‎Kakaa/Dadaa Yangu….
‎
‎Unapambana, eeh?
‎Unajituma.
‎Lakini bado hauoni matokeo?
‎
‎Kuna wakati unajiuliza:
‎
‎Hivi shida iko wapi?
‎Unaamka mapema, unajitahidi, lakini mwisho wa mwezi bado unakopa.
‎
‎Unalipwa mshahara.
‎Lakini baada ya siku tatu tu, unakuwa huna hata mia.
‎Kama mtu aliyekula mshahara kwa ndoto.
‎
‎Unajituma kama punda…
‎Lakini kipato chako ni kama tone la maji baharini.
‎Linatoweka kabla hujalitumia.
‎
‎Inakera, sio?
‎
‎Sasa ngoja nikuambie ukweli mchungu.
‎Tatizo sio kazi yako.
‎Tatizo sio kwamba huna mtaji.
‎Na wala sio kwamba huna bahati…
‎
‎Tatizo ni kwamba HUJUI KUUZA!
‎
‎Ndio hiyo!
‎Hujui kuuza ndoto zako.
‎Hujui kuuza bidhaa zako.
‎Hujui hata kujiuza wewe mwenyewe kama mtu wa thamani.
‎
‎Ukiwa hujui kuuza, utabaki kuwa mtumwa wa mishahara.
‎Na mishahara huwa haikutoshi huwa inakupiga marufuku na ndoto zako kubwa.
‎
‎Sasa ngoja nikushtue tena…
‎
‎Uuzaji sio kubeba bidhaa na kuzunguka mtaani.
‎Hapana!
‎Uuzaji ni kutumia mdomo wako vizuri.
‎
‎Ni kutumia simu yako vizuri.
‎Ni kuandika sentensi moja tu ambayo inamfanya mtu aseme:
‎”Nataka hii kitu sasa hivi!”
‎
‎Kama hujui kuuza, ni sawa na mtu asiyejua kuogelea kwenye bahari ya pesa.
‎Utazama tu.
‎
‎Lakini kama ukijifunza kuuza…
‎Weeh! Maisha yanabadilika chap chap.
‎
‎Sasa sikiliza hii stori ya ukweli…
‎
‎Kuna binti mmoja, anayeitwa Mishi.
‎Alikuwa anauza viatu vya mitumba.
‎
‎Kibanda chake kilikuwa kona ya soko, watu walikuwa hawapiti sana.
‎Alikuwa analala na stock.
‎
‎Siku moja akajifunza namna ya kuuza kupitia WhatsApp.
‎Akajua namna ya kuandika status tamu zinazochangamsha.
‎Akaanza kujua maneno ya kugusa hisia.
‎
‎Leo hii, Mishi ana group tatu za WhatsApp za wateja.
‎Kila anachopost kinanunuliwa.
‎
‎Na ajabu, stock inaisha hata kabla hajafungua duka.
‎
‎Aliniambia hivi:
‎
‎Siku hizi siuzi viatu, nauza hisia za watu kutamani viatu vyangu!
‎
‎
‎Na wewe unaweza.
‎Ndiyo, wewe!
‎Huna haja ya kusubiri mwaka.
‎Kwanza anza kwa kujifunza kuuza.
‎
‎Jifunze kutumia maneno kama silaha.
‎Jifunze kuandika sentensi za kuuza bidhaa, huduma, hata ndoto zako.
‎
‎Kama hujui kuuza utaendelea kuwa mtazamaji wa maisha ya wengine.
‎Ukiwa na simu ya laki mbili mkononi, lakini haina maana.
‎
‎Ukiwa na akili ya darasani, lakini haina matumizi.
‎
‎Na hiyo ni hatari kuliko ugonjwa wa ukoma.
‎
‎
‎Sasa swali ni moja tu…
‎Unataka kuendelea kubaki hapo ulipo?
‎
‎Au uko tayari kujifunza ujuzi wa pesa,
‎Ujuzi wa kuuza.
‎Ujuzi wa kuongeza kipato?
‎
‎Kama jibu ni ndiyo…
‎
‎Karibu kwenye dunia ya wauzaji wakali wanaotokea mitaani.
‎Wanaouza bila duka.
‎
‎Wanaopiga hela bila mtaji mkubwa.
‎Wanaouza kwa status, caption, voice note moja tu.
‎
‎Karibu kwenye ligi ya watu wanaotengeneza pesa kwa kutumia maneno.
‎
‎Kama Unataka Kuongeza Kipato Chako, Basi Bonyeza Hapa 👇
‎
*‎https://wa.link/cc2rgj*
‎
‎Karibu.
‎0756694090.
‎Imeandikwa Na Mkufunzi Ramadhan Amir.
‎