Rafiki Yangu Mpendwa,

‎Watoto wa siku hizi wanajua kutumia pesa.
‎Lakini hawajui kuitunza.
‎Kila pesa wanaipata, wananunua pipi, vinywaji, data, na michezo.

‎Lakini nani amewafundisha?
‎Nani kawapa misingi ya kuweka akiba?
‎Kuwaza uwekezaji?
‎Au hata kujua maana ya kuvumilia hadi malengo yatimie?

‎Hakuna.
‎Na hapo ndo tunaharibu kizazi.
‎Tunaandaa watoto wa kulalamikia umasikini baadae.

‎Kama mtoto wako hawezi kutunza shilingi mia tano…
‎Ataweza vipi kuendesha biashara ya milioni kumi kesho?

‎Kama hajui kutofautisha matumizi ya lazima na ya tamaa…
‎Atawezaje kuishi maisha yenye mipango?

‎Unampeleka shule.
‎Anapata “A”.
‎Lakini hawezi kumiliki akiba ya elfu tano.
‎Unajenga kisima bila maji.

‎Na siku utakapofariki ukimwachia mali…
‎Ataimaliza kabla hata hujazikwa vizuri.

‎Watu wengi hufikiri:
Watoto ni wadogo sana kufundishwa pesa.

‎Sawa.
‎Lakini watoto wa Kichina wanaanza kuuza vitu wakiwa darasa la pili.
‎Watoto wa Kizungu wanaanza kuandika bajeti wakiwa na miaka 8.
‎Wengine wananunua hisa, hata kabla hawajamaliza sekondari.

‎Na watoto wetu bado wanajifunza kutumia hela ya mzazi tu?

‎Tusifanye mzaha na maisha ya baadae ya watoto wetu.
‎Wale wanaosema mtoto ni mdogo
‎watawatazama watoto wao wakilia njaa miaka ijayo.

‎Sasa sikia hii…

‎“Semina Ya NGUVU YA BUKU TOTO”

‎Ni mafunzo spesho kwa watoto na familia.
‎Inafundisha watoto kutumia pesa kwa akili.
‎Kuweka akiba.
‎Kuwekeza.
‎Kujua thamani ya subira.
‎Kujifunza kusema “hapana” kwa tamaa.

‎Na wazazi pia wanapata elimu ya kuwalea watoto kipesa.
‎Ili mtoto awe na maarifa ya pesa kabla hata hajaanza kuingiza pesa.

‎Hii hapa story ya mtoto mmoja aitwaye Irene.
‎Miaka 10 tu.
‎Alishiriki kwenye semina yetu mwaka jana.
‎Tulimfundisha kuweka akiba ya buku moja kila siku.
‎Miezi mitatu tu baadaye, alikuwa amejikusanyia 90,000.

‎Tulimsaidia kununua mabox ya kuuza juisi shuleni.
‎Leo anauza juisi kila wiki kwa faida.
‎Anaakaunti ya benki.
‎Na anajua bajeti yake kila mwezi.

‎Mzazi wake anasema:

‎“Irene ni mtoto wa tofauti.
‎Hata mimi sasa najifunza kutoka kwake.”


‎Sasa jiulize…
‎Mtoto wako anajua nini kuhusu pesa?
‎Anajua kuitunza au kuitapanya?
‎Utakaa tu umtazame anaharibika au utamwekea msingi mapema?

‎Watoto wa leo ni mabilionea wa kesho…
‎Ila ni wale waliopandikiziwa mbegu sahihi sasa.

‎Usikose hii semina.
‎Ni zawadi bora kuliko toy, kuliko chipsi, kuliko outing.

‎Tuma neno “TOTO” kwemda 0756694090 ili ujisajili.
‎Au bofya hapa 👉 https://wa.link/qghfsv

‎Karibu.
‎Imetoka Kwa Rafiki Yako Anayekupenda Na Kukujali Sana,

‎Mkufunzi Ramadhan Amir