Asante Kwa Mrejesho Wako Mzuri.

Ndugu msomaji wa AMKA MTANZANIA naomba nikupongeze kwa kutoa ushirikiano wa kutosha katika kuuboresha mtandao huu. Wiki iliyopita niliweka utafiti mfupi wa kutaka kupata picha ya wasomaji wa AMKA MTANZANIA. Watu wengi wamejibu maswali ya utafiti huo kuliko ambavyo nilitegemea.

  Hii inaonesha tuko pamoja katika safari na harakati hizi za kuboresha maisha yetu. Kupitia utafiti huu nimejua mambo mengi zaidi yanayowakwamisha wasomaji wa mtandao huu kufikia malengo waliyojiwekea.

  Natoa shukrani kwako uliyechukua muda wako kidogo na kujibu maswali ya utafiti huu. Naahidi kuandaa makala zinayoelezea suluhisho la kila tatizo linalomsumbua msomaji wa mtandao huu. Lengo ni kuweza kusaidiana ili mwisho wa siku kila mtu afikie malengo yake.

  Kama bado hujajibu maswali ya utafiti huu nakuomba uchukue dakika zako chache na ujubu maswali haya. Bonyeza maandishi haya ili kuweza kujibu maswali ya utafiti huu muhimu.

  Utafiti huu ni siri kwani hakuna sehemu yoyote utaweka jina lako, hivyo taarifa utakazotoa hakuna atakayejua ni za nani. Lengo kuu ni kujua matatizo na vikwazo mbalimbali vinavyowazuia watanzania kufikia malengo yako.

 kitabu kava tangazo

Wiki hii ndio mwisho wa utafiti huu kwani baada ya hapa utafiti utafungwa na hutaweza kutoa tena changamoto zako. Hivyo kama unahitaji msaada zaidi tafadhali jibu maswali haya.

Kumbuka kubonyeza maandishi haya na kujibu maswali ya utafiti kama bado hujafanya hivyo.

  Nakutakia kila la kheri, TUKO PAMOJA.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: