Mara nyingi katika safari yoyote ya mafanikio kukutana na changamoto ni kitu ambacho kinakuwa  hakikwepeki. Wengi wetu mara kwa mara tumekuwa tukikutana na changamoto za aina mbalimbali katika maisha yetu. Unapokutana na changamoto hizi usipokuwa makini na kuwa mtulivu unaweza  ukakata tamaa na kuamua kuachana na malengo yako makubwa uliyojiwekea.
Wengi wanapokutana na changamoto za namna hii katika maisha yao, huwa wanajiona hawafai, wamekosea na kuona maisha hayawezekani tena kwao, pasipo kujua wao ni watu muhimu sana na wa pekee katika hii Dunia ambao wanauwezo wa kufanya kitu chochote kile bila ya kuzuiliwa na mtu.
Inawezekana kabisa katika maisha yako umekutana na changamoto nyingi ambazo zimekufanya ukate tamaa, ukose tumaini na kujiona kama vile umekosea sana na umechelewa katika maisha kufikia ndoto zako ulizojiwekea. Kitu unachotakiwa kujua hakuna changamoto yoyote ambayo ina uwezo wa kukuzuia kufanikiwa, sema tu wewe hujaamua kukabiliana nayo.
Pengine inawezekana changamoto yako unaona huna mtaji, umri wako unafikiri umeenda na unaona huwezi kufanikiwa tena au una ulemavu wa aina Fulani unaokufanya uamini toka moyoni kuwa wewe huwezi kitu katika maisha. Ninachotaka kukwambia hayo yote si kitu una uwezo mkubwa wa kufanikiwa kwa hali yoyote uliyonayo.
Ukiamua kufanikiwa utafanikiwa tu, bila kujali changamoto ulizonazo wala sura ya maisha uliyonayo sasa ikoje. Kama unafikiri natania kwa dakika hizi chache ulizonazo angalia na ujifunze kitu kikubwa sana katika maisha yako kupitia watu hawa waliofanikiwa bila ya  kujali vizuizi na changamoto zilizokuwa zikiwakabili.
1. Stevie Wonder.
Kwa wale wasiomjua vizuri huyu ni moja kati ya wanamziki maarufu duniani ambaye alizaliwa akiwa na ulemavu wa macho. Kutokana na kutokuona kwake hakukumzuia asifanye kitu katika maisha yake, akiwa na umri wa miaka 11 tu alitoa rekodi yake ya kwanza ambayo ilifanya vizuri.
Kitu pekee tunachojifunza kwa Stevie Wonder ni kutojiona wanyonge,tumeshindwa pengine kutokana na udhaifu wetu. Vyovyote vile ulivyo hujakosea katika maisha yako upo sawa, unaweza kufanya lolote katika maisha yako.
 
Huyu ni mwanadada pekee Duniani ambaye alizaliwa hana mikono yote miwili lakini anauwezo wa kuendesha ndege, gari na kucheza piano ingawa vitu vyote hivyo anavifanya kwa kutumia miguu yake.
Jessica anatufundisha kuwa hakuna lisilowezekana chini ya jua kama utaamua kweli unataka kufanikiwa. Kama Jessica angekaa na kulaumu ulemavu wake asingeweza kuwa rubani. Sasa jiulize mwenyewe ni kitu gani kinachokuzuia kufanikiwa? Na nini hasa ulichokikosa?
3. Oscar Pistorius.
Unapozungumzia wanaridha maarufu Afrika ya kusini huwezi kukosa kumzungumzia kijana huyu Oscar. Ni mwanariadha ambaye hana miguu  pia, anatumia miguu ya bandia lakini ameonyesha uwezo na kipaji chake kuwa hakuna chochote kinachoweza kumzuia mwanadamu kufanikiwa zaidi yake yeye mwenyewe.
Pamoja na ulemavu wake wa miguu Oscar amejizolea medali nyingi ndani na nje ya Afrika kusini kutokana na mchezo wa mbio za miguu. Hii yote inatuonyesha na kutufundisha kuwa binadamu ana kila anachokihitaji kufikia malengo yake.
4. Elizabeth Jolley.
Katika maisha yake siku zote alikuwa na kipaji cha kuandika na alitamani sana katika ujana wake kuchapa vitabu vyake lakini alishindwa kutokana na kukosa pesa. Hilo halikumkatisha tamaa kuendelea kuandika aliamini ipo siku moja ndoto yake itatimia tu. Akiwa na umri wa miaka 56 kwa mara ya kwanza alifanikiwa kutoa “Novel”yake ya kwanza, baada ya muda alichapa vitabu vingine vingi zaidi. Elizabeth hakufikiri kama amechelewa aliwaza ndoto zake tu zitimie.
Kumbuka hakuna chochote kinachoweza kukuzuia kufanikiwa, huchalewa wala hujakosea kitu katika maisha yako, unauwezo wa kubadili maisha yako kwa jinsi unavyotaka yawe endapo tu utachukua hatua ya kuamua na kuachana na visingizio.
Nakutakia mafanikio mema, chukua hatua juu ya maisha yako na endelea kufatilia mtandao huu wa AMKA MTANZANIA kwa kujifunza zaidi.
DAIMA TUKO PAMOJA.

IMANI NGWANGWALU0767048035/ingwangwalu@gmail.com