Karibu kwenye utaratibu wa kujisomea vitabu ambapo kila mwanachama wa mtandao huu anatumiwa kitabu cha kujisomea. Vitabu vinavyotumwa ni vitabu vya kuhamasisha, kutia moyo na pia kutoa mafunzo mbalimbali muhimu kwa ajili ya kufikia malengo tuliyojiwekea kwenye maisha.
  Leo kila mwanachama anatumiwa kitabu kinachoitwa
The Top 200 Secrets of Success and the Pillars of Self-Mastery
kilichoandikwa na Robin S. Sharma
  Kitabu hiki kimetoa mbinu mbalimbali ambazo unaweza kuzifanya kila siku na zikakusaidia kufikia malengo yako na kufanikiwa kwenye maisha.

200
  Kuna vitu vidogo vidogo ambavyo huwa tunavipuuza ila ni vya muhimu sana kwenye maisha yetu na kufikia mafanikio. Kitabu hiki sio kwamba kimebeba siri nzito wala mambo ambayo inabidi kutumia fedha au teknolojia. Mambo haya 200 kila mtu anaweza kuyafanya bila kujali umri wala kiwango cha elimu.
  Tafadhali tenga muda wa kusoma kijitabu hiki kidogo na uanze kutekeleza yale yaliyoandikwa humo mara moja.

  Tofauti kubwa kati ya watu waliofanikiwa na ambao hawajafanikiwa sio umri, elimu, akili ama utofauti mwingine wowote isipokuwa jinsi wanavyofikiri na wanavyofanya mambo yao.

  Jifunze njia 200 za kufanya mambo kwa utofauti na ujihakikishie kufanikiwe kwenye jambo lolote unalofanya.
  Kwa wale wavivu wa kusoma, huna sababu yoyote ya kutosoma kitabu hiki kwa sababu kwanza ni kidogo sana(kurasa 26) na njia hizo 200 zimewekwa kwa namba hivyo unaweza kuchagua kusoma njia kumi kila siku na kuwa umemaliza njia hizo 200 ndani ya wiki mbili.
  Nakusihi tena soma kitabu hiki na uanze kushika usukani wa maisha yako.
  Bonyeza hayo maandishi hapo chini yenye jina la kitabu kukidownload.
The Top 200 Secrets of Success and the Pillars of Self-Mastery
By Robin S. Sharma

  Asante kwa kuendelea kuwa mwanachama wa mtandao huu na tafadhali waalike marafiki zako wajiunge na mtandao huu ili nao wapate mambo haya mazuri.

  Kama bado hujajiunga na mtandao huu jiunge sasa kwa kubonyeza maandishi haya na uweke email yako.
  Kama unajambo lolote la kuhitaji ushauri ama unataka kutushirikisha usisite kuniambia kwa kutumia mawasiliano haya yanayopatikana kwenye blog hii.
 

  ENDELEA KUTEMBELEA BLOG YAKO AMKA MTANZANIA UENDELEE KUJIFUNZA NA KUHAMASIKA.