Habari njema muuzaji bora kabisa kuwahi kutokea,
Karibu sana kwenye mwendelezo wa makala zetu za ukamilishaji ambazo ni mwendelezo wa makala kutoka CHUO CHA MAUZO.
Hongera sana kwa kuendelea kujifunza na kuchukua hatua kwa haya unayoendelea kujifunza hapa.
Leo ni jumatano ya ukamilishaji tukiongozwa na kauli mbiu inayosema ABC ALWAYS BE CLOSING-MARA ZOTE KUWA UNAKAMILISHA WATEJA.
Kama kauli mbiu inavyosema, mara zote unapaswa kukamilisha wateja na wewe pia unapaswa kukamilisha wateja. Na kukamilisha ndiyo wajibu wako namba moja kwenye biashara yako.
Wajibu wako namba moja ni kuuza na unapokuwa umemuuzia mteja maana yake umemkamilisha.
Hivyo basi, kila wakati wageuze wateja tarajiwa uliokuwa nao na waweze kununua na kuwa wateja kamili.

Ukamilishaji ndiyo kitu muhimu sana kwenye mauzo kwa sababu ndiyo kitu pekee kinacholeta fedha kwenye biashara kupitia kile unachouza iwe ni bidhaa au huduma.
Kwenye somo letu lililopita tulijifunza mbinu mbili za uhakika za ukamilishaji wa mauzo nayo ni mbinu namba 29 na 30.
Kwenye mbinu namba 29 tulijifunza ukamilishaji wa bajeti namba moja.
Na kwenye ukamilishaji wa namba 30 tulijifunza ukamilishaji wa bajeti namba mbili.
SOMA; Mbinu Mbili Za Uhakika Za Ukamilishaji Wa Mauzo 29-30
Kama ulienda kuzifanyia kazi na kupata matokeo basi karibu sana utushirikishe namna ulivyonufaika nazo mbinu hizo.
Leo kwenye ukamilishaji tukiongozwa na kauli mbiu yetu inayosema ABC ALWAYS BE CLOSING-MARA ZOTE KUWA UNAKAMILISHA WATEJA, tunakwenda kujifunza mbinu nyingine mbili za uhakika za ukamilishaji wa mauzo nazo ni mbinu namba 31 na 32
Zifuatazo ni mbinu mbili za uhakika za ukamilishaji wa mauzo ambazo tunakwenda kujifunza hapa;
31.Ukamilishaji wa bajeti – 3.
Mteja anakuambia yuko juu ya bajeti, wewe mwambie; “Naelewa na nategemea maamuzi haya hayatakuwa pekee kwako, yatakuwa na wenza nyumbani.”
(Mteja anauliza; “Unamaanisha nini?”) Unamjibu; “Hii haitakuwa ndiyo mara ya kwanza kwako kununua kitu ambacho ni zaidi ya bajeti. Nahitaji tukamilishe hili, au nahitaji ulipie sasa”
Mteja atacheka sana kwa hili, kwa sababu ni ukweli na ukweli una nguvu. Watu huwa tayari kulipa ziada kwa vitu wanavyovitaka.
Mwambie mteja kwamba usijizuie kupata kitu kizuri kwa sababu uko juu ya bajeti.
Tukamilishe mauzo.
32. Ukamilishaji wa bajeti – 4.
Mteja anakuambia yuko juu ya bajeti, unamwambia;
“Kama unaweza kumudu kulipia kodi, umeme, ada, wasaidizi, mavazi na mahitaji mengine muhimu, utaweza kulipia na hiki pia. Si ndiyo?
Vizuri, tukamilishe mauzo, tukamilishe hili. Lipia ili uende ukafurahie uwekezaji wako mzuri uliofanya.
Orodhesha vitu vyote wanavyoweza kuwa wanalipia kwa sasa na waonyeshe kama wanaweza kuvilipia wanaweza pia kulipia unachowauzia.
Hatua ya kuchukua leo; pale wateja wanapokupa mapingamizi mbalimbali kuhusu bajeti,nenda kazitumie mbinu hizi mbili za uhakika za ukamilishaji wa mauzo.
Kutoka kwa muuzaji mwenzako, rafiki anayekupenda na kukujali,
Mwl.Deogratius Kessy
Mwalimu/Mwandishi/Mkufunzi wa mauzo.
Makamu Mkuu wa CHUO CHA MAUZO.
makamu@mauzo.tz, 📞0717101505