
Karibu rafiki tujifunze wote,
“Kitu pekee kinachokomboa mwanadamu ni ushirikiano” Alisema, Bertrand Russell
“Nguzo moja haitoshi kujenga nyumba”. Alisema, Rais wa China Xi Jinping. Pia, aligongezea kuwa “Kwenda ni kugumu kunapofanywa peke yako; kwenda hurahisishwa pale kunapofanywa na wengine wengi”.
“Mto una kina kirefu kwa sababu ya chanzo chake”.
“Amani sio tu kutokuwepo kwa vita. Bali ni hali ya ushirikiano, heshima na upendo kati ya watu. Succes Path Network.
“Ukitaka kwenda haraka, nenda peke yako. Ukitaka kufika mbali, ungana na wengine”.
Tunapozungumzia ushirikiano tunamaanisha, mchakato ambao watu wawili au zaidi hufanya kazi pamoja ili kufikia lengo moja.
Ushirikiano ni wakati watu wawili au zaidi wanafanya kazi pamoja kufikia lengo moja. Timu zinaundwa na watu ambao wana ujuzi tofauti. Hii hufanya timu kuwa za kipekee ikilinganishwa na aina zingine za vikundi. Kazi inafanywa na timu, lakini kazi ya pamoja pia ni muhimu sana.
Ushirikiano ni ufunguo wa kuendesha biashara yenye mafanikio makubwa. Wahenga wanasema, “Palipo na watu wawili halikosi jambo”. Pia, waliongezea kuwa; Jicho la pili lina nguvu zaidi kuliko jicho mojal. Kwahiyo ni muhimu kuendelea kuonyesha ushirikiano na wengine wakati wa utendaji kazi.
Nia zikiungana kilicho mbali huja.
Ushirikiano katika sehemu za kazi unamaanisha kwamba kila mtu anafanya kazi pamoja kutatua matatizo. Wafanyakazi na wasimamizi wanapaswa kushirikishwa katika maamuzi kuhusu kile kinachohitajika kufanywa. Kila mtu anapaswa kufanya kazi pamoja ili kufikia malengo ya pamoja.
Ushirikiano ni wazo zuri. Wafanyakazi wanapaswa kushirikiana na kila mmoja ili kuboresha kampuni. Hii ni hatua muhimu sana kuelekea kuboresha kampuni.
Faida za kuwa na ushirikiano;
Moja; Utatuzi wa matatizo katika njia mbalimbali. Hapa kila mmoja anashirikisha ujuzi na uelewa kuhusu tatizo husika. Rejea msemo wa, “Kidole kimoja hakivunji chawa.
Mbili; Inaondoa presha na kuongeza kujiamini.
Hii ni kwa sababu unakuwa na watu wa karibu wa kushirikisha mkwamo wako. Hasa pale unapokutana na mapingamizi ya mteja.
Tatu; Kujifunza.
Unaposikiliza maelekezo au simulizi za watu wako wa karibu unajifunza na kujiboresha. Mfano, suala la uwasilishaji.
Nne; Hamasa.
Wakati mwingine unaweza kuona mambo yako hayaendi lakini akiona mwingine anafanikisha jambo fulani ni rahisi kuhamasika na kuchukua hatua.
Tano; Kuongezeka kwa ufanisi.
Kila mtu anapokuwa anafanya kazi kwa ushirikiano, kila kitu hukamilika kwa haraka na ufanisi zaidi.
Sita; Uhirikiano huokoa muda pia, kwa sababu wafanyakazi na wasimamizi hawahitaji kutenga muda wa kusuluhisha migogoro, pia umoja wa wafanya kazi hawa kufanya kazi zifanyike kwa kiwango cha juu sana.
Shirikiana na wafanyakazi wenzako mfikie malengo husika. Biashara ikifikia malengo yake basi na wewe unafikia malengo yako.
Je, unashirikiana na wengine kukuza mauzo yako? Fanyia kazi yote uliyojifunza katika somo hili.
Imeandaliwa na Lackius Robert Mkufunzi Msaidizi Chuo Cha Mauzo. Tuwasiliane 0767702659 au mkufunzi@mauzo.tz