3001; Wape ushindi.
Rafiki yangu mpendwa,
Falsafa kuu ambayo ndiyo huwa naendesha nayo huduma zangu, ambayo nilijifunza kutoka kwa Zig Zigler inasema; unaweza kupata chochote unachotaka kwenye maisha yako, kama utawasaidia watu wengi zaidi kupata kile wanachotaka.
Swali ni watu wengi wanataka nini ili uweze kuwapatia na wewe upate unachotaka?
Jibu ni moja, watu wanataka ushindi.
Ushindi ndiyo kitu ambacho watu wengi wanakitaka sana, lakini pia hawakipati.
Na watu wanapokosa ushindi kwao binafsi, wanajipa ushindi usio halisi.
Angalia jinsi ambavyo michezo imepata umaarufu zama hizi, ambapo watu wengi sana wanaifuatilia michezo.
Ni kwa sababu michezo inawapa watu ushindi feki, wanajiona wameshinda wakati siyo ushindi wao.
Pale ambapo timu ambayo mtu anashabikia inashinda, mtu huyo anaona amepata ushindi.
Atatumia nguvu kubwa kusherekea ushindi wa timu yake, kwa sababu tu hana ushindi wa kusherekea kwenye maisha yake.
Tunaona pia wanaowapa watu ushindi huu feki wanapata wanachotaka.
Vyombo vya habari vimekuwa na vipindi vingi vya michezo.
Kumekuwa na wachambuzi wengi wa michezo.
Na hata michezo mingi ya kubahatisha imewekwa kwenye michezo.
Wote walio nyuma ya hiyo michezo wananufaika sana, kwa kuwapa watu ushindi feki.
Sasa hebu pata picha utanufaika kiasi gani kama utawapa watu ushindi halisi.
Lazima watakuwa tayari kukupa kila unachotaka.
Na ushindi halisi namba moja kwa wengi ni kwenye eneo la fedha.
Ndiyo unataka fedha, lakini lazima kwanza uwasaidie watu wengi zaidi kupata fedha nyingi kadiri wanavyotaka.
Kwa kila unachofanya, jiulize kinawasaidiaje watu kupata ushindi kwenye fedha.
Je kinawawezesha watu kuongeza kipato chao au kinawasaidia kupunguza gharama?
Ni lazima uguse eneo moja au yote mawili kama unataka kuwavuta watu kuja kwako na kukupa unachotaka.
Watu wanahangaika na ushindi wa michezo kwa sababu hawana ushindi wa kutosha kwenye maisha yao.
Wawezeshe watu kupata ushindi halisi kwenye maisha yao na wao watakuwezesha kupata ushindi mkubwa unaoutaka kwenye maisha yako.
Hii pia inaenda kwa watu tunaofanya nao kazi, yaani wafanyakazi tunaowaajiri. Kama tunataka wafanye kile tunachowataka wafanye, tuwape ushindi.
Kwa majukumu tunayowapa wafanye, tuweke vigezo ambavyo wakifikia wanakuwa wamepata ushindi.
Hilo litawasukuma kufikia vigezo hivyo na kupata ushindi, kitu kitakachokupa yale unayotaka.
Kwa maana hiyo basi, watu hatari na wa kuwaepuka sana kwenye maisha yako ni watu ambao hakuna ushindi wanaoutafuta.
Hawa ni watu ambao hawawezi kukupa ushindi unaoutaka hata uwafanye nini
Utahangaika nao sana, lakini wataishia kukuangusha.
Tumia njaa ya ushindi kama mchujo wa watu utakaojihusisha nao.
Jihusishe na wale tu ambao wana kiu kubwa ya ushindi kwenye maisha yao.
Ona jinsi utakavyoweza kuwasaidia kupata ushindi mkubwa kwenye maisha yao ili na wao wakuwezeshe wewe kupata ushindi mkubwa kwenye maisha yako.
Usipoteze muda na nguvu zako kwa watu wasio sahihi.
Unataka ushindi, ambatana na wanaotaka ushindi pia.
Wawezeshe kupata ushindi ili nao wakuwezeshe kupata ushindi pia.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#BilioneaMafunzoni
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Ili nipate ushindi ni lazima niwape ushindi wengine. Asante
LikeLike
Hakika
LikeLike
Hakika kocha Kila mtu duniani anatamani kuwa mshindo, wape Watu ushindi wakupe ushindi zaidi
LikeLike
Huo ndiyo mpango mzima.
LikeLike
Asante kocha kwa makala hii
Nitahakikisha nawachuja watu wasiotaka ushindi kwenye maisha yao ili niambatane na watu wanaoutaka ushindi kwenye maisha yao ili wanisaidie na mimi kuupata ushindi ninaoutaka kwenye maisha yangu
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Ahsante na Hongera sana kocha Kwa uandishi wa makala nzuri ya Leo “Wape ushindi”
Nitaifanyia KAZI kwa kuhakikisha team na wateja wangu nawapa ushindi ili nipate ushindi pia kwenye biashara.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Nitajitajhd niwape ushindi
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Nitaambatana siku zote na wale wanaotaka ishindi
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Nitahsinda kama nitawafanya wengine washinde ahsante sana kocha.
LikeLike
Karibu
LikeLike
Nitahakikisha ninawawezesha watu kushinda ili nami nipate ushindi
LikeLike
Vizuri
LikeLike
“Kwa kila unachofanya, jiulize kinawasaidiaje watu kupata ushindi kwenye fedha.
Je kinawawezesha watu kuongeza kipato chao au kinawasaidia kupunguza gharama?.”
Kama unataka fedha, jiulize nimsaidie nani kwenye kile anachotaka Ili na wewe uweze kupata kile unachotaka?
Maishi ni kutoa ushindi kwa wengine kisha asili inakurudishia ushindi.
Asante sana
LikeLike
Hakika
LikeLike
Asante Kocha,
Ninataka ushindi, nitaambatana na wanaotaka ushindi.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Kilamara ninapo husiana na mtu/watu nitahakikisha nawapa ushindi katika kuhusiana nao.
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Wape ushindi kwenye fedha.
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Kwa sababu kila mtu anataka ushindi hapo.
LikeLike
Tukae na watu wanaotaka ushindi na kuepukana na wale wasio utaka ushindi
Asante
LikeLike
Wasiotaka ushindi ni sumu kubwa.
LikeLike
Ushindi unaambukizwa, sawa na kushindwa.
LikeLike
Nitapata ninachotaka kama nitawapa watu wanachotaka
LikeLike
Hakika.
LikeLike
Asante sana kocha kwa Falsafa hii ya kutoka kwa zig zigler,kuwa unaweza kupata chochote unachotaka kwenye maisha yako, kama utawasaidia watu wengi zaidi kupata kile wanachotaka,hii nitaendelea kuhakikisha naitumia sana.
LikeLike
Karibu.
LikeLike
Nitawapa ushindi Wa kifedha wanaoutaka, Ili nipate ushindi Wa kifedha ninaoutaka.
LikeLike
Safi sana.
LikeLike
Nawawezesha wengine kupata ushindi Ili nami nipate ushindi, Asante Kocha.
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Usipoteze muda na nguvu zako kwa watu wasio sahihi.
Unataka ushindi, ambatana na wanaotaka ushindi pia.
Wawezeshe kupata ushindi ili nao wakuwezeshe kupata ushindi pia.
Nitahakikisha Nawapa Ushindi Ili Nao Waniwezeshe Kupata Ushindi.
Ahsante sana Kocha.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Ha ha . . . . Kwa hiyo Arsenal ikishinda na mimi nimeshinda!?
LikeLike
Ha ha haa,
Wewe unakuwa umeisaidiaje Arsenal kushinda?
LikeLike
kwa sasa nitatafuta ushindi halisi namba moja ambao ni kupata fedha nyingi na kupunguza gharama ndipo uhuru ulipo
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Mimi happ huwa ndiyo napata shida sana mpira unachezwa ulaya wewe hapa Tanzania unapoteza muda kuangalia na kurukaruka na bado baadae urudi nyumbani hujaingiza chochote kama siyo kulogwa ni nini
LikeLike
Hawana ushindi kwenye maisha yao, hivyo wanachukua wa kudandia.
LikeLike
Asante kocha mtajitahidi kuwapa watu ili ushindi ili niweze kukamilisha mambo kwenye maisha na kuweza kukamilisha mipango kwenye maisha
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Watu wengi wanahangaika na ushindi wa michezo kwa sababu hawana ushindi wa kutosha kwenye maisha yao.
Na ushindi halisi namba moja kwa wengi ni kwenye eneo la FEDHA.
Kwa hiyo basi unaweza kupata chochote unachotaka kwenye maisha yako, kama utawasaidia watu wengi zaidi kupata kile wanachotaka.
LikeLike
Wasaidie wapate pesa,
Na wewe utapata pesa.
LikeLike