LENGO LA BIASHARA NI NINI?

  Watu wengi wanafanya biashara na watu wengi wanampango wa kuingia kwenye biashara ama ujasiriamali. Katika hao wengi wanaofanya biashara wachache wanafanikiwa na wengi wanashindwa na kuona labda biashara haiwafai wao. Kuna sababu nyingi za kwa nini watu wengi wanashindwa kufanikiwa kwenye biashara. Moja ya sababu hizo ni kutokujua lengo la biashara ni nini. Hebu nijibu lengo la biashara ni nini? Ni nini hasa kilichokusukuma ukafanye biashara ama utake kufanya biashara? Majibu ya wengi ni lengo la biashara ni kupata hela ama kutengeneza faida. Kama na wewe ndio jibu lako basi uko kwenye njia ya wanaoelekea kushindwa ama unashindwa. Lengo la biashara sio kupata hela ama kutengeneza faida, kuwaza tu hivyo tayari ni chanzo kikubwa cha kushindwa kwenye biashara.

  Lengo la biashara ni kutengeneza wateja, hakuna cha ziada. Ukishatengeneza wateja hivyo vingine kama hela na faida vitakuja vyenyewe kutoka kwa hao wateja. Nguvu yoyote unayoweka kwenye biashara yako hakikisha ni kutengeneza wateja, yaweza kuwa wateja wapya ama kuhakikisha wateja wanaendelea kununua kwako. Biashara yoyote inayokufa ni biashara iliyoshindwa kutengeneza wateja wapya ama kubakisha wateja wa zamani. Wateja ndio uhai wa biashara yoyote, hivyo kipaombele cha kwanza kwenye biashara lazima kiwe kumridhisha mteja. Kwa nini mteja anunue kwako na asinunue kwa mwingine? Hilo ndilo swali la msingi unalotakiwa kujiuliza ili kuweza kutengeneza wateja wapya ama kufanya wazamani wasiondoke na kwenda kununua kwa mwingine.

biashara wateja

  Kuna njia nyingi sana za kutengeneza wateja kwenye biashara, ila hapa nitazungumzia moja (njia nyingine nitazizungumzia siku nyingine). Njia mojawap ya kutengeneza wateja ni KUTENGENEZA THAMANI. Thamani ni kitu ambacho watu wanakitaka na wako tayari kukilipia ili kuwa nacho. Hakikisha bidhaa ama huduma unayouza ina thamani kwa mteja unaetaka kumuuzia. Hakikisha ni kitu ambacho watu wanakihitaji sana na wako tayari kutoa hela zao walizozipata kwa uchungu ili kupata thamani hiyo. Hakuna mtu ambae anapenda kupoteza hela hasa ambazo zimepatikana kwa kazi ngumu, hivyo hakikisha kuna sababu ya watu kushawishika kutoa hela zao.

  Kama utawaza biashara kama njia ya kutengeneza wateja basi itakuwa rahisi sana kukua na kuendelea. Kama ukiwaza kama kitu cha kukupatia faida itakufa haraka sana hasa pale faida itakapkuwa ngumu kupatikana. Badili mtizamo wako juu ya biashara ili uweze kufikia malengo yako.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: