2972; Hatari umeibeba wewe.
Rafiki yangu mpendwa,
Kuendesha biashara kuna changamoto nyingi sana.
Kila wakati kuna kitu unakuwa unapambana nacho.
Kama hiyo haitoshi, kuna hatari kubwa unayokuwa umeibeba kila siku kibiashara.
Changamoto unazokabiliana nazo kibiashara zinakuwa na hatari ya kuweza kupelekea biashara kufa.
Tatizo zaidi ni kwamba hatari yote ya biashara yako umeibeba wewe.
Chochote kinachotokea kwenye biashara, wewe ndiye utakayeumia kuliko wengine wote.
Cha kushangaza, kuna watu ambao wanataka wakupangie uendesheje biashara yako, wakati wao hawabebi hatari yoyote uliyonayo.
Watu hao watakuwa na uthubutu wa kukupinga kwenye baadhi ya hatua muhimu unazochukua kwa ukuaji wa biashara yako.
Pale unapojisukuma kwa kuweka juhudi zaidi ili kutatua changamoto za biashara watakuona kama unajitesa na kukutaka uende kawaida.
Watu hao hujiona kama wana wajibu wa kukueleza nini unapaswa kufanya na nini hupaswi.
Lakini inapokuja kwenye hatari, hawataki kabisa kuhusika nayo.
Tatizo kubwa ni kwamba kwenye jamii zetu, kila mtu ana maoni kwenye kila kitu.
Hata kama mtu haelewi kitu kwa undani, bado anakuwa na maoni yake.
Na zaidi, watu huwa wapo tayari kutoa ushauri hata kama hawajaombwa.
Wanaona tu kitu kwa nje na kukimbilia kutoa ushauri wao.
Wewe unapaswa kuwa makini sana na watu gani unaowasikiliza na kuchukua ushauri wao.
Kwanza jua kuna kitu unakiona wewe kwenye fikra zako ambacho wengine hawaoni.
Watu kukimbilia kukupa maoni na kukushauri kwa mambo waliyoona kwa nje na hawajajua kwa ndani, ni jambo unalopaswa kulipuuza kabisa.
Unapuuza kwa sababu unajua maoni na ushauri ambao mtu anatoa haujakamilika.
Lakini pia hakuna hatari yoyote watoa maoni na ushauri wanakuwa wanaingia.
Kuongea ni rahisi sana, kila mtu anapenda kufanya hivyo.
Hatari ipo kwenye kuchukua hatua, ambapo ni wachache sana wanaofanya hivyo.
Jikumbushe hulazimiki kuchukua maoni na ushauri wa kila anayejitolea kukupa.
Hatari yote umeibeba wewe, picha ya wapi unaenda unayo wewe.
Jiamini na fanya maamuzi sahihi ambayo yanapunguza hatari na kukupeleka kule unakoelekea.
Watu wengi huziona biashara ni nzuri na rahisi kwa kuangalia kwa nje.
Wanakuwa hawajui moto unaokuwa unaendelea ndani, ambapo kila wakati kazi kubwa ni ya kuzima moto.
Usisahau hili kwenye kila maamuzi unayofanya ya kibiashara.
Unaweza kusikiliza maoni na ushauri kadiri unavyotaka.
Lakini inapokuja kwenye kutekeleza, jikumbushe hatari umeibeba wewe peke yako.
Hivyo fanya maamuzi yenye tija, hata kama kwa wengine yanaweza kuonekana ni ya kipuuzi.
Usibabaishwe na wale wanaokulazimisha ufanye vitu vya aina fulani kwa sababu ndivyo wanavyoona wao.
Jua hatari ilipo na fanya maamuzi sahihi kulingana na hatari hiyo.
Watu wengi wanapenda sana kuongea, lakini hakuna anayependa kuwajibishwa kwa yale aliyoongea.
Hilo tu likupe funzo kubwa kuhusu uzito unaopaswa kuweka kwenye yale wengine wanakuambia.
Kama mtu hayupo tayari kugharamia kile anachoongea, inakudhihirishia wazi uzito wa hicho anachokuambia.
Kama kingekuwa muhimu na cha uhakika, angekuwa tayari kubeba hatari yake.
Tusidanganyike, mambo siyo rahisi na wala hayatakuja kuwa rahisi.
Kama maoni na ushauri unaotolewa na kila mtu ungekuwa unafanya kazi, changamoto nyingi za kibiashara zisingekuwepo.
Lakini kuendelea kuwepo kwa changamoto hizo na hatari za biashara kufa, ni kiashiria jinsi maoni na ushauri mwingi unaotolewa bure na kirahisi kabisa havina thamani yoyote.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#BilioneaMafunzoni
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Kama mtu hatawajibika Kwa aina ya ushauri anaokupa basi uchaguzi sahihi unabakia kwako.
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Napaswa kukigaramia kile Ninachokiongea vingnevyo nitaadhiirisha kuwa cjaweka uzito wowote
LikeLike
Hakika
LikeLike
Hatari nimeibeba mimi peke yangu ,inapokuja kwenye ushauri na maoni nasikiliza lakini uamuzi ni juu yangu.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Ni kweli kabisa.
Juzi nilipoajiri mfanyakazi wa kike. Kuna mtu aliniambia kwa Nini ninaajiri mfanyakazi wa kike badala ya mwanaume. Nilipaswa kuajiri mwanaume.
Sasa hivi nimeongeza wafanyakazi wawili, ananiambia nilipaswa kuajiri mwingine mmoja kwanza.
Lakini yeye hajui Moto unapendelea ndani na kila tunavyopaswa kufanya.
#Hauna kurudi nyuma
#Najenga biashara
#Hakuna kuremba mwandiko
LikeLike
😂😂
Watu wanakosaga kazi za kufanya na kuzurura sana.
Mtu anajitolea kukushauri kwenye jambo ambalo hujamwomba.
Ni jambo la kushangaza.
Tuwashe moto, waone majivu tu.
LikeLike
Maoni na ushauri wa bure kutoa ni rahisi sana kutoa kwa wengine.Lakini kwako ina gharama sana maana hakuna anaeingia kwa fikra zako kujua kwa undani na kuwa tayari kubeba athari zitakazotokea baadae.
LikeLike
Ushauri wa bure unaanza kuulipia pale unapoutumia, maana unakugharimu sana.
LikeLike
Hatari ya biashara na maisha yangu nimeibeba mwenyewe, nahitaji kuwa makini sana ushauri na maoni ninayopewa, maana mwisho wa yote mimi mwenyewe ndiyo wakuharibikiwa na kuumia.
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Tusidanganyike, mambo siyo rahisi na wala hayatakuja kuwa rahisi.
LikeLike
Tuanzie hapo kwa usahihi, ili tujiandae kwa mapambano makubwa yaliyo mbele yetu.
LikeLike
Tatizo zaidi ni kwamba hatari yote ya biashara yako umeibeba wewe. Hivyo basi Jiamini na fanya maamuzi sahihi ambayo yanapunguza hatari na kukupeleka kule unakoelekea.
Usisikilize na kufuata saaana ushauri wa wengine maana wanaiona biashara yako kwa nje tu.
LikeLike
Tunahitaji sana huo ujasiri, maana umekosekana kwa wengi na kuwa madhara makubwa.
LikeLike
Si kila ushauri naopewa juu ya namna ya kuendesha biashara yangu napaswa kuufanyia kazi kwani hatari kunwa ya biashara nimeibeba mimi,na kila mtu ni mshauri kwenye kila jambo lakin napaswa kujiuliz je anaenipa ushauri wa hii bishara yangu alishawahi kufanya biashara?na ni kweli anaipenda na kuijali biashara yangu kuliko mimi?akili kichwani mwangu.
Asante kocha
LikeLike
Hakika.
LikeLike
Ni kweli kabisa kwenye biashara hatari yoyote unaibeba wewe sikiliza ushauri lakini fanya unachojua wewe
Asante sana
LikeLike
Kweli kabisa.
LikeLike
Mtaani mabingwa wa ushauri ni wengi ila watendaji ni wachache.
LikeLike
Ukiwasikiliza unaishia kuwa kama wao.
LikeLike
Napaswa kuwa makini na washauli. Wanashauli Jambo kwa kuliona kwa nje, Mimi ndie ninaeiona bicha ya matokeo nitakayopata wao hawaioni , lakini pia Kama hatari itatokea wao hawatawajibika.
Asante Sana kocha ni Somo Bora kabisa.
LikeLike
Vizuri kabisa.
LikeLike
Napaswa kuwa makini na washauli. Wanashauli Jambo kwa kuliona kwa nje, Mimi ndie ninaeiona picha matokeo nitakayopata wao hawaioni , lakini pia Kama hatari itatokea wao hawatawajibika.
Asante Sana kocha ni Somo Bora kabisa.
LikeLike
Tatizo kubwa ni kwamba kwenye jamii zetu, kila mtu ana maoni kwenye kila kitu.
Hata kama mtu haelewi kitu kwa undani, bado anakuwa na maoni yake.
Na zaidi, watu huwa wapo tayari kutoa ushauri hata kama hawajaombwa.
Wanaona tu kitu kwa nje na kukimbilia kutoa ushauri wao.
Asante sana Kocha Dr Makirita Amani.
LikeLike
Lazima tuwe makini sana na hawa watoaji wa ushauri wa bure, la sivyo tutaishia kuwa kama wao.
Maana aliye tayari kutoa ushauri wa bure kwenye mambo ambayo hajaombwa, hawezi kuwa amepiga hatua kubwa kwenye jambo lolote lile.
LikeLike
Asante Sana kwa SoMo la Leo.
Mie nimekuwa mhanga wa kupata ushauri wa watu ambao hata hujauomba. Na anachukia Sana usipofata mawazo yake. Kibaya zaidi la.a kakupa ushauri ukaupuuza halafu itokee umeshindwa kutokana na changamoto zingine anafurahi anasema SI NILIKWAMBIA UKAPUUZA. Atakutangaza na kukuona hufai. Ila unakuwa na bahati ukisimamia Misingi yako na ikafanikiwa.
LikeLike
Dawa ni kuwa bize sana kiasi kwamba hapati hata hiyo nafasi ya kukupa ushauri ambao hujamwomba.
LikeLike
Mtu asiyejua undani wa kitu hawezi kutoa ushauri sahihi, hususan kama hajawahi kufanya kitu hicho yeye mwenyewe binafsi.
LikeLike
Kwa nje mambo ni rahisi,
Kwa ndani, siyo rahisi kihivyo.
Tuwe makini na ushauri tunaopata kwa wanaoona kwa nje.
LikeLike
Ni ukweli kabisa
LikeLike
Karibu.
LikeLike
ushauri wowote ambao mtu hawezi kulipa gharama ili umpe yeye kwanza faida,
nitaupuuza maana unamfaa yeye sio mimi.
asante kocha.
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Kwenye ushauri ni vyema kuzingatia na mtu ambae anakupa ushauri kwenye kile unachokifanya..
LikeLike
Hakika, maana ushauri ni rahisi kutoa, ila mgumu kutekeleza.
LikeLike
Hatari yote nimeibeba mimi, picha ya wapi naenda ninayo mimi.
Natakiwa kujiamini na kufanya maamuzi sahihi ambayo yanapunguza hatari na kunipeleka kule ninakoelekea.
Ahsante sana Kocha Dr. Makirita Amani.
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Angalia kama anayekupa ushauri yeye anaishi hivyo.
LikeLike
Skin in the game.
LikeLike