3303; Wa kumfuata mwenzake.
Rafiki yangu mpendwa,
Pale unapokuwa unashirikiana na watu wengine, na wewe ukawa uko mbele zaidi ya hao wengine, huwa unafanya nini ili muweze kwenda pamoja?
Kwa walio wengi huwa wanapunguza kasi yao na kuwasubiri hao wengine ili waambatane nao.
Hapo wanakuwa wameshusha viwango vyao ili kuweza kueleweka na wengine ambao viwango vyao chini.
Kwa wachache wanaopata mafanikio makubwa wanayokuwa wanayataka, huwa wanawataka wengine kuongeza kasi ili wawafikie.
Wanakataa kushusha viwango vyao ili kueleweka na wengine.
Badala yake wanawataka hao wengine kukuza viwango vyao ili wawafikie na kuweza kushirikiana vizuri.
Rafiki, swali linakuja kwako unatumia njia ipi?
Je unapunguza kasi ili wengine wakufikie mwende pamoja?
Au unaendelea na kasi yako na kuwataka wengine nao waongeze kasi ili waweze kukufikia.
Kujenga mafanikio makubwa, lazima ushirikiane na wale wanaoongeza kasi ili kukufikia.
Hao wanakupa msukumo wa kuendelea kufanya makubwa zaidi.
Watu wote wanaojihusisha na wewe wanatakiwa kuielewa sheria yako rahisi inayosema; panda kufikia viwango vyangu au nisikuone kwenye maisha yangu.
Simamia viwango vyako mara zote ili kuhakikisha wengine wanapambana kuvifikia ndiyo waweze kushirikiana na wewe.
Kataa mengine yote ambayo yapo chini ya viwango vyako, hivyo ndivyo unavyoweza kujenga mafanikio makubwa na ya uhakika.
Ni muhimu kila wakati kujikumbusha malengo yako makuu ili usiingie kwenye mtego wa kudhani kuwafurahisha wengi zaidi ndiyo mafanikio.
Mafanikio kwako ni kupata matokeo makubwa unayoyadhamiria.
Hilo halitawezekana kama pia unataka kila mtu ajisikie vizuri.
Mafanikio makubwa yanamtaka mtu ajitoe kisawasawa. Wale wanaotaka wewe ushushe viwango ndiyo muweze kushirikiana badala ya wao kukuza viwango, siyo ambao wanaweza kukusaidia wewe kupata mafanikio makubwa unayoyataka.
Wajibu wako mkubwa kwenye maisha ni kupata kile unachotaka hasa na siyo kuwafanya wengi wajisikie vizuri.
Na ili kupata unachotaka, lazima uwasukume wengi wapandishe viwango vyao ili kufikia viwango vyako wewe.
Hakikisha hilo ndiyo unalofanya na siyo kinyume na hapo.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Siku zote watalazimika kupandisha viwango vyao kufikia viwango vyangu.
LikeLike
Kabisa, hakuna kuwalegezea.
LikeLike
Na ili kupata unachotaka, lazima uwasukume wengi wapandishe viwango vyao ili kufikia viwango vyako wewe.
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Mafanikio makubwa yanamtaka mtu ajitoe kisawa sawa na kuongeza viwango mara Kwa mara
Asante
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Sitapunguza kasi ili wengine wanifikie twende pamoja bali nitaendelea na kasi yangu kuwataka wengine nao waongeze kasi ili waweze kunifikia.
LikeLike
Kabisa,
Ongeza kasi.
LikeLike
Asante Kocha,
Wajibu wangu mkubwa kwenye maisha ni kupata kile ninachotaka hasa, na siyo kuwafanya wengine wajisikie vizuri.
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Fikia viwango vyangu au ondoka kwenye maisha yangu, kamwe sitashusha viwango Ili kumuacomodate mtu yoyote.
LikeLike
Vizuri sana, wapambane.
LikeLike
Asante kocha mtapambana kupandisha viwango mara zote
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Nitakaa kwenye viwango vyangu, na wengine watatakiwa kupandisha viwango vyao ili kuvifikia vya kwangu.
LikeLike
Ndiyo, wapambane.
LikeLike
Asante sana,,,
LikeLike
Karibu.
LikeLike
Ni kweli dawa ni kutoshusha viwango ili kuwasubiria ni wao waongeze kasi ya kunifuata au aapotee
LikeLike
Kabisa.
LikeLike