‎Kakaa/Dadaa Yangu…
‎
‎Kuna uongo mmoja hatari sana unaoenezwa Kwenye jamii zetu…
‎
‎Watu wanaambiwa mafanikio ni siku moja kubwa.

‎Siku moja utajikuta na gari.
‎
‎Siku moja utakuwa na pesa za kukutosha.
‎
‎Siku moja utahama mtaa.
‎
‎Siku moja…
‎
‎Siku moja…
‎
‎Siku hiyo haiji bwana.
‎
‎Mafanikio si sherehe ya ghafla.
‎
‎Ni safari ya kila siku bila makelele.
‎
‎Wewe unasema unataka kufanikiwa, sawa…
‎
‎Lakini unalala hadi saa nne asubuhi.
‎
‎Simu ndiyo bibi yako.
‎
‎Series zimekuwa chakula cha akili yako.
‎
‎Maisha yako yanaenda kwa “autopilot”.
‎Upo tu.
‎
‎Ukisubiri muujiza.
‎
‎Bro, Sister, hakuna muujiza bila jasho.
‎
‎Hii dunia haitoi zawadi kwa wavivu.
‎
‎Ina wanyonya.
‎
‎Na inawatupa bila huruma.
‎
‎Sikiliza vizuri…
‎
‎Mafanikio ni mazoea madogo unayorudia kila siku.
‎
‎Ni kuamka mapema, hata kama hupendi.
‎
‎Ni kusoma ukurasa mmoja, hata kama huna mood.
‎
‎Ni kupanga siku yako kabla haijaanza.
‎
‎Ni kukataa vishawishi vidogo  kwa ndoto kubwa.
‎
‎Wale wanaosema “take it easy, usijibane sana”
‎
‎Ndiyo wale wale watakucheka ukifeli.
‎
‎Wakupe pole usiku, mchana wakutangaze.
‎
‎Usikubali!
‎
‎Hata kama ni kwa dakika 15.
‎
‎Soma, tafakari, panga.
‎
‎Jifunze kitu kipya.
‎
‎Andika ndoto zako.
‎
‎Jikumbushe sababu zako.
‎
‎Chapa kazi hata kama haionekani leo.
‎
‎Hiyo ndiyo siri.
‎
‎Mafanikio hujificha ndani ya maumivu ya kila siku.
‎
‎Na mwishowe hutokeza kwa kishindo.
‎
‎Mimi ni shahidi.
‎
‎Nilianza kuandika bila jina.
‎
‎Nilikuwa naandika status zinasomwa na watu wawili.
‎
‎Nilikaa hadi usiku nikiandika makala kama hii bila malipo.
‎
‎Wakati wengine wanalala, mimi nilikuwa naota nikiwa macho.
‎
‎Leo hii…
‎Watu wananitafuta.
‎Wananilipa.
‎Wananiamini.
‎
‎Lakini yote yalianza na ile siku niliyoamua kuamka mapema.
‎
‎Siku niliyoamua… kila siku ni nafasi ya kufika mbali.
‎
‎Na sitaki nisikie mtu anasema, “wewe ni bahati.”
‎
‎Hapana.
‎
‎Ilichongwa kwa jasho la kila siku.
‎
‎Mafanikio ni kila siku.
‎
‎Sio mwendo wa kusprint.
‎
‎Ni marathon ya moyo, bidii, na nidhamu.
‎
‎Usijilinganishe.
‎
‎Jilinganishe na wewe wa jana.
‎
‎Na hakikisha kesho, unamshinda huyo wa leo.
‎
‎Leo umeamka sasa swali ni moja tu:
‎
‎Utafanya nini?
‎
‎Anyway,
‎
‎Kama bado hujajiunga na wenzake makini kwenye huduma za ukocha, bonyeza hapa 👇 na utapewa utaratibu wa kujiunga.
‎
‎https://wa.link/i2r67s
‎
‎Karibu.
‎0756694090.
‎Imeandikwa Na Mkufunzi Ramadhan Amir.
‎
‎