KABLA HUJAFIKIRIA KUTENGENEZA PESA KWENYE MTANDAO SOMA HAPA

  Kwa siku za hivi karibuni kumekuwa na wimbi kubwa la fursa za kutengeneza fedha kwa kutumia mtandao(make money online). Kuna baadhi ya fursa za kutengeneza pesa kwenye mtandao ni za kweli na kuna baadhi ni sio za kweli.

moneyonline

  Kama tunavyojua linapokuja swala la fedha matapeli hawakosekani, vivyo hivyo hata kwenye fursa ya kutengeneza fedha kwenye mtandao kuna matapeli wengi sana.

  Kuna link nyingi zimekuwa zikiwekwa kwenye mitandao mbalimbali na watu kuwashawishi wenzao kujiunga na link hizo. Link hizo zinashawishi watu kuzibonyeza na pia kuwashirikisha marafiki zao na kila unapobonyeza unalipwa dola moja ya kimarekani($1). Kuna mitandao mingine imekwenda mbali zaidi na kusema wanatoa mpaka dola tatu($3) kwa kila unaemshirikisha na kubonyeza link. moneyonline2

  Kama mtandao unakwambia unalipwa dola moja ya kimarekani kila unapobonyeza link ama kumwalika rafiki inamaana ukiweza kuwaalika na kubonyeza link 50 kwa siku unapata dola 50 sawa na shilingi elfu 80 za kitanzania!! Yaani utengeneze 80,000/= tsh ukiwa umekaa tu mbele ya kompyuta yako?  Hela haijawahi kuwa rahisi kupatikana kiasi hiki!

  Niliwahi kujiunga na moja ya mitandao hii na nikafikisha mpaka dola 500 ila nilipotaka kupatiwa changu ndipo nilipanza kuzungushwa. Mara nipewe sijui mafumbo gani ya kufumbua mara niingizwe kwenye shindano la kushinda simu, na mara nyingine wanaleta lugha ata zisizoeleweka.

  Usidanganyike kwamba unaweza kupata fedha kirahisi hivyo, fedha inapatikana kwa kazi na sio kwa kubonyeza link za mitandao.

  Kama unataka kutengeneza fedha kwenye mtandao kuna njia kuu tatu

  Njia ya kwanza kuudha bidhaa ama huduma kwa njia ya mtandao. Kama unafanya biashara mtandao ni sehemu rahisi sana kupata wateja wa kitaifa na kimataifa.

Njia ya pili ni kutengeneza tovuti ama blog unayoweza kuitumia kuuza bidhaa zako ama za wengine na ukalipwa kutokana na matangazo ama huduma nyingine unazotoa.

 moneyonline3

Njia ya tatu na iliyo ya muhimu kwa wengi ni kupunguza muda unaoutumia kwenye mitandao. Kama hakuna fedha unayoingiza kwa njia hizo mbili basi ni bora upunguze muda unaotumia mitandao na kutumia muda huo kutengeneza fedha za kweli.(soma; jinsi ya kupunguza muda kwenye mitandao)

moneyonline4

  Tuitumie mitandao kwa faida. Usidanganyike kwamba unaweza kupata fedha kirahisi kwa kupitia mtandao. Fedha sio rahisi kiasi hiko kupatikana, lazima ufanye kazi ndipo upate fedha, ukiona tangazo la kupata fedha bila kufanya kazi usijaribu hata kulisogelea kwa sababu utaishia kupoteza muda wako wa dhamani.(soma; thamani ya muda wako)

 

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: