3002; Unajiangusha mwenyewe.
Rafiki yangu mpendwa,
Hakuna mtu yeyote anayeweza kukuangusha kwenye maisha yako isipokuwa wewe mwenyewe.
Chochote unachotaka kwenye maisha na hujakipata, hakuna aliyekunyima ila wewe mwenyewe.
Ni wewe ndiye unayejizuia kupata yale yote unayoyataka kwenye maisha yako.
Na picha linaanzia pale unachotaka hakiendani na kile unachofanya.
Unakuwa unataka makubwa sana, lakini unachofanya ni kidogo sana.
Malengo unayokuwa nayo ni makubwa,
Lakini hatua unazokuwa unachukua ni ndogo sana au wakati mwingine hata haziendani na malengo uliyonayo.
Ni sawa na una safari ya kwenda kisiwani, ambapo usafiri ni wa majini, lakini wewe unaenda kwenye kituo cha basi.
Halafu ukiwa pale unalalamika umeangushwa kwa sababu hujapata usafiri.
Malengo yote makubwa ambayo umewahi kujiwekea kwenye maisha yako na hujayafikia, hakuna mwingine aliyekuzuia isipokuwa wewe mwenyewe.
Ndiyo, panaweza kuwa na changamoto mbalimbali za nje, lakini kama unakuwa umejitoa kweli kweli kutoka ndani yako, hakuna cha kukuzuia.
Hivyo sababu pekee ya kushindwa kwenye maisha ni kujizuia wenyewe.
Kutaka na kupanga makubwa, lakini kuchukua hatua ambazo ni ndogo sana na haziwezi kukupa matokeo unayokuwa unayataka.
Halafu sasa, ni kujitesa.
Kuwa na malengo makubwa, halafu kuchukua hatua ndogo, ni kujitesa kinafsi.
Haina maana kuendelea kutaka vitu vikubwa kama haupo tayari kujitoa kafara ili kuvipata.
Ni kujitesa tu bure, kujitamanisha na makubwa ambayo huwezi kuyapata kwa sababu hujitoi vya kutosha.
Kama unajiona huwezi kuishi aina ya maisha unayopaswa kuishi ili kufikia malengo makubwa uliyonayo, ni bora kuachana na tamaa ya malengo hayo makubwa.
Kama unajiona huwezi kukaa kwenye mchakato unaokupeleka kwenye matokeo unayoyataka, ni bora uachane nayo.
Kutamani matokeo na siyo mchakato ni njia ya uhakika ya kujiangusha wewe mwenyewe.
Na sehemu kubwa ya maisha ya watu imepotelea kwenye hilo.
Wanayatamani sana matokeo, lakini wanapuuza mchakato.
Mwishowe wanayakosa matokeo na kuanza kulaumu wengine.
Kama kuna kitu unakitaka na hujakipata, hupaswi kumlaumu mtu mwingine yeyote.
Unapaswa kuwa kwenye mchakato wa kupata kitu hicho bila ya kuchoka.
Au unapaswa kujilaumu kama hata haupo kwenye mchakato.
Yaani kama bado hujapata unachotaka, unapaswa kuwa kwenye mchakato wa kukipata muda wote bila kuyumba.
Na kama upo kwenye mchakato sahihi, hupaswi hata kuwa na wasiwasi, ni swala la muda tu kupata kile unachotaka.
Lakini kama hujapata unachotaka na pia haupo kwenye mchakato wa kukipata, hupaswi hata kuwa unakizungumzia, iwe ni kwa wema au ubaya.
Hujapata unachotaka na haupo kwenye mchakato wa kukipata basi kaa kimya.
Chochote utakachosema hakina maana.
Kwa sababu utakimbilia kulaumu wengine wakati wewe mwenyewe ndiye uliyejiangusha.
Matakwa yako yaendane na hatua unazochukua.
Kama unataka makubwa, lazima pia uchukue hatua ambazo ni kubwa.
Kama haupo tayari kuchukua hatua kubwa, ambazo pia zitakuukiza, ni bora uachane na tamaa za hayo makubwa.
Kwa sababu ni kujitesa na tamaa kama haupo tayari kujitoa kafara kuzitimiza.
Chochote unachotaka kwenye maisha yako kinawezekana kama upo tayari kulipa gharama ya kukipata.
Kama kuna kitu unataka na hujapata, tatizo ni hujalipa gharama unayopaswa kulipa.
Lipa gharama yote unayotakiwa kulipa bila kujali ukali wake na utaweza kupata kila unachotaka kwenye maisha yako.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#BilioneaMafunzoni
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Nitalipa gharama na kujitoa kwa namna yoyote ili kupata kile ninachokipata
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Kulipa gharama inayostahili.
LikeLike
Hilo halikwepeki.
LikeLike
matamanio makubwa kuna gharama lazima ulipe.
Gharama zenyewe ni;
kukaa kwenye mchakato sahihi ambapo ni kuchukua hatua zinazoendana na lengo lako.
kutoa kafara ya muda,muda wako kujitesa kufanyia kazi ndoto zako huku wengine wakila starehe.Wengine wakiwa wamelala wewe ushaamka na mchakato wa BM
Wengine wakitumia pesa wewe ukiwekeza.Safari siyo rahisi kama lengo ni kubwa lazima kujikana kwenye mengi sana.
LikeLike
Hakuna namna.
LikeLike
Nipo tayari kulipa gharama ya kupata kile ninachokitaka kwenye maisha yangu na kukaa kwenye mchakato ili nipate kile ninachokitaka.
Asante sana kocha.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Kukaa kwenye mchakato, kulipa gharama inayostahili,kuwa na Nidhamu kali ya kuamua na kufanya.
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Kitu chenye thamani kubwa kinahitaji gharama kubwa
LikeLike
Hakika
LikeLike
Kupata chochote unachokitaka ni kukaa kwenye mchakato.
LikeLike
Bila kuyumba.
LikeLike
Asante Kocha;
Kama unataka mambo makubwa ni lazima uchukue hatua ambazo ni kubwa.
LikeLike
Tusijidanganye
LikeLike
Kuwa katika mchakato ndio tiketi ya kiniruhusu hata kuongelea nditi kubwa.
LikeLike
Kabisa
LikeLike
NIPO TAYARI KUCHUKUA HATUA KUBWA
LikeLike
Usirudi nyuma.
LikeLike
Malengo makubwa yaendane na hatua ninazochukua.
LikeLike
Nje ya hapo ni kujidanganya.
LikeLike
🤔 umeniingiza kwenye tafakari ndefu sana, asante kocha
LikeLike
Chukua hatua.
LikeLike
Kweli ni lazima kulipa gharama kwenye maisha ili kufikia lengo malengo makubwa kwenye maisha
LikeLike
Gharama haikwepeki.
LikeLike
lipa gharama ya kupata unachokita bila kujali ukali wake.
nimeelewa vizuri nachopaswa kufanya ili kufika ninapotaka
shukrani kocha.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Nguvu niliyoweka miaka yote itakuwa sawa na kujitesa tu bure, kujitamanisha na makubwa ambayo siwezi kuyapata kwa sababu ya kushindwa kujitoa vya kutosha.
Hivyo nimeamua kujitoa haswaa, kuweka nguvu kubwa na kujitoa hasa kwelikweli, kujitoa kafara Hadi nipate ninachotaka.
LikeLike
Jitoe mzima mzima, usijibakishe.
LikeLike
Nguvu niliyoweka miaka yote itakuwa sawa na bure.
Hivyo nimeamua kujitoa haswaa, kuweka nguvu kubwa na kujitoa hasa kwelikweli, kujitoa kafara Hadi nipate ninachotaka.
LikeLike
Haina maana kuendelea kutaka vitu vikubwa kama haupo tayari kujitoa kafara ili kuvipata.
Ni kujitesa tu bure, kujitamanisha na makubwa ambayo huwezi kuyapata kwa sababu hujitoi vya kutosha.
Ahsante Kocha.
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
“Yaani kama bado hujapata unachotaka, unapaswa kuwa kwenye mchakato wa kukipata muda wote bila kuyumba.
Na kama upo kwenye mchakato sahihi, hupaswi hata kuwa na wasiwasi, ni swala la muda tu kupata kile unachotaka”
Nitakaa kwenye mchakato mwisho wa safari.
LikeLike
Safi sana.
LikeLike
Kupata unachotaka lazima ulipe gharama inayoendana na unachokitaka
Asante
LikeLike
Gharama haikwepeki.
LikeLike
Ni kweli ndoto zangu kubwa haziendani na hatua ninazochukua hapa kuwa bilionea wa dola labda kwa miujiza.
LikeLike
Utayaaga mashindano, kwa uvivu na uzembe wako.
Colonel Sanders alifeli maisha yake yote na kukataliwa sana, ni mpaka alipofika umri wa miaka 65 ndiyo alianza kutoboa kibiashara (KFC) na akafa akiwa tajiri mkubwa.
Wewe kwa nini unakata tamaa mapema sana?
LikeLike
Kweli kabisa, tunajiangusha sisi wenyewe. Hatuna wa kumlaumu bali tujilaumu wenyewe. Tukilopa gharama,tutatoboa tu
LikeLike
Tulipe gharama.
LikeLike
Nalipa gharama yote ninayotakiwa kulipa bila kujali ukali wake na nitaweza kupata kile ninachotaka kwenye maisha yangu.
LikeLike
Safi sana.
LikeLike
Nalipa gharama yote ninayotakiwa kulipa bila kujali ukali wake na nitaweza kupata kile ninachotaka kwenye maisha yangu Asante Kocha.
LikeLike
Mimi Niko tayr na Gharama zenyewe ni;
kukaa kwenye mchakato sahihi ambapo ni kuchukua hatua kubwa zinazoendana na lengo la Ubilionea.
Kutoa kafara ya muda,
Kkujitesa kufanyia kazi ndoto kubwa nilizonazo bila kujali wengine wanasema au kufikiria ni juu yangu.
Wengine wakiwa wamelala wewe ushaamka na mchakato wa BM mapema unachapa kazi.
Wengine wakitumia pesa Mimi Niko UTT nikiwekeza kwenye vipande.
Nitakufa nikitafuta au nitatoboa nikiwahai.
LikeLike
Safi sana, timiza haya uliyojiahidi.
LikeLike