Moja ya njia rahisi sana ya kupata maarifa kutoka kwa watu wengine ni tabia ya kupenda kujisomea. Kujisomea vitabu kunakupa mambo mengi sana yatakayokufikiasha kwenye mafanikio.
Kama utajijengea tabia ya kujisomea, mambo haya matano yatatokea;
1. Utapata maarifa zaidi.
Kwa kujenga tabia ya kujisomea utapata maarifa mbalimbali kutoka kwa waandishi mablimbali. Maarifa haya ndiyo yatakayokuwezesha kufanya kazi au biashara yako kwa ufanisi mkubwa.
2. Utakuwa mbunifu.
Unapokuwa na tabia ya kujisomea unaifanya akili yako kufikiri zaidi na hata kutengeneza taswira mbalimbali. Hii hukufanya kuwa mbunifu zaidi.
3. Utajua vitu vingi.
Kama utasoma vitabu vingi hakuna ubishi kwamba utajua vitu vingi. Iwe ni kuhusu kazi au biashara unayofanya au hata mambo ya kawaida kama historia au sayansi. Unapojua mambo mengi zaidi ndio unaongeza nafasi yako ya kufanikiwa.
4. Unaondoa msongo wa mawazo.
Tabia ya kupenda kujisomea itakuwezesha kuondoa msongo wa mawazo na hivyo kuwa na mawazo mazuri. Hii ni kwa sababu unaposoma unasahau mawazo yanayokusonga na kupata mawazo mapya. Hivyo badala ya kukimbilia pombe au madawa unapokuwa na msongo, chukua kitabu kizuri na usome.
5. Utafurahia foleni au kusubiri.
Mara nyingi huwa tunakuwa kwenye foleni mbalimbali, labda foleni ya magari au foleni ya kupata huduma fulani. Na kuna uwezekano mkubwa unachukua sana foleni hizi. Au kuna wakati mnakubaliana na mtu mkutane muda fulani, halafu yeye anachelewa, hivyo unajikuta unachukua. Ukiwa na tabia ya kujisomea utagundua muda wa foleni au kusubiri ni muda mzuri wa wewe kuchukua kitabu chako na kuanza kusoma.
Anza sasa kujijengea tabia ya kujisomea. Kama bado una uvivu wa kujisomea karibu kwenye kundi la kujisomea ambapo utapata kitabu cha kujisomea kila wiki.
Kuingia kwenye kundi hilo Download application inayoitwa TELEGRAM MESSENGER na kisha nitumie mesej kwa telegram kwenye namba 0717396253 na kuniambia unataka kuingia kwenye kundi la kusoma vitabu.
Nakutakia kila la kheri kweye usomaji,
TUKO PAMOJA.