‎Kakaa/Dadaa Yangu…
‎
‎Wengi Wanashindwa.
‎Watu wengi wanatamani sana kuwa na biashara zao.
‎
‎Wanachoka kuamka asubuhi kwenda kazini kwa mtu.
‎Wanakasirika kuona pesa zao zikilipia ndoto za wengine.
‎
‎Lakini kila wakitaka kuanzisha biashara, akili inagoma.
‎
‎Nakujiambia…
‎
‎“Mwanangu biashara inahitaji mtaji mkubwa…”
‎
‎“Aaah, siku hizi biashara ni ngumu bana…”
‎“Bora nikatae tu, nisijiumize moyo…”
‎
‎Unasikia hizo sauti?
‎
‎Zinaonekana kama ushauri, lakini ni mtego.
‎Mtego wa ubaki pale pale.
‎Ukiwa na ndoto kubwa, lakini ukiishi maisha madogo.
‎
‎Inaumiza sana,
‎
‎Kwa sababu kila siku inaisha bila kupiga hatua yoyote.
‎Unaamka. Una scroll Instagram.
‎
‎Unamuona jamaa yako wa zamani anaendesha gari mpya.
‎Anaposti “Nashukuru Mungu kwa neema.”
‎
‎Unamjua vizuri kwamba hana hata degree.
‎Hakusoma sana kama wewe.
‎
‎Lakini ana biashara. Ana uhuru. Anaishi maisha ya ndoto zake.
‎
‎Wewe bado upo hapo unajiambia, “Siku moja nitaanza.”
‎
‎Siku moja haiji. Mwaka unaisha. Maisha yanasonga.
‎
‎Unakuwa mtaalamu wa kupanga, sio wa kuchukua hatua.
‎
‎Na hapa ndipo watu wengi wanakosea.
‎Wanasubiri hali iwe sawa.
‎Wanasubiri mtaji wa milioni.
‎Wanasubiri mtu awashike mkono.
‎
‎Hebu Nikuambie Ukweli,
‎Na Tuivunje Ile Imani Potofu.
‎
‎Biashara haianzi na pesa.
‎Biashara haianzi na duka kubwa.
‎Biashara haianzi na mkopo wa benki.
‎
‎Biashara inaanza na wazo + ujasiri + hatua ndogo.
‎
‎Kama huwezi kuuza kitu cha buku, huwezi kuuza kitu cha elfu 10.
‎
‎Kama huwezi kupata mteja mmoja, huwezi kupata mia.
‎
‎Watu wanalala wakisubiri kuamka na mtaji.
‎Lakini hawajui hata namna ya kuuza idea zao.
‎
‎Unataka biashara yako ikue?
‎
‎Acha kufikiria sana. Anza kufanya.
‎
‎Acha kutafuta approval ya watu.
‎Anza kutafuta mteja wako wa kwanza.
‎
‎Sasa Sikiliza Nikuambie….
‎
‎Na Hizi Hapa Ndizo Mbinu Zenyewe.
‎
‎(a) Anza na kitu unachokielewa au unachokipenda.
‎
‎Usianze kwa kufuata pesa. Anza kwa kufuata suluhisho unaloweza kutoa.
‎
‎(b) Fanya utafiti.
‎Tafuta watu wenye shida hiyo.
‎Angalia wanahangaika na nini.
‎Uwauzie suluhisho.
‎
‎(c) Tengeneza kitu cha bei rahisi.
‎Toa sample. Toa ladha ya huduma yako.
‎Watu waone thamani kabla hawajatoa hela.
‎
‎(d) Tengeneza jina.
‎Tumia WhatsApp, status, Facebook, IG.
‎Simama kama mtu anayeaminika.
‎
‎(e) Kua pole pole.
‎Kama leo unapata mteja mmoja, kesho wawili.
‎Boresha. Rudia. Panua.
‎Hapo ndipo biashara inapanuka.
‎
‎Bado namkumbuka….
‎
‎Dada Yangu Mary Alinifunza Mengi.
‎
‎Mary alikuwa anauza maandazi kwa shilingi 100.
‎Watu walimcheka. Walisema, “Hii si biashara.”
‎
‎Lakini alikuwa na kitu kimoja consistency.
‎
‎Alikuwa analeta kwa wakati.
‎Anacheka na wateja.
‎
‎Anatoa bonus kwa mteja wa tatu.
‎Miezi mitatu baadaye, alipata mteja wa catering.
‎
‎Akapika kwenye harusi.
‎Akapata hela ya kuongeza mtaji.
‎
‎Sasa ana duka la vyakula.
‎Ana wafanyakazi wawili.
‎
‎Wale waliomcheka, sasa wanamuuliza anatoa kazi lini.
‎
‎Biashara yake ilianza na mafuta ya buku tano na unga wa kilo moja.
‎Lakini aliweka moyo.
‎Aliweka ubunifu.
‎Aliweka tabasamu.
‎
‎Sasa Ni Zamu Yako
‎Acha kuogopa.
‎Acha kungoja hali iwe “shwari.”
‎
‎Anza na ulicho nacho.
‎Fanya vizuri kuliko wote.
‎Fanya kwa moyo.
‎Fanya kila siku.
‎
‎Kumbuka Hii:
‎Biashara si ya matajiri.
‎Biashara ni ya wale waliochoka kusubiri.
‎
‎Na kitabu kilichomfungua Dadaa Mary ni kitabu Kinachoitwa ELIMU YA MSINGI YA BIASHARA.
‎
‎Kama unacho hongera na rudia kuisoma sura ya kwanza.
‎
‎Lakini kama bado hujakipata bonyeza hapa 👇
‎
‎https://wa.link/gr5iim
‎
‎Karibu.
‎0756694090.
‎Hii Makala Imeandikwa Na Mkufunzi Ramadhan Amir.
‎