3053; Turudi kwenye misingi.
Rafiki yangu mpendwa,
Iwapo unajenga nyumba ya ghorofa, lakini kila unapojaribu kwenda ngazi za juu zaidi unakwama, hapo inabidi urudi kwenye msingi.
Unapaswa kuangalia msingi mzima ambapo ghorofa hiyo imejengwa na kama utagundua msingi siyo sahihi basi unapaswa kuuboresha kwanza kabla hujaendelea.
Hivyo pia ndivyo ilivyo kwenye kila safari ya mafanikio kwenye maisha yako.
Unaweza kuwa unajua kile unachotaka na ukawa tayari unaweka juhudi ili kukipata.
Lakini licha ya juhudi zote unazoweka, bado inakuwa vigumu kupiga hatua.
Changamoto hii ni kubwa zaidi kwa wale ambao tayari wana timu kwenye biashara zso.
Timu inakuwepo na hatua zote muhimu zinafanyiwa kazi.
Lakini tatizo kubwa linabaki pale pale na hakuna hatua kubwa zinazokuwa zimepigwa.
Na hii inaanzia pale ambapo kiongozi anaona hawezi kufanya yale ambayo wafanyakazi wanayafanya.
Tunaona jukumu letu kuu ni kuwaelekeza yale wanayopaswa kufanya.
Na kweli tunawaelekeza vizuri, lakini inapokuja kwenye kufanya, huwa hawafuati maelekezo tuliyowapa, bali wanaiga yale ambayo unayafanya.
Kwa kifupi unaweza kuongea sana, lakini watakachofanya watu siyo kile unachosema, bali kile unachofanya.
Watu wanakuiga kuliko wanavyokusikiliza.
Hivyo basi, kama juhudi tunazoweka ili kukuza biashara yako hazileti matokeo unayoyataka, ni vyema kuingia ndani na kupambana kuijenga biashara yako.
Ni muhimu urudi kwenye misingi yako yote ambayo uliitumia wakati unaanza na ukaweza kupiga hatua kubwa.
Ni wakati sasa wa kurudi kwa kina ndani ya biashara yako, ufanye kwa vitendo na kuongoza kwa mfano kama ulivyojitoa wakati unaanza.
Kwa kufanya hivyo, timu yako itasukumwa kuwa bora zaidi kupitia yale wanayofanya au wale ambao wanaona hawawezi kwenda na kasi hiyo wanajiweka pembeni.
Unapokuwa hukifanyi kitu kwa karibu ni rahisi sana watu kukudanganya.
Lakini pale unapokuwa mfanyaji mkuu, watu hawawezi kuja na mambo ya uzushi kwako.
Kuna maeneo mengi ya kufanyia kazi kwenye biashara yako.
Lakini eneo moja muhimu sana ambalo unapaswa kulijua kwa kina na kulifuatilia kwa karibu kwenye biashara yako ni mauzo.
Na hapo ndipo unapopaswa kuweka juhudi zako zote, kuhakikisha unaijenga biashara yako kuwa mashine ya mauzo.
Kwa kujenga misingi sahihi ya mauzo kwenye biashara yako, unaipa biashara hiyo nafasi nzuri ya kukua.
Tayari tunao mchakato sahihi wa mauzo, ambao ukifanyiwa kazi unapelekea mauzo kukua zaidi kwenye biashara.
Rai yangu kwako ni wewe kurudi kwenye misingi sahihi ya kujenga na kukuza biashara yako.
Kwa kukaa vyema kwenye mchakato sahihi, kunazalisha matokeo bora kabisa.
Haijalishi biashara yako imekuwa kubwa kiasi gani.
Wala haijalishi imeajiri wafanyakazi wangapi.
Kama wewe mmiliki wa biashara hautakaa kwenye misingi sahihi, kazi yako itakuwa mara mbili. Yaani utawaajiri watu na bado utalazimika kurekebisha kazi zao.
Kuna majukumu makubwa mawili ambayo nataka uyashike kwa kina kwenye biashara yako kwa sasa.
Jukumu la kwanza ni kuwa meneja mkuu wa biashara, hapo unahakikisha kila kitu kinatekelezwa kama kilivyopangwa.
Jukumu la pili ni kuwa muuzaji bora kabisa kuwahi kutokea. Kwa kuwa vizuri kwenye mauzo unatengeneza nafasi za ukuaji zaidi.
Usiruhusu sababu zozote zile kukuzuia kutekeleza majukumu hayo makubwa mawili.
Hayo ndiyo kipaumbele cha kwanza kwako hivyo unapaswa kutatekeleza kwa msimamo kila mara bila kuacha.
Lengo letu ni kujenga uhuru kutoka kwenye biashara zetu.
Lakini hatuwezi kufika huko kama misingi haijakaa sawa.
Turudi kwanza kwenye misingi ili kuweza kusimama imara na kuendesha biashara yenye mafanikio.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Kusimamia kuhakikisha mambo yanafanyika kama yalivyopangwa na kuwa muuzaji mkuu.Haya ndio majukumu yangu makuu.
LikeLike
Kuwa meneja mkuu wa biashara na kuwa muuzaji bora kuwahi kutokea.
LikeLike
Tukifaulu hayo mawili tumemaliza.
LikeLike
watu awafati unachosema bali unachofanya. nitafanya ili niwe muuzaji bora na meneja bora .
ahsante
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Hili linanipelekea kurudi nyuma ili kuanzia keenye msingi moja ntarudi kukaa reseption nusu siku na nusu nyingine ntatoka kusaka hili nitalifanya mfululizo mwezi kuanzia leo hadi kuona mababadiliko
LikeLike
Vizuri sana Dickson, ikiwezekana siku nyingine kaa mwanzo mwisho ili uone mambo yanavyoenda, Tenga hata siku mbili katika wiki kukaa mapokezi, kwa mfano Jumatatu na jumanne ujue mambo yanaendaje.
LikeLike
Wazo zuri sana, lazima tuone nini kinakwamisha mauzo.
LikeLike
Vizuri sana, unaweza kuhangaika sana kutafuta wateja, halafu wakifika kwenye biashara wanapewa huduma mbovu. Ni wajibu wetu kuhakikisha sehemu zote zimekaa sawa.
LikeLike
Watu wanakuiga,kuliko kukusikiza,kama kiongozi nahitaji kuongoza kwa matendo siyo maneno.Asante kocha.
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Nitakaa katika mchakatu na kuendelea kuwahimiza vijana.
Kuwa meneja na muuzaji Bora kuwahi kutokezea
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Mimi meneja mkuu nina majuku mawili, Kuisimamia mambo kamam yalivyo pangwa na kuuwamuuzaji bora kuwahi kutokea.
LikeLike
Kamilisha hayo kwa uhakika.
LikeLike
Asante kocha,nitarudi kwenye misingi ili biashara yangu iwe na mafanikio na kuwa makini na mauzo.
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Majukumu makubwa nayoyatekeleza kwenye biashara yangu kwa sasa ni meneja mkuu kwa kusimamia maendeleo ya biashara kwenye masoko mauzo na timu na ni muuzaji bora kuwahi kutokea kwenye biashara yangu
LikeLike
Yakamilishe majukumu hayo kwa uhakika.
LikeLike
Kwa kifupi unaweza kuongea sana, lakini watakachofanya watu siyo kile unachosema, bali kile unachofanya.
Watu wanakuiga kuliko wanavyokusikiliza
Asante sana
LikeLike
Huo ndiyo ukweli.
LikeLike
Mauzo ni moyo wa biashara na Masoko ni mapafu ya biashara. Eneo moja muhimu sana ambalo ninapaswa kulijua kwa kina na kulifuatilia kwa karibu kwenye biashara yangu ni mauzo. Asante sana Kocha.
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Ahsante sana kocha, nakwenda kuwa meneja mkuu na muuzaji bora kuwa kutokea ili kuongeza ufanisi katika biashara yangu
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Nina majukumu makubwa mawili kwenye biashara yangu:
1- kuwa Meneja mkuu wa biashara yangu,kwa kuhakikisha kila kitu kinatekelezwa kama kilivyopangwa.na
2- kuwa Muuzaji bora kabisa kuwahi kutokea. Asante sana Kocha.
LikeLike
Kila la kheri katika kutekeleza majukumu hayo mawili.
LikeLike
Asante sana kocha, msingi ukiwa imara na nyumba inakuwa imara. Msingi ndiyo umebeba nyumba.
LikeLike
Hakika.
LikeLike
Asante Kocha ninapaswa kuangalia msingi na kufanya kile kinachotakiwa kama meneja na muuzaji
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Nipo najenga msingi
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Narudi kwenye misingi ili kuweza kusimama imara na kuendesha biashara yangu kwa mafanikio.
Nitakuwa meneja mkuu kwenye biashara yangu na muuzaji bora kuwahi kutokea
Asante
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Kurudi kwenye Misingi na kufanya yaliyo kipaumbele kwa biashara yangu na uwekezaji
LikeLike
Hakika
LikeLike
Asante sana kocha kwenda kuwa manager wa biashara zetu zitarudi.kukua zaidi maana tunarudi kwenye mchakato msingi na kurekebisha pale palipo bomoka
LikeLike
Hongera sana Elihuruma kwa kuanza kusoma kurasa. Nimefurahi mno kuona umekomenti.
LikeLike
Ni hatua nzuri, awe na mwendelezo.
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Unapokuwa hukifanyi kitu kwa karibu ni rahisi sana watu kukudanganya.
LikeLike
Kweli
LikeLike
Nitarudi kwenye msingi kwa kutekeleza kila kitu kwa vitendo ili wale walioko chini yangu waweze kujifunza kwa kuona. Asante sana kocha.
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Majukum yangu makubwa 2 ni kuwa meneja mkuu,na kuwa muuzaji bora.
LikeLike
Yafanye kwa ubora wa hali ya juu sana.
LikeLike
watu wanakuiga kuliko kukusikiliza
LikeLike
Huo ndiyo ukweli.
LikeLike
Kuna maeneo mengi ya kufanyia kazi kwenye biashara yako.
Lakini eneo moja muhimu sana ambalo unapaswa kulijua kwa kina na kulifuatilia kwa karibu kwenye biashara yako ni mauzo.
Na hapo ndipo unapopaswa kuweka juhudi zako zote, kuhakikisha unaijenga biashara yako kuwa mashine ya mauzo.
Asante sana Kocha Dr Makirita Amani
LikeLike
Hakika.
LikeLike
Naenda kuwa Meneja Mkuu wa biashara yangu na muuzajj bora kabisa kuwahi kutokea
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Turudi kwanza kwenye misingi ili kuweza kusimama imara na kuendesha biashara yenye mafanikio.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Mimi ni muuzaji Bora kabisa kuwahi kutokea
Mimi ni meneja mkuu Wa biashara_nahakikisha kila kilichopangwa kinafanyika kama kilivyopangwa.
Naonyesha mfano kwenye timu Kwa kufanya zaidi kuliko kuongea sana
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Ni muhimu kuendelea kukaa kwenye misingi
LikeLike
Kabisa.
LikeLike