3287; Mabadiliko ya watu.
Rafiki yangu mpendwa,
Moja ya vitu vigumu sana kutokea ni watu kubadilila.
Mabadiliko huwa ni kitu kigumu sana kwa watu kiasi kwamba ukiona yametokea kweli, basi mtu anakuwa amelipa gharama kubwa sana.
Katika hali za kawaida, watu huwa hawabadiliki.
Kile ambacho kwa nje tunaweza kuona kama ni mabadiliko ya mtu, huwa ni mtu kurudi kwenye uhalisia wake baada ya kuchoka kuigiza.
Pale unapoona mtu amerudi nyuma ukilinganisha na alivyokuwa anafanya awali, anakuwa hajarudi nyuma, bali hakuwa vizuri kama ulivyodhani.
Huenda ulikuwa unamwona kwenye nyakati nyepesi na kudhani anafanya makubwa, kumbe siyo.
Hata pale unapoona watu wamepiga hatua fulani kubwa kwenye maisha yao, siyo kwa sababu ndiyo wamekuwa bora kuliko walivyokuwa huko nyuma. Bali wanakuwa wamepata fursa ya kudhihirisha uwezo mkubwa ambao tayari upo ndani yao.
Ni asili ya binadamu kwamba watu huwa hawabadiliki. Hivyo chochote unachokiona kama mabadiliko kwa mtu, ni anakuwa tu amechoka kuigiza na kuamua kuwa halisi kwao.
Kumbuka hili mara zote ili usishangazwe na watu.
Na kwa upande wako, yaishi maisha yako halisi mara zote ili watu waweze kukutegemea kwa uhakika kwenye kile unachofanya.
Pale watu wanapokuwa na uhakika na mtu, wanafanya naye kazi kwa muda mrefu na manufaa yanakuwa mazuri kwa wote.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Tuyaishi maidha yetu ya uhakika na siyo ya kuigiza na tufanye kazi hiyo kwa uhakika ili tuweze kuaminika na kukubalika
LikeLike
Hakika.
LikeLike
Kile unachoona kama ni watu wamebadilika sio mabadiliko bali ni mtu amechoka kuishi kwa maigizo hivyo ameamua kurudi kwenye uhalisia wake.
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
“chochote unachokiona kama mabadiliko kwa mtu, ni anakuwa tu amechoka kuigiza na kuamua kuwa halisi kwao.”
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Katika hali za kawaida, watu huwa hawabadiliki.
Kile ambacho kwa nje tunaweza kuona kama ni mabadiliko ya mtu, huwa ni mtu kurudi kwenye uhalisia wake baada ya kuchoka kuigiza.
Ahsante sana Kocha.
Nimekuelewa vema.
LikeLike
Karibu
LikeLike
Hakuna mtu ambaye anaweza kuigiza kwa muda mrefu.
Hivyo kile ambacho mtu huwa anaonesha basi jua ndiyo asili yake ilivyo.
Asante sana Kocha Dr Makirita Amani.
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Unapoona watu wamepiga hatua fulani kubwa kwenye maisha yao.
Wanakuwa wamepata fursa ya kudhihirisha uwezo makubwa ambao tayari upo ndani yao.
Shukrani kocha.🙏
LikeLike
Karibu
LikeLike
Asante kocha
LikeLike
Karibu
LikeLike
Ni sahihi kabisa, kubadilika kuna gharama kubwa sana hasa kubadilika kwa improvements.
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Ili niweze kutegemea lazima kuishi maisha yangu kwa uhalisia.
Watu Huwa hawabadiliki Bali wanakuwa wamechoka kuigiza
LikeLike
Ndiyo
LikeLike