3055; Usijipe kazi usizoziweza.
Rafiki yangu mpendwa,
Safari ya mafanikio ambayo tupo ni safari ngumu na ndefu.
Ugumu wa safari hii ni kazi kubwa tunayopaswa kuweka ili kupata matokeo makubwa tunayotaka kuyapata.
Wengi huwa wanashindwa kazi hiyo, siyo kwa sababu haiwezekani, bali kwa sababu wanachoka kwa kazi nyingine wanazokuwa wamejipa.
Yaani wanakuwa wamejipa kazi ambazo zinachukua nguvu na muda wao, lakini hazina matokeo mazuri kwao.
Kuna kazi kubwa tatu ambazo watu wamekuwa wanajipa na zinaishia kupoteza muda wao na kuwa kikwazo kwao kufanikiwa.
Ya kwanza ni kutaka kubadili watu.
Hapa mtu anachagua kujihusisha na watu ambao hawana tabia wanazozitaka, ila wanajiambia watawabadili watu hao.
Hakuna kitu kinachowapoteza watu kama hitaji la kuwabadili watu wengine.
Wanahangaika sana kwa kila namna, lakini hakuna mafanikio wanayoyapata.
Watu huwa hawapendi kubadilishwa.
Wanaweza kuamua kubadilika wao wenyewe kama watataka na kuwa tayari kujitoa, lakini siyo kubadilishwa na watu wengine.
Ili upeleke juhudi zako zote kwenye mafanikio, ni vyema uchague kwenda na watu ambao tayari wana tabia unazotaka na huhitaji kuwabadilisha.
Anza na watu ambao wanaweza kutekeleza kile unachotaka kitekelezwe bila ya kulazimishwa kufanya hivyo.
Na hapo unakuwa umeshashinda nusu ya kazi unayopaswa kuweka ili matokeo yapatikane.
Ya pili ni kutaka kumfurahisha kila mtu.
Hivi umewahi kugundua kwamba biashara zilizojikita kwenye kuwafurahisha watu ndizo zinazotoza gharama kubwa sana?
Ndiyo, angalia burudani nyingi bora na kubwa. Watu wanalazimika kuingia gharama kubwa kuzipata.
Hiyo ni kwa sababu ni kazi kubwa sana kuwafurahisha watu.
Halafu sasa, ni jambo lisilowezekana kumfurahisha kila mtu.
Kwa mfano hata burudani ambayo ni ghali sana na inawapa watu furaha kubwa, huwa siyo kwa kila mtu.
Kuna mtu hata akipewa burudani hiyo bure, hatakuwa tayari kuipokea.
Anza kwa kujifurahisha wewe mwenyewe, kwa kufanya kile kinachokupa burudani na hapo utawaalika wale ambao wanaburudika na hicho unachoburudika wewe.
Kwa kuwa unaburudika, utakuwa tayari kufanya kwa ukubwa zaidi na hapo utaendelea kuwafurahisha wale wanaoelewa kitu hicho.
Lakini wakati huo huo kuna watu utakuwa unawatibua na kuwaudhi sana kwa hicho unachofurahia wewe.
Na hilo siyo tatizo lako wewe, bali ni tatizo lao binafsi, hivyo hakuna unachoweza kufanya.
Huwezi kumfurahisha kila mtu hata ufanyeje.
Na mbaya zaidi, unapofanikiwa, utafanikiwa pia kuwachukiza baadhi ya watu.
Kuna watu ambao wataona hustahili kupata mafanikio uliyoyapata.
Na hapo huna namna ya kuwabadili, zaidi ya kuwaacha na kisirani chao wenyewe.
Ya tatu ni kuwahamasisha watu.
Hii ni ngumu kidogo kueleweka na kukubalika, ila twende nayo taratibu.
Watu wanahitaji hamasa ili kufanya mambo makubwa.
Hamasa zipo za aina mbili; ya nje na ya ndani.
Hamasa ya nje ni ile inayotoka kwa watu wengine, hii huwa haidumu kwa muda mrefu.
Hamasa ya ndani ni ile inayoanzia ndani ya mtu mwenyewe, hii huwa inadumu kwa muda mrefu.
Lengo la kuwahamasisha watu kwa nje ni kuibua hamasa ya ndani yao ambayo itawasukuma watu kwa muda mrefu.
Lakini kama utawapa watu hamasa ya nje, huku ndani yao wakiwa hawaha hamasa, ni sawa na kuwasha kuni mbichi, utapoteza nguvu nyingi na hazitawaka.
Epuka sana kuwahamasisha watu ambao ndani yao hawana hamasa kabisa.
Badala yake chagua kwenda na watu ambao tayari wana hamasa kubwa ndani yao na kinachohitajika ni wewe kuiibua na kuwapa msukumo wa kwenda zaidi.
Hiyo ni kwa wafanyakazi, washirika na hata wateja.
Ukitegemea hamasa unayowapa watu ndiyo iwasukume kupiga hatua, utagundua wanafanya pale unapowapa hamasa na ukiacha kuwapa hamasa nao wanaacha kufanya.
Hapo unakuwa umejipa kazi ngumu ya muda wote kuwapa watu hamasa, kitu ambacho kinakuwa kikwazo kwako kufanya mambo mengine muhimu.
Unapotaka kupata moto, unaweka kazi kwenye kuwasha nishati iliyopo, iwe ni kuni, mkaa, mafuta au gesi. Ukishaweka nguvu ya mwanzo ya kuwasha, moto unaendelea kujichochea wenyewe kwa nguvu iliyo ndani ya nishati husika.
Huhitaji kuwa unapepea moto huo wakati wote ndiyo uwake.
Hivyo ndivyo ilivyo kwenye hamasa. Hamasa yako ya nje inapogusa mtu mwenye hamasa ya ndani, anaendelea kuhamasika na kutokuhitaji hamasa yako kila mara.
Lakini unapohamasisha watu ambao hawana hamasa ya ndani, unahitajika kuendelea kutumia hamasa yako muda wote. Inakuwa ni sawa na kuwasha kuni mbichi, ukiacha kuchochea zinazima.
Safari ya mafanikio inaweza kutuchosha na bado mafanikio yenyewe tusiyapate kama nguvu zetu zinapotelea kwenye maeneo yasiyokuwa sahihi.
Peleka nguvu zako kwenye kazi zilizo sahihi kwako ili uweze kuzalisha matokeo yenye tija na yatakayokupa mafanikio makubwa.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Ni vigumi sanaa kuwabadilisha watu na tabia zao lakini tupambane sisi wenyewe na kufanya yake sahihi na bila kujali wao wanafurahia au wanachukizwa nayo wabadilishe kwa wao kujifunza kutoka kwako na lingine nililoliona kumbe watu wengine hawakua wanataka wewe ufanikiwe bali walitaka wewe ubaki chini hivyo waonyeshe kwa kufanikiwa kwako kuwa kumbe inawezekana kwa kufanya bidii tusitake kuwalazimisha watu kubadilika nje bila wao kubadilika ndani kwanza
LikeLike
Umesema vyema, tupambane na yetu, kujihangaisha na ya wengine ni kujikwamisha.
LikeLike
Napeleka nguvu zangu kwenye kazi zilizo sahihi kwangu ili niweze kuzalisha matokeo yenye tija kwangu na yanayonipa mafanikio makubwa.
Sitaweza kumfurahisha au kumhamasisha mtu kama hivi vitu havitaanzia ndani ya mtu husika,napaswa kujihamasisha na kujifurahisha mimi mwenyewe kwanza mana ni vitu ambavyo vinaanzia ndani yangu.
Asante sana kocha.
LikeLike
Hakika.
LikeLike
Asante sana kocha, hamasa ni kama vile starter kama gari Ina uwezo itakimbia na kufikia kwa wakati, lakini kama Haina uwezo itachelewa haijalishi Ina starter au Haina.
LikeLike
Mfano mzuri, kama gari haina mafuta, hata upige stater kiasi gani, hakuna mahali unaenda.
LikeLike
Nitapeleka nguvu zangu kwenye kazi iliyo sahihi
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Kuwahamasisha watu wasiokuwa na hamasa ya ndani ni sawa na kuwasha kuni mbichi.
LikeLike
Utapata tabu sana kufanya hivyo.
LikeLike
Napeleka nguvu zangu kwenye kazi zilizo sahihi.
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
NITAFANYA YALIYO SAHIHI NA MUHIMU
ILI KUOKOA NGUVU ZNG.
asante kocha.
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Asante kocha nitaweka nguvu kubwa kwenye mambo ambayo ni sahihi kwangu ili niweze kupata mafanikio.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Asante sana Kocha najifurahisha mimi mwenyewe kwa kufanya kile kinachonipa burudani.
LikeLike
Safi sana.
LikeLike
Ili upeleke juhudi zako zote kwenye mafanikio, ni vyema uchague kwenda na watu ambao tayari wana tabia unazotaka na huhitaji kuwabadilisha.
Anza na watu ambao wanaweza kutekeleza kile unachotaka kitekelezwe bila ya kulazimishwa kufanya hivyo.
Na hapo unakuwa umeshashinda nusu ya kazi unayopaswa kuweka ili matokeo yapatikane.
Asante sana
LikeLike
Kabisa, tunapoteza nguvu nyingi kwenye mambo yasiyo sahihi.
LikeLike
Asante sana kocha,sipo tayari kujichosha na kushindwa kuyafikia mafanikio yangu kwa kuhangaika na watu.
LikeLike
Vizuri, simamia hilo.
LikeLike
Asante sana kocha, somo hili binafsi nimeelewa vyema sana sipo tayari kujichosha na kushindwa kuyafikia mafanikio kwa kuhangaika na watu wengine wanasema nini.
LikeLike
Vizuri, fanyia kazi.
LikeLike
Kazi ngumu humu duniani ni kutaka kuwafanya watu wawe vile unataka wewe
LikeLike
Ngumu mno.
LikeLike
Nitaeleleza nguvu znagu kwenye kazi na mambo yenye tija katika mafanikio yangu. Na kamwe sitafanya kazi ya kumfurahisha kila mtu
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Asante Kocha, Nifanye yangu,na niwaachie wengine wafanye yao.
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Nitapeleka nguvu zangu kwenye kazi zilizo sahihi ili niweke kuzalisha matokeo yenye tija na yatakayonipa mafanikio makubwa.
Natambua kuwa siwezi kuwabadilisha watu na siwezi kumfurahisha kitu mtu.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Peleka nguvu zako kwenye kazi zilizo sahihi kwako ili uweze kuzalisha matokeo yenye tija na yatakayokupa mafanikio makubwa, asante Sana Kocha, nitaendelea kupeleka nguvu zangu kwenye kazi sahihi.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
1, La kubadili watu uwa siangaiki nalo
2, Kufurahisha watu si hangaiki nalo.
3, La kuhamasisha watu hasa TIMU yangu huwa nalifanya sana. kwa kuwa mimi ndio muhamasishaji mkuu.
Ila sasa nita tafakari kama kuni hizi ni kavu au mbichi,
LikeLike
Kuhamasisha siyo mbaya, ila sasa lazima uangalie kama kuni ni mbicho au kavu. Maana usijekuwa unapoteza nguvu ambazo ungeweza kuzitumia vizuri mahali pengine.
LikeLike
Safari ya mafanikio inaweza kutuchosha na bado mafanikio yenyewe tusiyapate kama nguvu zetu zinapotelea kwenye maeneo yasiyokuwa sahihi.
Peleka nguvu zako kwenye kazi zilizo sahihi kwako ili uweze kuzalisha matokeo yenye tija na yatakayokupa mafanikio makubwa.
LikeLike
Hakuna kinachochosha kama kutawanya nguvu.
LikeLike
Nguvu zangu daima zinaenda katika mambo sahihi ili kuleta matokeo sahihi.
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Nimeamua vyema kupeleka nguvu zangu zote kule ambako kunazalisha matokeo
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike