hukihofia kipindi hiki na kukimbilia kufafuta wateja wengi zaidi kabla hawajawajua vizuri wateja wachache walionao.
Hakuna tatizo lolote kwenye kutaka kufikia wateja wengi zaidi. Lakini itapendeza sana kama utawatumia vizuri wateja wachache wa awali unaokuwa nao.
Wakati biashara yako inakuwa na wateja wachache ndiyo kipindi kizuri kwako kuwajua kwa kina.
Ndiyo kipindi cha kujifunza mengi sana kutoka kwao kwa namna ya kuwahudumia vizuri.
Ndiyo kipindi cha kuwahudumia vizuri sana na kuwapa thamani kubwa ili kuwajengea imani kwako.
Na pia ndiyo kipindi cha kupata wateja wengine bora zaidi kutoka kwa wateja ulionao.
Kwa umuhimu huo wa wateja wa awali, wanakuwa ndiyo tegemeo la biashara yako.
Washike mikono yao, wajue kwa kina na wape mapenzi ya kweli.
Wajibu wako mkubwa ni kuhakikisha wateja hao wa mwanzo wanafanikiwa kwenye eneo unalowahudumia, ili wasiwe na sababu ya kwenda kwa washindani wako.
Na hilo halina muujiza wowote kwenye kulifanya. Unapaswa kuwapigia simu, kuwatembelea na kuongea nao kwa kina.
Unapaswa kuwauliza nini hasa wanachotaka, nini cha kuboresha na mawazo mengine yoyote waliyonayo.
Waombe ushauri na maoni yao kisha fanyia kazi mapendekezo wanayotoa.
Wafanyabiashara wengi wamekuwa wanapuuza hili na baadaye kujikuta kwenye changamoto kubwa.
Kila wanapokazana kufikia wateja wengi wapya, wanajikuta wakipoteza wa zamani waliokuwa nao.
Biashara yako inapokuwa na wateja chini ya 100, ni kipindi cha kuwajua wateja hao wote kwa undani na kuwapa thamani kubwa sana.
Na hata kama biashara yako ina wateja zaidi ya 100, chagua 100 ambao hutaki uwapoteze kwa namna yoyote ile. Kisha wajue kwa kina na uwape thamani kubwa mno kiasi cha wao kukosa sababu ya kwenda kununua pengine.
Ni jambo la kuumiza sana pale unapotumia nguvu kubwa kufikia wateja wapya na kuwashawishi kununua, wakati wale ambao tayari walishanunua hawarudi tena, badala yake wanaenda kununua kwa wengine.
Ni uzembe wa hali ya juu sana pale mfanyabiashara anapokuwa hana taarifa za wateja ambao wameshanunua kwenye biashara yake na mwenendo wao kwenye matumizi.
Na uzembe wa aina hii ndiyo umekuwa chanzo cha biashara nyingi kufa.
Iko hivi rafiki, ni rahisi sana kumuuzia mteja ambaye ameshanunua kuliko ambaye ni mpya kabisa.
Na kama mteja ameshanunua kwako mara moja, anapaswa anunue kipindi chote cha maisha yako.
Kama wateja wananunua mara moja na hawarudi, kuna uzembe mkubwa sana unaofanyika na hata uhangaike na kufikia wateja wapya wengi kiasi gani, bado biashara itashindwa kukua.
Biashara yako inahitaji wateja wasiopungua elfu 1 ili iweze kujiendesha kwa faida na kupata ukuaji.
Lakini wewe binafsi kama mfanyabiashara, unahitaji wateja wasiopungua 100 ambao unawajua hao ni mashabiki wa kweli, wasioweza kwenda kununua pengine ila kwako, na hao ndiyo watakuwezesha kukaa kwenye mapambano ya kujenga biashara yako.
Unawajengaje wateja hao 100 ambao ndiyo tegemeo lako?
Ni kwa kuwajali kwa kupitiliza.
Kuwajua kwa undani, kuwapa thamani kubwa sana na kuwa nao karibu mno.
Kuwa tayari kuacha mengine yote na kuwahudumia vizuri wateja 100 ambao ndiyo tegemeo lako.
Kuna mengi utakayojifunza kwa wateja hao 100 ambayo yatakuwezesha kuikuza sana biashara yako.
Hivyo pia ndivyo ilivyo kwa wafanyakazi wa biashara yako.
Wakati unapokuwa nao wachache, chini ya 30, wajue kila mmoja kwa undani na kuwajali sana.
30 ni idadi ambayo mnaweza kuenea kwenye chumba kimoja cha kufanya mkutano. Ni rahisi kumjua kila mtu kwenye wafanyakazi 30.
Lakini wanapokuwa wengi zaidi, wanakuwa chini ya viongozi wengine, hivyo wewe unaweza usiwajue moja kwa moja na kwa undani.
Tumia sana fursa za awali wakati wafanyakazi ni wachache kujenga utamaduni bora kabisa wa eneo lako la biashara.
Tumia yale unayojifunza kwa wafanyakazi wachache unaokuwa nao kuweza kujenga timu kubwa zaidi ya wafanyakazi sahihi kwenye biashara yako.
Kwa sababu tunataka sana kukua, huwa hatupapendi chini, lakini ndivyo asili inavyofanya kazi.
Mbegu hukaa chini kwa muda na kushika mizizi kabla haijakua.
Nyumba hujengewa msingi imara sana chini ya ardhi kabla haijapandishwa na kuwa nyumba.
Zingatia sana hatua za awali, hapo ndipo penye nguvu kubwa ya kujenga biashara kubwa na itakayokufikisha kwenye malengo makubwa uliyonayo.
Usitake tu kukimbia, jua unakimbia kuelekea wapi.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#BilioneaMafunzoni
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Hiyo ni nafasi nzuri sana pia kukua kama utatoa huduma nzuri
LikeLike
Hakika, ukiwahudumia vizuri wachache, watakuletea wengi zaidi.
LikeLike
Leo naacha mengine yote ili KUWAHUDUMIA wateja wangu 100
LikeLike
Washike mkono, wapende, wahudumie vizuri na jipe jukumu la mafanikio hao.
Hapo ndipo pa kutokea kwa uhakika.
LikeLike
Asante sana kocha nimejifunza jambo kubwa sana leo ,kipindi cha kuwa karibu sana na wateja na kuwahudumia kwa thamani kubwa ni kipindi ambacho wateja wa biashara ni wachache,wengi tunakimbilia kutafuta wateja wapya wakati hawa wachache tulio nao hawarudi kununua tena kwasababu tumewasahau,napambana kuwahudumia wateja wangu wachache nilionao kwa kuwajali na kuwapa huduma bora na bidhaa bora ili kujenga wateja 100 bora ambao watakua mashabiki wa biashara yangu.
LikeLike
Hakika, pamoja na kuendelea kutafuta wateja wapya, tusiwasahau wale tulio nao. Maana hao ndiyo wenye nguvu kubwa ya kutuwezesha kukua sana.
LikeLike
Asante Kocha,
Nisitake tu kukimbia, nijue ninaelekea wapi.
LikeLike
Uelekeo ni muhimu kama zilivyo mbio zenyewe.
LikeLike
Kipindi ambacho biashara bado ni changa na ina wateja wachache, ndiyo muda wa kujijenga biashara yako kwenye misingi mizuri; wafanyakazi na wateja
LikeLike
Kabisa, ukiweka msingi mzuri hapo, biashara itaweza kukua vizuri.
Ukikosea hapo, ukuaji utakuja na changamoto kubwa.
LikeLike
Kuwafahamu wateja kiundani ni msingi muhimu wa kuwatunza na kuwafanya wawe wazalendo na washabiki kwa biashara
LikeLike
Na wateja wenye uzalendo ndiyo wenye nguvu ya kutuletea wateja wengine wengi zaidi.
Tuweke nguvu za kutosha hapo.
LikeLike
Asante sana Kocha,nimejifunza kutumia fursa za awali kujenga utamaduni bora kwenye biashara yangu.
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Asante sana Kocha Dr Makirita Amani, ni kweli tunapaswa kuweka nguvu kwanza kwa wale ambao tayari wamenunua na kuwapa thamani kubwa wateja 100 kwanza wa awali kabla ya kukimbilia wapya.
LikeLike
Hapo ndipo pa kujenga msingi imara wa biashara zetu, ambao utaziwezesha kukua kwa ukubwa sana.
LikeLike
Wajibu wako mkubwa ni kuhakikisha wateja hao wa mwanzo wanafanikiwa kwenye eneo unalowahudumia, ili wasiwe na sababu ya kwenda kwa washindani wako.
LikeLike
Watu wanapenda mafanikio,
Wasaidie kufanikiwa na watakuwa waaminifu kwako.
LikeLike
Asante kocha,nitajitahidi kuweka nguvu kubwa kwa kuwajali wateja wangu wachache kuliko kuwa na wateja wengi na kusahau wa mwanzoni.
LikeLike
Vizuri,
Haimaanishi tusikue kwa wateja, ila ukuaji usisababishe tuwasahau wateja ambao tayari tunao.
LikeLike
Nitajenga msingi imara wa biashara yangu ingali bado changa.
LikeLike
Vizuri.
Huo ndiyo wakati sahihi wa kuweka msingi imara.
LikeLike
Kipindi ambacho biashara ina wateja wachache ndio kipindi kizuri cha kujenga biashara.
1. Wajali sana wateja wako na wape thamani kubwa
2. jenga nao urafiki kwa kuwapigia simu, kuwatumia jumbe mbali mbali na kuwatembelea.
3. Watumie kupata wateja wa rufaa.
4. Weka mkakati wa kuwa nao 100 kamawa kudumu ila watengeneze wengine mpaka wafikie 1,ooo
LikeLike
Kanuni ya uhakika ambayo haiwezi kushindwa.
Itakayokusaidia kujenga msingi imara wa biashara.
Tukae humo.
LikeLike
Ni jambo la kuumiza sana pale unapotumia nguvu kubwa kufikia wateja wapya na kuwashawishi kununua, wakati wale ambao tayari walishanunua hawarudi tena, badala yake wanaenda kununua kwa wengine.
Huu uzembe unaua sana biashara, ni kuwa mtu makini tu sasa ili kuwahudumia wateja vizuri.
Ahsante sana Kocha.
LikeLike
Tuhakikishe wakishanunua kwetu hawana tena sababu ya kwenda kununua kwa washindani wetu.
LikeLike
Kujenga biashara kubwa unaanza na biashara ndogo Kwa kuwahumia wateja wachache Kwa kutoa thamani kubwa sana
Asante
LikeLike
Kanuni ya uhakika hiyo.
Tukae humo.
LikeLike
Asante sana Kocha napambana kuhakikisha nakuwa na wateja wa uhakika 1,000 ambao watakuwa ni wateja wazalendo
LikeLike
Vizuri sana,
Hilo linawezekana kabisa.
Na linahitaji kazi,
Ambayo tupo tayari kuiweka.
LikeLike
usitake tu kukimbia,jua unakimbilia wapi
LikeLike
Kabisa,
Unaweza kupoteza nguvu nyingi bure, wakati ungezipeleka eneo sahihi zingekuwa na tija zaidi.
LikeLike
Nitaendelea kuweka juhudi kubwa kuhakikisha natumia kipindi cha wateja wachache kuwapa huduma bora
LikeLike
Vizuri, usidharau uchache, badala yake utumie kwa manufaa.
LikeLike
asante kocha ,kipindi ambacho nina wateja wachache natoa huduma kabisa ili wateja wenyewe waambiane wao na bishara ikue. pia mm ndo napata kujifunza mengi.
LikeLike
Wahudumie vizuri sana wateja wachache wa mwanzo na wao watakuwa mabalozi wazuri kwako kwa wateja wengi wa baadaye.
LikeLike
Nachagua wateja 100, nitakaowajua vizuri Kwa undani.
Sikimbii tuu, ila Natafuta kujua nakimbia kuelekea wapi.
Najali sana na kuwa karibu na wafanyakazi wangu.
Nawathamini sana wateja na wafanyakazi wangu.
LikeLike
Vizuri,
Weka juhudi sahihi kwenye eneo sahihi na zitazaa matunda makubwa.
LikeLike
Najenga misingi na mifumo imara kwa biashara yangu ikiwa bado ndogo ili itakapofikia kukua nisipate tangamoto kunwa kwani mambo mengi nitakua nimeshayajengea misingi imara huko mwanzo.
Asante sana kocha
LikeLike
Vizuri, fanya hivyo.
LikeLike
Ni kweli wateja 100 ukiwapa huduma nzuri wakawa mashabiki Wako na wewe ukanenga urafiki nao utafika mbali sana naanza na kutengeneza hiyo cream yangu ya wateja hao nikiwamudu 100 ntaenda zaidi ya hapo hadi wanifikishe kule tunapoenda
LikeLike
Mpango bora kabisa huu.
Utekeleze.
LikeLike