Ushauri Kwa Lady Jaydee, Wasanii, Waandishi Na Wajasiriamali.

Siku chache zilizopita mwanamziki maarufu wa Tanzania Judith Wambura maarufu kwa jina la Lady Jaydee aliweka ujumbe kwenye mtandao wa facebook kwamba hayuko kwenye kipindi ambacho anaweza kutunga nyimbo. Ujumbe huo ulisomeka kama ifuatavyo;

Hiki ni kipindi ambacho siwezi kutunga/kuandika nyimbo, sina hisia zozote na nikilazimisha hazitakuwa nzuri,
Huwa nakaa hata miaka 3 au 5 pengine mwezi mmoja au miwili au 6 , yaani huwa haitabiriki, pale inapotokea tu ndio huwa.
Natumaini jibu hili ni muafaka na litawaridhisha walio uliza, Poleni kwa kusubiri, i wish ningeweza

Niliona linaweza kuwa tukio la kawaida kwake na hivyo sikufikiri sana kuhusu hilo mpaka nilipokutana na rafiki yangu siku chache baadae. Rafiki yangu huyu ni mwandishi na nilitaka kujua anaendeleaje kwenye uandishi, nae akanijibu hayupo kwenye wakati mzuri wa kuandika, yaani hajisikii kuandika na hata akijisukuma haoni kama anaandika kitu kizuri. Hapa niliona kuna tatizo na hivyo kuona umuhimu wa kutoa ushauri kwa watu hawa na kwako pia kama unakutana na hali kama hizi kwenye kazi zako.

Tatizo analopitia Jaydee, na huyo rafiki yangu, huenda na wewe pia linaitwa writer’s block. Yaani unakuwa kama mawazo yako yamebanwa na huwezi kufunguka kutoka hapo alipo. Ni tatizo linalowakumba watu wengi sana wanaofanya kazi zinazohitaji ubunifu na kufikiri sana.

Ili uweze kufikia mafanikio makubwa kupitia uandishi, usanii na hata kazi nyingine zinazohitaji ubunifu ni lazima uweze kupambana na changamoto hii ya kushindwa kuandika kwa kipindi fulani.

Unawezaje kupambana na changamoto hii?

Changamoto hii ilikuwa inanisumbua sana mimi mpaka nilipokutana na suluhusho moja linaloitwa The Sainfeld method. Jerry Sainfeld ni msanii maarufu wa vichekesho. Ameandika na kuigiza vichekesho vingi sana vilivyompelekea kuwa tajiri mkubwa sana duniani. Alipoulizwa kuhusu mafanikio yake kama mchekeshaji na anawezaje kuandika vichekesho vingi sana? Jerry alijibu kwamba kazi yake kubwa ni moja tu, kuandika kila siku. Anasema kila siku anajilazimisha kuandika iwe anajisikia au hajisikii. Katika kuandika huku kila siku anaandika vichekesho vingi, vingine vizuri, vingine vya kawaida. Hivyo kwa kuchukua tu vile vizuri bado anakuwa ameandika vichekesho vingi kuliko angetegemea kuandika wakati anajisikia kuandika.

Njia hii Jerry anaiita DON’T BREAK THE CHAIN, yaani usivunje mfululizo, na anashauri kuwa nakalenda kubwa ambapo mtu utaweka alama siku ambazo umeandika, hii inakupa motisha wa kutokukatisha mfululizo mzuri uliouanza.

sainfield method

Njia hii ni nzuri sana, mwanzoni inaweza kuonekana ngumu ila ukishazoea mambo yanakuwa yanamiminika yenyewe bila hata ya kujisukuma.

Kwa mfano mimi nilianza kuitumia kwenye kuandika kwa kuandika maneno 500 kwa siku. Mwanzo ilikuwa changamoto ila hatimaye nikaweza kuwa naandika maneno yasiyopungua 500 kwa siku. Sasa hivi naandika maneno yasiyopungua 1000 kila siku, mara nyingine yanafika 3000 mpaka 5000. Sheria yangu ni moja, kuamka asubuhi na mapema, kusoma kwa nusu saa au saa moja na kuandika kwa dakika 90, baada ya hapo ndio naweza kufanya mambo mengine.

Njia hii imenisaidia sana na sijawahi kukosa kitu cha kuandika, naamini itakusaidia pia na wewe ambaye unafanya kazi ya ubunifu au uandishi.

Kumbuka watu waliobobea na kufanikiwa kwenye kitu fulani hawasuburi kujisikia ndio wafanye, bali hujilazimisha kufanya hata kama hawajisikii.

Ili kujenga tabia hii unahitaji pia kujijengea nidhamu binafsi na kujiamini binafsi. Unaweza kujifunza jinsi ya kujijengea tabia hizi kwenye KISIMA CHA MAARIFA. Bonyeza maandishi hayo kujua JINSI YA KUJIUNGA NA KISIMA CHA MAARIFA 

Nakutakia kila la kheri katika safari yako ya kufikia mafanikio makubwa.

TUKO PAMOJA.

Kama una changamoto ambayo inakuzuia kufikia malengo yako unaweza kuitoa kwa kubonyeza maandishi haya na kujaza fomu. Changamoto yako inaweza kuwa moja makala zijazo kila siku ya jumatatu. Kama unahitaji ushauri wa haraka wasiliana na mimi kwa kwa email amakirita@gmail.com au simu 0717396253/0755953887.

kitabu-kava-tangazo432

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s