3018; Ushindi wa kiongozi.
Rafiki yangu mpendwa.
Ushindi wa kiongozi yeyote yule huwa unapimwa kwa matokeo anayozalisha.
Viongozi wote bora huwa wanazalisha matokeo makubwa.
Unaweza kuwa kiongozi mwenye huruma, anayejali na maarufu kwa wengi, lakini kama biashara yako itashindwa, hayo yote hayatakuwa na maana.
Kama biashara yako itashindwa, hakuna atakayejali wala kusikiliza sababu na visingizio unavyokuwa navyo.
Hakuna atakayejali kuhusu bahati mbaya ulizokutana nazo.
Kwa kifupi, matokeo yanapokuwa mabaya unakuwa huna popote pa kujificha.
Hayo yote yanaweza yasiwe sawa kwako kama kiongozi, lakini huna namna, utaendelea kuhukumiwa kwa matokeo unayozalisha, bila kujali ni mambo gani unayopitia katika kuzalisha matokeo hayo.
Hivyo ndivyo asili ilivyo, hivyo tunapaswa kwenda nayo hivyo.
Habari njema ni kwamba, kama utakuwa na unga’ng’anizi kwa muda mrefu, kama utaweka mkazo kwenye kutoa huduma bora sana kwa wateja na kama utajenga utamaduni wa nidhamu kali kwa wafanyakazi wako, italipa sana kwa muda mrefu.
Huwezi kuyaathiri matokeo moja kwa moja, lakini unaweza kuathiri moja kwa moja mambo hayo makubwa matatu yenye athari kwenye matokeo.
Unapaswa kuwa kwenye mchakato sahihi wa kukufikisha kwenye matokeo unayotaka kuyapata, kisha kukaa kwenye mchakato huo kwa unga’ng’anizi wa hali ya juu.
Kama mchakato ni sahihi, ni swala la muda tu kuhusu uzalisha matokeo unayoyataka. Anayeng’ang’ana zaidi ndiye anayepata ushindi mwishoni.
Unapaswa pia kuwapa wateja wako thamani kubwa sana na kuwawezesha kupiga hatua kubwa kwenye maisha yao.
Kwa kujali na kuweka mbele maslahi ya wateja wako, unawafanya waendelee kuiamini biashara yako na kuendelea kuwepo pamoja na kuleta wateja wengine wengi zaidi.
Kujenga utamaduni wa nidhamu kali kwa wafanyakazi wako ni jukumu muhimu na ambalo ni gumu sana kwako kama kiongozi.
Watu huwa wanapenda kukaa na kufanya vile wanavyotaka wao wenyewe.
Lakini wanapokuwa kwenye biashara yako, kuna namna wanapaswa kuwa na kufanya.
Hilo linasaidia timu ya biashara kufanya kitu kwa ushirikiano na umoja ambao unakuwa na nguvu ya kuzalisha matokeo bora.
Ni vigumu sana kumshinda kiongozi anayejua kwa hakika nini hasa anachotaka, anayejua mchakato wa kupata anachotaka na kukaa kwenye mchakato huo kwa unga’ng’anizi bila kukata tamaa na anayejenga timu bora na yenye umoja na ushirikiano mkubwa.
KWA NINI, NINI na NANI ni maeneo makubwa matatu ya kila kiongozi wa biashara kujijenga kwa uimara.
KWA NINI ni kile unachotaka, maono ambayo biashara inayo, lazima yawepo na yawe na msukumo kwa kiongozi kuchukua hatua.
NINI ni mchakato wa kufika kule ambapo mtu anataka kufika. Kujua mchakato kamili na kuufuata ni hitaji muhimu sana.
NANI ni watu unaoambatana nao kwenye safari ya kufikia maono ya biashara. Unapaswa kuambatana na timu ambayo ni sahihi kwenye kutekeleza mchakato uliopo.
Kwa kuyakuza maeneo hayo matatu utaweza kuzalisha matokeo bora kabisa kama kiongozi.
Ni wajibu wako kuzalisha matokeo bora na siyo sababu au visingizio vyovyote.
Visingizio vinaweza kuwa rahisi kutamka, lakini mwisho wa siku kinachohesabiwa ni matokeo yaliyozalishwa.
Wewe kama kiongozi bora zalisha matokeo na siyo visingizio.
Uwe na safari njema ya uongozi kwenye biashara yako.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#BilioneaMafunzoni
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Ahsante.
Kwa nini kubwa?
Nini nifanye ( mchakato)
Na nani ( timu imara)
tunataka matokeo na sio sababu.
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Ahsante sana kocha, siku zote nitakuwa kiongozi bora wa kuomgoza maono makubwa ambayo nahitaji kuyafikia kwenye biashara yangu
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Wajibu wangu kama kiongozi ni a matokeo
LikeLike
Zalisha matokeo na siyo sababu.
LikeLike
Kwa nini? Maono makubwa ya TLG kufikia waajiri 50,000
Nini? Mchakato kwa msimamo
Nani? Watu sahihi wa kuambatana nao kufikia maono ndani ya mchakato
LikeLike
Huo ndio mkeka wako, kaa humo.
LikeLike
Kiongozi ni kuzalisha matokeo na siyo sababu.
Mara zote tunapaswa kuwa watu wa kuzalisha matokeo.
Asante sana
LikeLike
Hakika
LikeLike
Nitangangana mpaka nipate mafanikio
LikeLike
Safi sana.
LikeLike
Muhimu kwangu ni matokeo, nitajitahidi mara zote kukaa kwenye mchakato
LikeLike
Yapambanie hayo.
LikeLike
why (kwa Nini): What ( Nini) , and Who. ( Nani) ni MANENO niliyozoea kuwafundisha wanafunzi wetu kazini lakini dikuyaoanisha kwenye uongozi wa biashara.
Asante Sana kocha
LikeLike
Sasa umeshaweza kuyaoanisha, yafanyie kazi.
LikeLike
Mimi kama kiongozi Bora nazalisha matokeo na sio sababu.
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Kama kiongozi ni wajibu wako kuzalisha matokeo na sio sababu.
Tumia maneno kwa nini, mini, na nani kama kiongozi ili uzalishe matokeo bora.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Kama kiongozi Bora nazalisha matokeo makubwa, na siyo visingizio.
Haijalishi magumu Gani napitia bado nitapimwa Kwa matokeo ninayozalisha.
LikeLike
Zalisha matokeo na siyo sababu.
LikeLike
Kinachojalisha ni matokeo.
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Wewe kama kiongozi Bora zalisha matokeo na sio visingizio
Asante
LikeLike
Tuzalishe matokeo.
LikeLike
Asante sana kiongozi bora ni pamoja na kuonyesha matendo
LikeLike
Onyesha matokeo.
LikeLike
Asante kocha
Nidhamu Kali inahitajika kufikia mafanikio
LikeLike
Hakika.
LikeLike
Kionozi ni sawa na timu ya mpira. Ushindi unapimwa kwa magoli na siyo chenga nyingi. Magoli ndiyo matokeo. Kiongozi naye anapimwa kwa matokeo na siyo kitu kingine.
LikeLike
Tuyape kipaumbele matokeo.
LikeLike
Hakika matokeo tu, sababu hazina manufaa kwa watu
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Nitakuwa kiongozi ninayezalisha matokeo bora kwenye biashara yangu.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
👉Kwanini kuleta suluhisho la furniture (MVFF)
👉NINI focus,msimamo na kasi
👉NANI mchakato,uzalishaji na timu imara
Shukrani kocha,tupo pamoja.
LikeLike
Kaa humo.
LikeLike
Ni kweli maneno haya ya KWANINI, NINI na NANI ni maeneo ambayo yanakubalika sana kukupeleka kwenye malengo yako
Kujua ni kqanini unafanya hilo nini unachopaswa kufanya na unaambatana na watu gani ahsante sana kocha
LikeLike
Hakika
LikeLike
matokeo yanapokuwa mabaya unakuwa huna popote pa kujificha.
LikeLike
Matokeo yanakuanika wazi.
LikeLike
Ni jambo muhimu kukaa kwenye mchakato kwa kupata matokeo bora
LikeLike
Hakika.
LikeLike
Napaswa kuzalisha matokeo mimi kama kiongozi na si kutoa sababu na visingizio,mana nitapimwa kwa mateo na si visingizio au sababu
LikeLike
Safi sana.
LikeLike
Nataka kuwa na unga’ng’anizi kwa muda mrefu, kuweka mkazo kwenye kutoa huduma bora sana kwa wateja na kuajenga utamaduni wa nidhamu kali kwa wafanyakazi italipa sana kwa muda mrefu.
Nidhamu uadilifu na kujituma ndiyo nguzo kuu
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike