Mambo Mapya Na Mazuri Ndani Ya KISIMA CHA MAARIFA; Usikose.

Kupitia kisima cha maarifa sasa tutaanza kutoa mafunzo ya kubadili au kutengeneza tabia za mafanikio. Kwanzia mwezi wa tano kila mwezi tutakuwa tunaandika kuhusu tabia moja muhimu ya kukufikisha kwenye mafanikio. Kila siku ya jumanne ya kila wiki utapata makala moja kwenye kisima cha maarifa ikielezea umuhimu wa tabia tunayozungumzia na jinsi ya kuitengeneza kwako ili uweze kupata mafanikio makubwa.

Kwa nini tabia?

Ni ukweli usiopingika kwamba mafanikio kwa kiasi kikubwa yanatokana na tabia fulani ambazo watu wanazo. Wengi wa waliofanikiwa wana tabia hizo, na wewe kama hujafanikiwa ni kutokana na kutokuwa na tabia hizi au kuwa na tabia ambazo zinakurudisha nyuma,

Mafanikio hayaji kwa sababu ya kufanya kitu fulani ndani ya siku chache na ukapata majibu makubwa, bali mafanikio yanatokana na mambo madogo madogo unayofanya kila siku na baadae yanajikusanya na kuwa mengi na ndio yanakuwa mafanikio yako. Na hata kutofanikiwa nako kunakwenda hivyo hiyo, kuna vitu ambavyo unavifanya kila siku, unaweza usione madhara yake mara moja ila baadae vinakuwa kikwazo kikubwa kwako kufanikiwa.

Kitu chochote unachokifanya kwa kurudiarudia mwishowe unakuwa mtaalamu wa kitu hiko. Hivyo pia kwa tabia, kama utakuwa na tabia zinazokupeleka kwenye mafanikio na ukawa unazirudia kila siku ni lazima utafanikiwa.

Hii ndio sababu kubwa ya kuanza na kubadili au kutengeneza tabia za mafanikio.

kitabu kava tangazo

Tabia tutakazobadili miezi michache ijayo;

Kama upo tayari kwa ajili ya mafanikio kwenye maisha yako basi karibu uungane nasi katika safari hii ya kutengeneza tabia za mafanikio. Tabia tutakazobadili au kutengeneza miezi michache ya mwanzo ni;

1. Mwezi wa tano; Muda. Utunzaji wa muda, kupunguza muda unaopoteza na kupata muda wa ziada kila siku na kila wiki. Kama unavyojua kwamba muda ndio kila kitu, unaweza kupata mamilioni ya fedha baada ya kuyapoteza ila huwezi kupata sekunde moja uliyoipoteza. Asilimia 50 ya muda wetu tunaupoteza tu, hapa tutaona ni jinsi gani ya kutumia muda wetu vizuri ili kufikia mafanikio.

2. Mwezi wa sita; Kujisomea vitabu na kujifunza. Kujifunza kila siku na kila mara ni moja ya viungo muhimu sana kwenye mafanikio. Watu wengi hawajifunzi vitu vipya kwenye maisha yao kwa sababu ya uvivu wa kusoma. Hapa tutapeana mbinu ni jinsi gani unaweza kujisomea na kujifunza zaidi bila ya kutumia nguvu kubwa.

3. Mwezi wa saba; Kujijengea ujasiri na kujiamini. Hofu ni moja ya vitu vinavyorudisha watu wengi sana nyuma. Inawezekana ulishakutana na fursa mbalimbali ukaogopa kuchukua hatua ila baadae ukaja kujutia kutochukua hatua mapema. Hii inatokana na kukosa ujasiri, udhubutu na kujiamini. Ni vigumu sana kufanikiwa kwenye jambo lolote kama hujiamini. Hapa tutapeana mbinu mbalimbali za kujijengea ujasiri, udhubutu na kujiamini ili uweze kufikia mafanikio unayotarajia.

Ni muhimu sana kwako kujenga tabia hizi za ushindi ili uweze kufikia mafanikio unayotarajia. Uzuri ni kwamba jinsi ambavyo unarudia jambo mara kwa mara ndivyo linavyokuwa tabia.

Kama utafanya kitu cha kuboresha maisha yako kila siku baada ya muda itakuwa tabia. Ndio maana nimetenga mwezi mmoja kwa kila tabia tunayotaka kuitengeneza. Mwanzo wa kutengeneza tabia yoyote mpya ni mgumu sana ila baada ya muda inakuwa rahisi na baadae inakuwa kitu cha kawaida kwako.

Kama bado hujajiunga na kisima cha maarifa fanya hivyo mapema ili uweze kupata mafundisho haya muhimu. Sasa hivi utaratibu wa kujiunga na kisima unabadilika, badala ya kujiunga kwa siku yoyote unayotaka utaweza kujiunga siku tatu kabla ya mwezi kuanza ili tuweze kwenda vizuri kwenye mafunzo haya ya mwezi kwa mwezi.

Kujiunga na kisima cha maarifa tuma fedha tsh elfu kumi kwa mpesa au tigo pesa 0717396253/0755953887 na utume email yako kisha utaunganishwa. Ni vizuri ukawa na email ya GMAIL, ila kama huna unaweza kuniambia nikakutengenezea email na kukuunganisha. Kumbuka kutuma email pale unapotuma fedha maana wengi wanajisahau.(kwa maelezo zaidi kuhusu kisima cha maarifa bonyeza hapa)

Wahi kujiunga na kisima kabla ya jumatano tarehe 30/04/2014, ukichelewa hapo itabidi usubiri mpaka tarehe 31/05/2014.

Karibu sana katika safari hii ya kuboresha maisha yetu.

Kumbuka TUKO PAMOJA.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s