HAKUNA JIBU MOJA SAHIHI

  Shuleni tumefundishwa kuchagua jibu moja sahihi, unapewa swali na majibu mengi ila jibu moja tu ndio sahihi. Kwenye maisha ni tofauti kabisa, hakuna jibu mja sahihi, kuna majibu mengi sahihi na mengi ambayo sio sahihi. Hakuna njia moja ya kufanikiwa kwenye maisha, zipo njia nyingi sana, baadhi zitakupeleka pazuri ningine zitakupeleka pabaya.
  Usisumbuke kujaribu kuiga kila njia ambayo baadhi ya watu wamepita wakafanikiwa, wapo wengi na zipo nyingi. Na katika njia hizo hizo walizopita wakafanikiwa kuna wengine wamezipita wakashindwa. Tafuta njia inayokufaa wewe na itumie hiyo vizuri kufikia mafanikio yako. Huwezi kupita kila njia, lazima utafute njia moja inayokufaa wewe ndio uipite.

  Majibu ni mengi kwenye njia ya mafanikio na sio yote yanayokufaa wewe hata kama yamewatoa wengine. Usipoteze muda kufanya kitu ambacho hakikupatii majibu unayotarajia.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: