‎Kakaa/Dadaa Yangu…‎‎

Umesahau wewe ni nani.‎‎

Umesahau kuwa ndani yako kuna nguvu ya kutikisa dunia.

‎‎Umejikatia tamaa kimya kimya.‎‎

Kila siku unasema labda mimi sina bahati.

‎‎Umeanza kuamini maisha ni magumu na huwezi kubadilisha chochote.‎‎

Lakini ukweli ni huu: UNA NGUVU YA MIUJIZA NDANI YAKO.

‎‎Unaitumia vibaya.‎Au hujui hata ipo.‎‎

Ulishawahi kumuona mtu aliyeanzisha biashara kwa buku 5 akafika juu?‎‎

Ulishawahi kumuona mtu aliyefeli shule lakini leo anaajiri waliopata division one?‎‎

Ulishawahi kumuona mtu aliyetelekezwa, akasota, lakini leo anajenga nyumba yake?‎‎

Wote hawa hawakuwa na miujiza ya mbinguni.‎‎

Walitumia nguvu ya ndani waliyoamka nayo kila siku.

‎‎Na hiyo nguvu wewe pia unayo.‎‎Lakini… unaitumia kuskroll TikTok.‎‎

Unaitumia kulalamika.‎‎

Unaitumia kutafuta huruma badala ya suluhisho.‎‎

Una nguvu lakini hauna mwelekeo.

‎‎Miujiza sio kupasuliwa mbingu.‎

Sio malaika kushuka.‎‎

Miujiza ni pale mtu wa kawaida anapoamua kuamka na kuchukua hatua isiyo ya kawaida.‎‎

Ni pale mtu anapoamua kuamka kabla ya wengine.

‎Kuanza kuandika ndoto zake.

‎‎Kuanza kusoma vitabu badala ya magazeti ya udaku.‎

Kuanza kuomba kazi kwa bidii badala ya kuomba msaada.

‎Miujiza ni matokeo ya msimamo.‎‎

Suluhisho Lipo.

Na Lipo Ndani Yako.‎‎

Badilisha namna unavyofikiri.‎

Acha kusema “sina mtaji” sema “naanza na hiki kidogo.

”‎‎Acha kusema “nimechelewa”  sema “leo ndiyo siku yangu ya kwanza.

”‎‎Acha kujificha nyuma ya visingizio.

‎Toka uvunguni.‎

Toka kwenye comfort zone ya umaskini wa mawazo.‎‎

Chukua hatua.‎

Anza leo.‎

Fanya kitu.‎‎

Kwa sababu NGUVU YA MIUJIZA UMEIBEBEA WEWE MWENYEWE.

‎‎Bado namkumbuka….‎‎

Kuna bro mmoja alichoka maisha.‎

Alikuwa hana kazi.

Hana mtaji.

Hana cheti.‎‎

Alikaa chini akaandika: “Mwaka huu lazima niwe mtu mwingine.

”‎‎Akaanza kuuza karanga mtaani.‎‎

Akaweka akiba ya mia mia.‎‎

Alikuwa anasoma vitabu alivyokopeshwa.‎‎

Alifungua YouTube kujifunza marketing.‎

Miaka mitatu baadaye…‎‎

Ana biashara ya kuuza nafaka.

‎Ana familia. ‎

Ana ndoto mpya kila mwaka.‎‎

Aliniambia hivi:‎‎“Miujiza haikunitokea, niliitengeneza mwenyewe.

”‎‎Sasa Wewe Una Sababu Gani Ya Kukata Tamaa?‎‎

Huna sababu.‎‎

Una kila sababu ya kusimama.

‎‎Chukua kalamu na kuandika ndoto zako.‎‎

Zima data saa tatu usiku na ipange kesho yako.‎‎

Na anza kutenda miujiza ya kweli kupitia nguvu yako ya ndani.‎‎

Kumbuka: Miujiza Haiporomoki.‎‎

Miujiza hutengenezwa.

‎‎Na hutengenezwa na watu kama wewe.‎‎

Watu wa kawaida lakini walioamua kuishi maisha ya ajabu.

‎‎‎Anyway, kama bado hujakisoma kitabu Cha UNA NGUVU YA KUTENDA MIUJIZA‎‎.

Basi weka oda yako hapa 👇

‎‎https://wa.link/q2m2dv

‎‎Kwasababu Vimebaki Vichache.‎‎

Nb. Hii ni leo tu, ukichukua hardcopy unazawadiwa na kitabu cha Jinsi Ya Kupata Chochote.

Unachotaka.‎‎

Karibu.‎

0756694090.‎

Imeandikwa Na Mkufunzi Ramadhan‎‎