Habari za leo mpenzi msomaji wa AMKA MTANZANIA, kama nilivyosema awali, wiki hii tulikuwa tunatoa memory card yenye vitabu muhimu vya kujiongezea ujuzi ili kuweza kuwa bora zaidi.

Kupitia memory card hii utapata vitabu ambavyo utajifunza vitu vitatu muhimu sana kwako wewe ili kuweza kufanikiwa. Vitu hivi ni muhimu iwe umeajiriwa, umejiajiri au unafanya biashara. Vitu hivyo ni;

1. Kujifunza jinsi ya kuuza(sales), kila mmoja wetu kuna kitu anauza, kama umeajiriwa unauza muda na utaalamu wako, kama unafanya biashara unauza huduma au bidhaa. Kwa vyovyote vile ni muhimu kujifunza jinsi ya kuuza ili uweze kufikia mafanikio makubwa.

2. Kujifunza mbinu za mawasiliano(communication skills). Jinsi unavyowasiliana na wengine kunaweza kukufanya uwe na nguvu kubwa au ukose nguvu kabisa. Ni muhimu sana wewe kujifunza mbinu nzuri za mawasiliano ili kuweza kuwa na ushawishi mkubwa.

3. Kujifunza jinsi ya kukubaliana(negotiation), kukwaruzana au kupishana ni kitu cha kawaida kwenye kazi, biashara na hata maisha kwa ujumla. Kama utakuwa na mbinu nzuri za kukubaliana unaweza kushawishi na mawazo yako kukubalika, kama huna mbinu hizo utakosa fursa nyingi sana.

Memory card hii ina vitabu 21(kupata maelezo zaidi na kujua vitabu vilivyopo bonyeza maandishi haya) na ina ukubwa wa 4GB. Gharama ya kadi hii ni tsh elfu 30.(30,000/=).

Kupata memory card hii tuma fedha tsh elfu 30 kwa mpesa 0755953887 au tigo pesa na airtel money kwenye 0717396253 na kisha utaandaliwa memory card na kupatiwa.

Kwa walioko mikoani utatumiwa kadi, na hivyo unaongeza tsh elfu 5 ya usafiri hivyo unatuma tsh elfu 35.

Leo ndio mwisho wa kupata memory card hii, chukua hatua sasa kabla siku ya leo haijaisha.

CHANGAMOTO YA KUSOMA VITABU MIA TANO(500)

Habari za leo rafiki? Naomba nikushirikishe changamoto mpya ninayokwenda nayo, kama utaiweza karibu.
Mpango uliopo sasa ni kusoma vitabu 500!!
Ndio vitabu mia tano na mpango huu ni wa miaka mitano.
Kila mwaka unasoma vitabu mia moja na kila wiki unasoma vitabu viwili.
Kwa nini vitabu 500?
Ukisoma vitabu 500 kwenye field yoyote ile utakuwa moja kati ya watu bora sana duniani.
Ukisoma vitabu 100-200 unaanza kujua ni nini cha kufanya.
Ukisoma vitabu 200-300 unaanza kupata kipato kupitia eneo ulilochagua.
Ukisoma vitabu 300-400 unakuwa bora na kipato kinaimarika.
Ukisoma vitabu 400-500 na unakuwa kwenye 1% ya watu wenye mafanikio sana duniani.
Ukiendelea kusoma zaidi ya hapo unaendelea kuwa juu zaidi.
Utapata wapi muda wa kusoma vitabu vyote hivi?
1. Utapunguza muda unaotumia kwenye mitandao ya kijamii na utaachana na baadhi ya mitandao hii.
2. Utacha kuangalia movie au tamthilia ya aina yoyote.
3. Utaacha kukaa vijiweni na kupiga story za kulalamika au zisizo na msaada kwako.
4. Utaacha kutumia simu yako kuchat mambo yasiyo ya msingi.
Kwa kufanya hivi utapata zaidi ya masaa mawili ya ziada kila siku.
Je upo tayari? Kama ndio nimeanzisha group maalum la telegram ambapo tutakuwa tunashare vitabu tunavyosoma.

Ili kuweza kuingia kwenye kundi hili la kusoma vitabu unahitaji kuwa unatumia TELEGRAM, kama hujui telegram ni application ambayo inafanana na WHATSAPP hivyo nenda kwenye PLAY STORE na search telegram download na install kisha sajili kwa namba yako ya simu kama ulivyofanya kwenye WASAP.

Baada ya kuwa na application hii nitumie mesej kwenye telegram kwa namba yangu 0717396253 na uniambie majina yako na kwamba unataka kuingia kwenye vitabu 500.

Nafasi za kuwepo kwenye group hilo ni chache hivyo mwanachama yeyote ambaye hatakuwa active ataondolewa. Kwenye telegram unaweza kushare vitabu kwa ku-upload na kudownload.

Karibu sana na nakutakia kila la kheri katika kusoma vitabu hivi 500.

Kwa wale ambao watapenda kujifunza jinsi ya kuweza kujijengea tabia nzuri ya kujisomea unaweza kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA ambapo utajifunza mbinu nzuri za kuweza kusoma zaidi na kujifunza zaidi. Bonyeza hilo jina kupata maelezo zaidi.

N.B Kama hujawahi kusoma kitabu chochote ukakimaliza tafadhali usinitafute.

Kumbuka kujifunza kila siku ndio hitaji la msingi la kufikia mafanikio, jipatie memory card ya vitabu na pia jiunge na KISIMA CHA MAARIFA ili kupata maarifa ya kuweza kukufikisha kwenye mafanikio makubwa.

Nakutakia kila la kheri, TUKO PAMOJA.