FACEBOOK; Biashara Iliyovunja Rekodi Nyingi Kushinda Biashara Yoyote.

  Tarehe 04/02/2014 Facebook imetimiza miaka kumi tokea ilipoanzishwa tarehe 04/02/2004. Katika miaka kumi ambapo facebook imekuwepo imevunja  rekodi nyingi sana za biashara kuliko biashara yoyote iliyowahi kutokea duniani.

  Mpaka sasa inapotimiza miaka kumi facebook ina watumiaji zaidi ya bilioni 1.23 kutoka duniani kote. Na karibu kila nchi duniani kuna watu wanaotumia facebook. Hii inamaanisha kwamba karibu robo ya watu wote duniani wanatumia facebook. Hii ni bidhaa na huduma pekee duniani ambayo imekuwa na watumiaji wengi sana.

              facebook

  Facebook ni kampuni yenye mafanikio sana duniani ambayo inaendeshwa na kijana mwenye umri mdogo kuliko waendeshaji wengine wa makampuni makubwa. Mpaka sasa mwanzilishi na mwendeshaji wa facebook Mark Zuckerberg ana miaka 29. Alianzisha Facebook akiwa na miaka 19 na imekuwa kampuni yenye mafanikio makubwa sana. Mark Zuckerbeg anasemekana ni moja ya watu wenye ushawishi mkubwa sana duniani na anatajwa kama myahudi mwenye ushawishi mkubwa kuliko wote. Mpaka kufikia septemba 2013 Zuckerberg alikuwa na utajiri unaofikia dola za kimarekani bilioni 19(zaidi ya trilioni 30 za kitanzania) sehemu kubwa ya mapato yake ikiwa facebook.

  Mpaka kufikia sasa inasemekana Facebook ina utajiri mkubwa kushinda makampuni haya makubwa ambayo yamekuwepo kwenye biashara muda mrefu sana kushinda facebook.

1. Hewlett-Packard(HP), kampuni kubwa ya kutengeneza kompyuta.

2. Dell, kampuni ya kutengeneza kompyuta. Facebook ina utajiri mara nne ya Dell.

3. The New York Times, shirika kubwa la uchapishaji wa majarida, vitabu na habari za kwenye mtandao.

4. Disney, kampuni kubwa ya burudani yenye miaka zaidi ya 90.

5. Nokia, facebook ilikuwa inaizidi kampuni ya simu ya nokia mara kumi kwa utajiri. Kwa sasa kampuni hiyo imeuzwa kwa kampuni ya microsoft.

  Facebook imekuwa na manufaa makubwa sana kwa dunia nzima. Facebook imerahisisha mawasiliano ambapo kwa sasa kuwasiliana na mtu yeyote alieko nchi yoyote duniani imekuwa rahisi sana na kwa gharama ndogo sana.

  Facebook imekuwa na mchango mkubwa sana kwenye siasa ambapo makundi mbalimbali ya kisiasa yametengenezwa na facebook imetumika kama sehemu ya kutoa taarifa na kupata wafuasi wapya.

  Facebook imesaidia harakati mbalimbali. Maandamano makubwa yaliyotokea kwenye nchi za kiarabu kati ya mwaka 2010 mpaka 2013 facebook ilitumiaka kama njia ya kuhamasishana na kupeana taarifa.

  Makampuni yote duniani kwa sasa yanatumia facebook kama njia ya kutangaza biashara zao na hata kuwa karibu na wateja wao. Kila kampuni hata hapa Tanzania ina ukurasa wa facebook ambapo inautumia kutoa taarifa mbalimbali na hata ofa.

  Facebook pia imeweza kukutanisha watu na kutengneza marafiki wapya. Inasemekana mtu mmoja anaweza kuwa na marafiki kwenye nchi 12 tofauti duniani kwa kupitia facebook. Pia kuna walioanzisha urafiki, uchumba na mpaka kufikia ndoa kwa kuanzia facebook. 

  Pamoja na rekodi hizo nyingi zilizowekwa na Facebook mpaka sasa, mwanzilishi na mwendeshaji wake bado hajatosheka ama kuridhika. Malengo yake ni kwamba miaka kumi ijayo kila mtu duniani awe anatumia facebook. Na kuna dalili nzuri kwamba malengo hayo yatafikiwa kwa sababu biashara yebye watumiaji bilioni 1.23 haiwezi kufa mara moja.

  Wakati anaanzisha facebook Zuckerberg hakuwahi kudhani kama ingekuja kuwa kampuni kubwa sana duniani. Hakuanzisha Facebook kwa njaa ya hela bali alikuwa anafanya kitu anachokipenda na alilenga kubadili maisha ya watu. Katika mahojiano yake na mwandishi David Kirkpatrick zuckerberg alisema hakuwahi kupanga kuja kuendesha kampuni. Ila kwa sasa anafanya mambo makubwa ambayo dunia nzima inanufaika.

  Tunajifunza nini sisi watanzania kutokana na mafanikio haya ya Facebook?

  Ni kitu gani tunaweza kufanya hapa Tanzania na kikawa na manufaa makubwa kwa dunia nzima?

  Tushirikishane kwenye maoni hapo chini.

3 thoughts on “FACEBOOK; Biashara Iliyovunja Rekodi Nyingi Kushinda Biashara Yoyote.

  1. Anonymous February 7, 2014 / 10:54 am

    Tuendelee kuumiza vichwa na kutoyaonea aibu mawazo yetu. Maana unaweza kuwa na wazo zuri na ukaona aibu au kuwa na hofu nakuona haliwezekani.

    Like

  2. Anonymous February 9, 2014 / 5:57 am

    unajua wahenga husema woga ni umaskin! weng wetu hatupend KUTHUBUTU.watu weng hapa nchn ni watalam wa hali ya juu lakn kwa vile hawana mahal pa kujaribia,mtu wa kuwaongoza, pia mfumo wa gvt wa vitisho watu hao wanaishia mitahan na fan zao. naomba tufunguke,tuuvae ujasir na tutoe kwa kushirikisha wenzetu yale tuliyonayo vichwan mwetu hakika tutabadilika

    Like

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s