2994; Tatu bila.
Rafiki yangu mpendwa,
Haya maisha ni sawa na mchezo wa mpira wa miguu.
Urahisi au ugumu wa sisi kupata ushindi unategemea sana uelewa wetu wa pale tunapoanzia na juhudi tunazoweka.
Kwenye mpira wa miguu, timu inayokuwa nyuma kwa magoli, yaani ambayo inakuwa imefungwa, inakuwa kwenye nafasi kubwa ya kushindwa.
Na kadiri muda unavyokwenda huku timu ikiwa nyuma, ndivyo kushindwa kunakuwa kwa uhakika.
Timu inayokuwa nyuma kwa magoli inapaswa kuweka juhudi za ziada ili iweze kupata
Kwenye mchezo wa maisha, watu wengi wanashindwa kwa sababu wanaanza wakiwa nyuma kwa magoli, lakini wanacheza kawaida badala ya kuweka juhudi za ziada.
Wanakuwa wanalinda goli kuliko kushambulia ili kupata ushindi.
Tunaanziaje nyuma kwenye huu mchezo wa maisha?
Kwa wengi, tunaanza huu mchezo tukiwa tayari tumefungwa magoli ya kutosha.
Hivyo ili tumalize kwa ushindi, tunalazimika kuweka juhudi kubwa mno.
Kuzaliwa kwenye nchi masikini unakuwa unaanza ukiwa umefungwa goli moja, yaani ni moja bila, unaingia kwenye mchezo ukiwa tayari umefungwa.
Hiyo ni kwa sababu kwenye nchi masikini mazingira na mifumo mingi inakuwa kikwazo kwa mtu kufanikiwa.
Kwa kuzaliwa kwenye nchi masikini, unapoteza muda mwingi kuhangaika na mambo yasiyokuwa na tija kabisa.
Kuna vikwazo vingi vinavyokuwa nje ya uwezo wako, ambavyo vitapoteza sana muda na fedha zako.
Kuzaliwa kwenye nchi masikini na familia masikini unakuwa umefungwa magoli mawili kwa bila kwenye kipindi cha kwanza cha mchezo.
Hiyo ni kwa sababu unapozaliwa kwenye familia masikini, unakuwa huna pa kuanzia, yaani unaanzia sifuri.
Lakini kama hiyo haitoshi, unakuwa na kundi kubwa la wanaokutegemea.
Hivyo hata ukipiga hatua kidogo, utavutwa nyuma na kundi hilo la wategemezi.
Kuzaliwa kwenye nchi masikini, familia masikini na ukawa na tabia za kimasikini ni tatu bila kwenye kipindi cha pili cha mchezo.
Yaani tayari umeshafungwa magoli matatu na mchezo upo kwenye kipindi cha pili.
Kupata ushindi katika hali kama hiyo ni lazima uweke juhudi kubwa mno, juhudi zisizo za kawaida kabisa.
Tabia za kimasikini zina nguvu kubwa ya kumkwamisha mtu asiweze kupiga hatua kwenye maisha.
Hata kama ataweka juhudi kiasi gani, bado tabia hizo zitakuwa kikwazo kwake.
Tabia za kimasikini zipo nyingi, lakini kubwa zinazowakwamisha wengi ni uvivu na uzembe. Uvivu ni kutokufanya kile ambacho mtu anapaswa kufanya. Na uzembe ni kukifanya kwa namna isiyo sahihi.
Uvivu na uzembe ni vikwazo vikubwa sana kwa mtu kuweza kupiga hatua kubwa kwenye maisha yake, hata kama amedhamiria kwa kiasi gani.
Kadiri mtu anavyochelewa kuachana na tabia hizo za kimasikini, ndivyo anavyojiweka kwenye nafasi kubwa ya kushindwa.
Unapogundua kwamba umezaliwa kwenye nchi masikini na familia masikini, halafu una tabia za kimasikini, unahitaji kupambana mno. Huhitaji kuangalia wengine wanafanya nini au wanafanyaje, wewe unapaswa kupambana kufa na kupona. Maana kadiri unavyochelewa ndivyo unavyozidi kuukosa ushindi unaoutaka.
Na hata kama umeshazivuka tabia za kimasikini, bado unahitaji kuendelea kujisukuma zaidi ili uweze kuvuka vikwazo vingine ambavyo tayari vinakuzuia usipate mafanikio makubwa.
Ndiyo, unaanza ukiwa nyuma, lakini hiyo haimaanishi kwamba huwezi kupata ushindi mkubwa unaoutaka.
Ushindi unaoutaka unawezekana, ila jitihada utakazopaswa kuweka siyo za kawaida ni za juu sana, ambazo kwa hali ya kawaida utaonekana kama unajitesa.
Siyo wajibu wako kuwafurahisha na kuwaridhisha wengine.
Wajibu wako ni kupata ushindi kwenye maisha.
Na kwa bahati mbaya sana unaanza ukiwa nyuma.
Hivyo huna budi kuweka juhudi za ziada.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#BilioneaMafunzoni
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Kwa kweli ni tatu bila. Na ukizaliwa kwenye jamii inayokujenga katika imani na itikadi za kuwa na matumaini hewa na hofu zisizo na mashiko inakuwa ni nne bila kipindi cha pili dakika ya 70′.
LikeLike
Hiyo siyo dakika za nyongeza kweli? 🤣🤣
Maana kwenye hali hiyo kutoboa itakuwa kudra tu.
LikeLike
Napambana kuzing’oa tabia za kimasikini ili niweze kupata ushindi hata wa dakika za majeruhi
LikeLike
Pambana hata mchezo uende kipindi cha ziada, ili tu kujenga nafasi ya kushinda.
LikeLike
Tatu bila, Kaz inahitajika nidham Kali mno ya kuweza kutembea hata juu ya Moto Ili kupata ushindi.
LikeLike
Hakuna chini ya hapo.
LikeLike
Ahsante sana kocha nitaweka juhudi zangu zote kuhakikisha kuwa napata ushindi
LikeLike
Tusikubali chochote ila ushindi.
LikeLike
Kweli hutakiwi kulala na kuruhusu uvivu wakati upo tatu bila
LikeLike
Ni kukubali kushindwa kizembe.
LikeLike
ni kupambana kufa na kupona
ahsante
LikeLike
Hakuna namna nyingine.
LikeLike
Kweli uvivu umekuwa changamoto kubwa kwenye maisha yetu ya kila siku na kufanya tushindwe kupiga hatua..
LikeLike
Hiyo ni dhambi kubwa mno.
LikeLike
Hii tatu bila ni balaa, maana huu ndiyo uhalisia wa maisha ya wengi wetu, muhimu ni kupambana tu hadi kieleweke.
LikeLike
Lazima tujue tunaanzia nyuma, ndiyo maana nasisitiza sana kasi.
LikeLike
Siyo wajibu wako kuwafurahisha na kuwaridhisha wengine.
Wajibu wako ni kupata ushindi kwenye maisha.
Na kwa bahati mbaya sana unaanza ukiwa nyuma.
Hivyo huna budi kuweka juhudi za ziada.
LikeLike
Na kasi inahitajika sana, maana unaanza ukiwa nyuma.
LikeLike
Kupambana kufa na kupona ili kuchomoa magoli ambayo tayari tumeshafungwa.
Asante sana
LikeLike
Hii game ushindi ni lazima, japo tunaanzia nyuma.
LikeLike
Kweli inahitajika kazi kubwa kupambania ushindi katika mazingira ambayo tumeyakuta
LikeLike
Naweka juhudi kubwa ili niweze kujikwamua kwenye umaskini na kufikia malengo na ndoto kubwa nilizo nazo kwenye maisha yangu
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Mazingira yapo kinyume na tunachotaka, lakini hatutakiwi kukubali.
LikeLike
Dah hizi makala zinatafakarisha sana haya magoli 2 ya nchi masikini na familia masikini hujapanga ila hili goli la 3 ni la kujifunga mwenyewe. Kwa kweli ninahitaji kubadilika sana tena sana.
LikeLike
Bill Gates aliwahi kusema wazi; kuzaliwa masikini siyo kosa lako, ila kufa masikini ni uzembe wako.
LikeLike
Kwa hakika kunahitajika jitihada kubwa ya kimapinduzi kutafuta ushindi. Kwano kabla mchezo haujaanza inaonekana timu zetu zimeelemewa
LikeLike
Kucheza kulinda ni kuhalalisha kushindwa, maana tunaanzia nyuma.
LikeLike
Uvivu na uzembe ni kikwazo kikubwa kwa walio wengi kushindwa kufanikiwa.
LikeLike
Hizo ni dhambi mbili kubwa sana.
LikeLike
Wajibu wangu ni kuwa na maisha bora; siyo kuwafurahisha na kuwaridhisha wengine.
LikeLike
Kila mtu awajibike na furaha ya maisha yake.
LikeLike
Kweli, lazima kufanya maandalizi mpaka ushindi upatikane.
Ahsante sana kocha
LikeLike
Ushindi ni lazima.
LikeLike
Asante Kocha, kwa makala hii ya tatu bila; ni lazima niweke nguvu kubwa mno, juhudi zisizo za kawaida kabisa ili kupata ushindi. Hasa kwa kuachana na tabia za kimasikini zikiwemo uvivu na uzembe ambazo ni bao la tatu na la kujifunga mwenyewe.
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Kwa hakika natakiwa kupambana sana kuvuka Vikwazo, vya umasikini na masikini wanaonizungukaa
LikeLike
Kuna umasikini wa kimkakati uliopo kwa ajili ya kuzuia wengi wasifanikiwe, tuwe makini nao.
LikeLike
Ninaenda kuweka juhudi kubwa zaidi kuhakikisha nakuwa bora zaidi lazima nipate matokeo bila kujari nimetanguliwa kufungwa ngap
LikeLike
Safi sana.
LikeLike
Tukatae kufungwa tatu bila.
LikeLike
Muhimu ni kurudisha yote tuliyofungwa na kuongeza ya ziada ili kupata ushindi mkubwa.
LikeLike
Napaswa kuweka juhudi sana Ili kutoka kwenye tatu bila,maana bila juhudi sitatoboa. Asante sana Kocha.
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Napaswa kuweka juhudi sana Ili kutoka kwenye tatu bila,maana bila juhudi sitatoboa. Nashukuru Kocha.
LikeLike
Kuzaliwa kwenye nchi maskini familia maskini na kuwa fikra za kimasikini ngumu sana kutoboa,hapo inahitajika juhudi kubwa sana.
Lazima ujitoe kafara
Asante
LikeLike
Hakuna namna nyingine.
LikeLike
Asante Kocha
LikeLike
Karibu.
LikeLike
Kweli tunatakiwa kuweka juhudi zaidi kwani Ni kipindi cha pili tu Ni tatu bila.
LikeLike
Na hapo panakuwa pabaya zaidi.
LikeLike
Asante Sana kocha , Somo limedhihilisha Hali HALISI.
Nimeweza kutambua hatua sahihi za kuchukua . Mimi BINAFSI wakati namaliza shule tayari nilishakuwa nimetandikwa magoli mawili bila. Makala HIZI kocha ni msaada mkubwa kwetu kwani inakuwa Kama vile mtu kakufunua shuka lililokuwa limefunika kichwa chote
na kuona chanzo Cha tatizo kwa uwazi kabisa .
Asante Sana.
LikeLike
Asante na karibu sana
LikeLike
hakuna sababu yeyote ya kupoa tupo kipndi cha pili kupambana mpaka msuli wa mwisho nila kuangalia mwingine anafanya nini ndio kauli mbiu.
LikeLike
Tumeanzia nyuma, lazima twende kwa kasi sana.
LikeLike
Ni kweli Kocha watu wengi tunaanza mchezo huku tayari tumeshafungwa. Na bado tunarudi kulinda goli. Hii ni hatari kubwa sana. Uvivu na uzembe ndio tatizo kubwa pia kwenye jamii yetu.
LikeLike
Bila kushambulia kwa kasi hii game inaisha tumeshindwa vibaya sana.
LikeLike