TOFAUTI 17 Kati Ya Matajiri na Masikini(kwa nini masikini wanaendelea kuwa masikini na matajiri kuendelea kutajirika)

Unajua kwa nini masikini wanaendelea kuwa masikini na matajiri wanaendelea kutajirika?

Hongera sana, leo utajua hapa;

1. Matajiri wanaamini wanatengeneza maisha yao, wakati masikini wanaamini maisha yanatokea.

2. Matajiri wanacheza mchezo wa fedha ili kushinda, masikini wanacheza mchezo huu ili kutopoteza,na mwishowe hawashindi.

3. Matajiri wamejitoa kweli na wana nia ya dhati ya kuwa matajiri, masikini wanatamani kuwa matajiri.

4. Matajiri wanafikiri vikubwa, masikini wanafikiri vidogo.

5. Matajiri wanaweka akili zao kwenye fursa, masikini wanaweka akili zao kwenye vikwazo.

6. Matajiri wanawapenda matajiri wenzao na watu waliofanikiwa, masikini wanawachukia na kuwaonea husuda matajiri.

7. Matajiri wanakaa na watu wenye mtizamo chanya na waliofanikiwa, masikini wanakaa na watu wenye mtizamo hasi na wasiofanikiwa.

8. Matajiri wako tayari kujitangaza, masikini wanaona aibu kujitangaza.

9. Matajiri ni wakubwa zaidi ya matatizo yao, masikini ni wadogo zaidi ya matatizo yao.

10. Matajiri ni wapokeaji wazuri, Masikini sio wapokeaji wazuri.

11. Matajiri wanachagua kulipwa kulingana na matokeo wanayozalisha, masikini wanachagua kulipwa kutokana na muda.

12. Matajiri wanafikiri kupata vyote, masikini wanafikiri kupata kimoja na kukosa kingine.

13. Matajiri wanalenga kwenye utajiri wao, masikini wanalenga kwenye kipato chao.

14. Matajiri wana usimamizi mzuri wa fedha zao, masikini wana usimamizi mbovu wa fedha zao.

15. Matajiri wanafanyiwa kazi na fedha zao, masikini wanazifanyia fedha kazi.

16. Matajiri wanachukua hatua licha ya kuwa na hofu, masikini wanakubali hofu iwatawale na kuwazuia kuchukua hatua.

17. Matajiri kila mara wanajifunza na kukua zaidi, masikini wanafikiri wanajua kila kitu.

Unaweza kujifunza zaidi kuhusu mambo haya kwenye kitabu SECRETES OF MILLIONAIRE MIND.

Kupata kitabu hiki  SECRETS OF MILLIONAIRE MIND jiunge na mtandao huu kwa kubonyeza maandishi haya na kuweka email yako.

Nakutakia kila la kheri kwenye safari ya mafanikio.

TUKO PAMOJA.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s